Mkandala ajiuzulu?

kamtu

Member
Mar 12, 2008
51
0
Kutokana na migogoro ya mara kwa mara inayotokwea chuo kikuu cha Dar es salaam nimefanya uchunguzi na kuongea na makundi mbalimbali ya wanafunzi walimu na wafanyakazi ambao kiujumla wanaelekeza lawama kwa Prof Mkandala kwamba anaendesha chuo kibabe, amejaa dharau na kiburi na pia ni mkabila,niliamua kufanya uchunguzi huu baada ya kuona siku moja kwenye kipindi cha jennerali on mondayvijana walipokuwa wanaongelea jinsi management inavyoingilia maswala ya wanafunzi na kusababisha matatizo. kilichoyokea ni kwamba Mkandala alipiga simu na kuomba waitwe wao pia, na generali akamjibu ile sio Jerry Springle show?? Kwa kweli nilistaajabu sana jinsi Prof anayojishushia heshima badala ya kusolve matatizo anataka aitwe kenye tv kubishana na kujibizana na wanafunzi. Kutokana na maoni ya wengi wanaona hawezi kuendesha chuo hata mimi naunga mkono, wenzangu nyie mnaonaje kwa maoni yenu? AENDEEEEEEEEEEEEE?
 
Sidhani kama ataenda kama Kikwete asipomtosa ila nakuunga mkono kuwa mafisadi na madikiteta kama Mukandala hawatakiwi kabisa kuwa na nafasi za uongozi kwenye chuo kikuu chochote hapo TZ.
 
Kutokana na migogoro ya mara kwa mara inayotokwea chuo kikuu cha Dar es salaam nimefanya uchunguzi na kuongea na makundi mbalimbali ya wanafunzi walimu na wafanyakazi ambao kiujumla wanaelekeza lawama kwa Prof Mkandala kwamba anaendesha chuo kibabe, amejaa dharau na kiburi na pia ni mkabila,niliamua kufanya uchunguzi huu baada ya kuona siku moja kwenye kipindi cha jennerali on mondayvijana walipokuwa wanaongelea jinsi management inavyoingilia maswala ya wanafunzi na kusababisha matatizo. kilichoyokea ni kwamba Mkandala alipiga simu na kuomba waitwe wao pia, na generali akamjibu ile sio Jerry Springle show?? Kwa kweli nilistaajabu sana jinsi Prof anayojishushia heshima badala ya kusolve matatizo anataka aitwe kenye tv kubishana na kujibizana na wanafunzi. Kutokana na maoni ya wengi wanaona hawezi kuendesha chuo hata mimi naunga mkono, wenzangu nyie mnaonaje kwa maoni yenu? AENDEEEEEEEEEEEEE?

Kama aliomba kutoa his side of the story na hakupewa aurtime than that is wrong and against all kinds of journalistic ethics. A story is incomplete until the other side is given a chance to air its version.
 
Kwa hakika tunayo haki ya kusikia upande wa Mukandara katika hili sakata ili tuweze kuwa na balanced impression. Na kama Mukandara ni kweli aliomba kuitwa kwenye hiyo dialogue, alifanya vema sana na alidhihirisha yuko tayari kwa mdahalo. Walipaswa wawaweke kwenye mdahalo tena laivu kwenye TV tuone na tusikie madai ya wanafunzi na majibu ya Mukandara, mbele ya watazamaji nchi nzima nina hakika kila upande ungeongea kwa adabu na hakuna ambaye angeogopa kunyanyaswa, maana unyanyasaji wowote ungeonekana laivu na watazamaji wangepiga simu kutoa reactions zao. Hapo tungepambanua kweli kati ya mchele na pumba.

Kwa mtazamo wangu hadi sasa kuna watu wamepenyeza siasa za fujo huko chuoni na wanataka kukifanya kisitawalike. Hayo malalamiko ya wanafunzi ya mambo ya maji, umeme, lifti nk ni matatizo ambayo yako nchi nzima, na yangeweza kupunguzwa ama kuondolewa kwa kupitia njia muafaka na kuwa na subira. Mambo ya uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi pia ni immaterial, hakuna issues zozote za maana hapo. Kuna watu wana ugomvi binafsi na Mukandara, na ni ugomvi hasa wa kisiasa, wanapenyeza sumu hizo kwa wanafunzi. Utaona baadhi ya posts zilizowekwa hapa JF kuhusu mgomo wa UDSM zimetaja REDET ya Mukandara kama vile inahusika na mgomo huo! Fanya tu uchambuzi, tafuta neno REDET kwenye mijadala yote iliyoko hapa JF inayohusu mgomo wa UDSM, utaelewa namaanisha nini. Kuna watu wanaodhani kuwa wameumizwa kisiasa na hiyo REDET ambayo Mukandara alikuwa mkuu wake kabla ya kuwa VC, wameamua kwenda "kumwaga tindikali" huko chuoni! Lakini kwa bahati mbaya, wanaoumia ni watoto wa wanyonge, wengi wao wako tayari kustahimili matatizo waipate elimu wanayoitafuta hapo kwa matumaini kuwa itawakomboa kimaisha. Ndio maana katika mgomo huo, kuna wanafunzi waliokataa kugoma baada ya kuona mgomo hauna maslahi kwao, lakini hawa mamluki waliwafuata madarasani na kuwatisha, katika kuwalazimisha waingie kwenye mgomo.

