Mkandarasi anayejenga lami Kigamboni baada ya daraja (Mnadani) hazingatii kanuni za ujenzi; ni kero kubwa kwa wapita njia

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Mkandarasi aliyepewa kumalizia kuweka lami eneo korofi baada ya kuvuka daraja la Kigamboni (Mnadani) amegeuka kero kubwa Sana kutokana na staili yake ya ujenzi usiozingatia kanuni za ujenzi!
  • Kanuni za ujenzi zinamtaka Mkandarasi kutumia Alama na michoro (posters) kutoa maelekezo kwa watumia barabara LAKINI HUYU hazingatii Hilo
  • Kanuni za ujenzi zinamtaka Mkandarasi kuandaa njia mbadala (njia mchepuko) kabla ya kufunga barabara, Huyu Mkandarasi hazingatii hili Wakati wowote anafunga barabara pasipo kuandaa/ kutoa maelekezo ya njia nyingine mbadala (mchepuko) kwa watumiaji wa barabara!
  • Mkandarasi anatumia Vifusi na mawe kufunga barabara pasipo kuweka (Reflection sign ) kwa watembea usiku.
  • Mkandarasi Huyu pamoja na kutambua kwamba eneo like Ni (busy area) lakini hafanyi kazi weekend wala USIKU zaidi ya kufunga njia na kuondoka Jambo linalosababisha kero kwa watumiaji wengine wa barabara.
IMG_20200713_194406_669.jpg

Tanroad/Tarura/RTO/DTO Mambo Kama haya mwisho wa siku ndiyo huchangia wananchi Kushambulia wajenga barabara!
 
Hilo hata mimi nimeliona. Jamaaa hawajali chochote,wanafunga barabara watakavyo huku wakijua hakuna njia mbadala labda uwe mwenyeji sana wa maeneo hayo. Mfano Jana wamefunga njia usiku bila taarifa watu wamehangaika sana.
 
Wapuuzi sana
 
Alama za divertion hakuna, wala huo mchepua hawaupangilii na kuandaa kufikia mashimo! yaani ni shagala bagala.
 
Alama za divertion hakuna, wala huo mchepua hawaupangilii na kuandaa kufikia mashimo! yaani Ni shagala bagala
Wendawazimu hawa jamaa kama ulivyosema kuna siku watachezea kichapo.
 
Kama unatokea daraja la nyerere mbele kidogo kushoto kuna chocho la kwenda kutokea kule karibu na geti la nevy
 
Yaani wanafanya kazi kiboss hata mimi nimeshangaa. Weekend wanalala siku za kaz wanaanza saa mbili asubuhi, usiku wanalala. Nadhan atakuwa mkandarasi mzalendo.
 
Huyo mkandarasi nakuja kumtoa sasa hivi namweka mwingine we subiria uone
 
Wanashindwa na MECCO wamemaliza kipande cha Kisiwani-Kibada vizuri tu.
hao jamaa wahuni Sana! wanadindwa hata kujenga upande mmoja mmoja ....zaidi wanaruka ruka Mara huku mara kule,
 
Back
Top Bottom