Mkandarasi wa Barabara ya Boko Kupitia Ununio Hafai, Rami yayeyuka kama barafu

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,139
2,000
Bila kusita, namtangaza Mhandisi wa barabara ya Boko kupitia ununio kuwa hana kiwango cha kutengeneza barabara za karibu na ufukwe, au hana kiwango kabisa, nashangaa hawa waandisi wa Tanroad wanakagua nini, ikiwa tayari kuna mashimo madogo mengi na lami imeoshwa na mvua ya juzi ya masaa matatu. karibu na nguzo za kwenda zanzibar hapo unaweza kula mweleka mbaya sana kwani barabara ina manundu kama vichuguu vya babati. barabara inateleza sana.
Mheshiwa Magufuri sitanii nenda kajionee mwenyewe kabla hawajakomba vi-ela vyetu vya kodi na kukimbia.
Kwa wale wote wenye mataili vipara msidhubutu kupita huku hatuna ambulance za wagonjwa.
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,180
1,250
Daaah ndiyo nchi yetu usifikiri Tanroads hawajui ila 10% hapo ndiyo inayofanya yote hayo.
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,139
2,000
kama mtu amepitia hapa aseme ukweli au tusubiri vifo vya watu wasio na hatia kwa sababu ya utelezi, mashimo. Nasikia Mwakwembe anaishi karibu na uko, naomba apitie hata kama haimhusu ili hamjulishe Dkt. Pombe
 

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
4,124
2,000
Hii ndiyo Tanzania, ikiwa kama barabara inayotumiwa na Mawaziri, viongozi wa Kimataifa pindi wanapokwenda kwenye hoteli n.k imechakachuliwa hivyo, je zile barabara za pembezoni zina viwango gani? Ikumbukwe hata barabara ya Kilwa ilirudiwa ujenzi baada ya kukataliwa na Magufuli.
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,139
2,000
angalia barabara ya kijitonyama mpaka kona ya peace club nayo bomu kweli kweli, hivi hawa watu huwa hawapimwi kwanza kwa kijisehemu kidogo kuliko kuharibu fedha zetu.
 

masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
14,710
2,000
Hiyo iliyochakachua barabara kampuni inaitwa Badr East Africa Ent. Ltd

Jamaa hawa ni makanjanja wa kutupwa na kila wanapopewa kazi wana vurunda.
Nasikia sina uhakika kuwa kuna mkono wa wasomali humo.

Kazi hiyo nimepata fununu walipewa na meneja wa Tanroads ambaye amehamishwa tayari.
Habari zinatonya kuwa hao Badr tenda yao ilikuwa chini sana kuliko makadirio lakini bado wakapewa kazi hiyo.
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,139
2,000
inaniuma sana kuona JK anasifiwa kwa kuweka barabara nyingi sana huku nyuma ya pazia zikimomonyo na mvua ya siku mbili, inabidi tuweke mikakati ya kuzuia makandarasi feki wanaotengeneza barabara kwa masaa, mfano mkandarasi anayehudumia barabara ya mwananyamala hospital naye mhmmmm, barabara ya kinondoni mpaka surrender , kila mara MAn At WORK isiyoisha au ndio kula kwao.
 

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,383
2,000
Jamaa yangu alikula mweleka na Rav4 yake kwenye kona mita chache toka Ununio kama unaelekea Kunduchi. Hii barabara nashauri usiendeshe zaidi ya speed 40kph. Ni hatari!!!
 
Top Bottom