Mimi nasema Mukandara aendelee kufanya kazi yake kwa kujibu wa kanuni zilizopo. Kama kuna makosa anayofanya, zitumike taratibu za kisheria kuyabaini, na yakidhihirika hatua zichukuliwe. Na serikali inapaswa kutumia mamlaka yake kulinda wananchi wake wote, kwa hiyo wanaosababisha fujo chuoni watafutwe na wakibainika sheria ichukue mkondo wake.

Haki ya wanafunzi fulani kugoma haipaswi kuingilia haki ya wanafunzi wengine ya kusoma. Anayetaka kugoma kwa maelezo kuwa ni haki yake, agome, lakini asiingilie haki ya mwenzie kukataa kushiriki mgomo huo. Kuna wanafunzi hapo masikini sana ambao wanaona elimu ni fursa pekee ambayo pengine "itawatoa", sasa mamluki wa migomo (ambaye pengine ameshafaidika na hela za ufisadi) anapokuja kuwaharibia wenzie matumaini yao ni jambo lisilovumilika hata kidogo.
 
Kama aliomba kutoa his side of the story na hakupewa aurtime than that is wrong and against all kinds of journalistic ethics. A story is incomplete until the other side is given a chance to air its version.

Pundit! Huyu bwana yuko nyumbani, amepiga simu wakati kipindi kinaendelea, hivi kweli alitegemea wamsubiri mpaka afike? Kama alitaka apewe nafasi ya kujieleza siku nyingine si angemtumia ujumbe producer wa hiyo show? kama alivyojibiwa, pale si mahali ambapo protagonists wanapambanishwa ili kufurahisha jamii. Naamini kuna TV stations kibao ambapo anaweza kupewa nafasi ya kujieleza kama kweli anataka kufanya hivyo na si kuwashikisha adabu wanafunzi.
 
kazi ipo,,UD bwana sio kandara tu hata Prof Osoro wa Economics nae ajiuzulu maana anafelisha watu kisa wanawake wakati ni mzee kabisa
 
Mimi sijaona kosa alilolifanya profesa Rwekaza Symphonia Mukandala sanasana ni ushabiki tu. Na hapo ukiangalia majority ya hao wanafunzi wanaogoma utakuta ni first year ambao wanatumiwa kama chambo. Mukandala ana sifa nzuri ya uongozi ukiachilia mbali REDET ameshashika nyadhifa ya ukuu wa idara yaani department of political science and public Administration Pia ameshakuwa mkuu wa kitengo cha sayansi ya jamii yaani Faculty of Arts and socialscience. Ni mtu mwenye nidhamu ya hali ya juu mchapa kazi na asiyependa majungu asiye na makuu hata chembe. Nimemjua yeye kama mwalimu wangu nikiwa chuoni na katika miaka yote sikuwahi kusikia kashfa yoyote inayomhusu. Napenda kukubaliana na mdau aliyeposti hiyo thread kuwa ni kweli anayoyasema na ninamuunga mkono. Kinachofanyika hapo ni njia za makusudi zinazolenga kumdhalilisha yeye binafsi pamoja na familia yake Mukandala kama Mukandala ni figure na UVC ni kitu kingine mbona haya hatukuyasikia kabla ya kuupata huo ukuu wa chuo? Na kama REDET inaipendelea serikali kama taasisi huru inayofanya tafiti zake kwa madai kuwa inakipendelea chama tawala ziko wapi hizo tafiti zingine ili kubatilisha? Ni lazima tukubaliane kwa hoja chuo kikuu ni taasisi ya umma iliyowekwa kwa ajili ya kuwasaidia wote watu wameyasahau yale maneno ya Nyerere na ninadhani hawayasomi tena yamebandikwa hata pale Cafeteria au DARUSO. Wamekuwa malimbukeni wa siasa pamoja na ushabiki unaochochea chuki hasira na ubinafsi huku taifa likiingia hasara. Ufisadi kama ufisadi ulikuwepo katika awamu zote za uongozi katika nchi yetu na wale walioanza kuliharibu taifa letu katika hatua za msingi na za awali wamegeuka kuwa wapinzani kwani siri zote wanazijua.Adui yako sio mtu wa mbali ni yuleyule unayekula kunywa na kucheka naye. MWACHENI MUKANDALA AKIONGOZE CHUO.
 
Mkandala ana kiburi, dharau,ukabila. ni mtu ambae hataki kufanya suluhu, ila anapendelea zaidi kukomoa na kushindana na wanafunzi ambao hata hawana degree wakati yeye ni profesa. hivi baba anaweza kuwa anawakomoa watoto wake, si yeye angekuwa na uelewa mkubwa zaidi? mukandala anatakiwa kuwa na uelewa mkubwa kuliko wanafunzi watoto wale. asifanye kama kuwakomoa, awasaidie.hata kama wamekosea, ajue tz bila wasomi wa kesho itahangaika. hivyo badala ya kufurahia kufukuza wanafunzi, ni bora angafanya kitu watu tuone yeye ni wa tofauti na wanafunzi. kukomoana na madent inaonyesha yeye ana akili sawa tu na za watoto wa shule ambao hawana hata degree bado. alitakiwa kufanya suluhu,diplomacy. siku zote profesa huyo amesifika kwa ukatili,kukomoa na kiburi. hata alipokuwa anafundisha. hakuna asiyemjua. ilipofika kuwa yeye ni swahiba wa JK tangu kipindi kile cha uchaguzi, basi tena. anajiona yeye ndo mtu wa ikulu. mimi nilishamaliza hapo chuo mda. bora hata luhanga alikuwa mtu. huyo hapo hafai. anaharibu chuo. yeye na Jumanne magimbi wake, hawana mawazo ya kiuprofesa.

kilichokuwa kinatakiwa ni kukaa na wanafunzi kujadili na kufikia suluhisho ili kila mtu dukuduku liishe moyoni. kitendo cha yeye kuwafukuza wanafunzi na kuonyesha jeuri, sawa, wanafunzi wameacha fujo, lakini dukuduku liko moyoni. nidham ya uoga hiyo. siku likija kulipuka, mzigo uko palepale. dukuduku likikaa moyoni huzaa mengi. ndo maana watu hufikia hata kiwango cha kujitoa muhanga. kwasababu walikuwa na dukuduku moyoni mda. sasa yeye anafikiri wanafunzi wa udsm ni vichanga kwamba hawajui kwanini wanaandamana?hivi yeye anafikiri nguvu hufanya suluhisho?nasikitika sana.
 
kwenye sentensi yako ya kwanza umeweka neno ukabila, lakini katika hoja zako sijaona ni wapi umeeleza kuwa amependelea kabila fulani. usirise hoja ambao hautaiongelea kwenye utetezi wako. pia wakati wa kugoma sikusikia hoja kama hiyo, hta vile, wale waliofikishwa mahakamani niliona majina ya kabila lake. huu sio muda wa kubwata tukakunyamazia. sisi wote ni watanzania na kosa la mtu haliwezi kumtia hatiani jamii fulani. kama huna point usiongee.
 
Inasikitisha sana kuona kuwa Mkandala kashindwa kuendesha chuo.Hilo ndio lilikuwa tarajio langu.Tatizo kubwa ni kupena nafasi kwa upendeleo.Mkandala kapata nafasi hii kutokana na baraka za JK.
Hapa USA vyuo makini vinamtafuta raisi wa chuo kwa muda mrefu na anahulizwa nini jipya atakifanyia chuo.Inabidi na sisi tuige mfumo huo.Inabidi chuo kikuu kiendeshwe na mtu yeyote as long ana management skills.
Kwa yaliotokea UD mie naona ni wakati wa Mkandala kwenda kuwa may mkuu wa wilaya.
 
Kutokana na migogoro ya mara kwa mara inayotokwea chuo kikuu cha Dar es salaam nimefanya uchunguzi na kuongea na makundi mbalimbali ya wanafunzi walimu na wafanyakazi ambao kiujumla wanaelekeza lawama kwa Prof Mkandala kwamba anaendesha chuo kibabe, amejaa dharau na kiburi na pia ni mkabila,niliamua kufanya uchunguzi huu baada ya kuona siku moja kwenye kipindi cha jennerali on mondayvijana walipokuwa wanaongelea jinsi management inavyoingilia maswala ya wanafunzi na kusababisha matatizo. kilichoyokea ni kwamba Mkandala alipiga simu na kuomba waitwe wao pia, na generali akamjibu ile sio Jerry Springle show?? Kwa kweli nilistaajabu sana jinsi Prof anayojishushia heshima badala ya kusolve matatizo anataka aitwe kenye tv kubishana na kujibizana na wanafunzi. Kutokana na maoni ya wengi wanaona hawezi kuendesha chuo hata mimi naunga mkono, wenzangu nyie mnaonaje kwa maoni yenu? AENDEEEEEEEEEEEEE?

Huyu Professor wa kubahatisha mwenye U-VC wa kupewa anapaswa kutimuliwa. Manake kujiuzulu haitoshi. Pia nashauri kuwa chuo kikuu sasa kisiwe ni jukwaa la siasa ambapo kila rais anajitundikia mtu wake. Mimi nafikiri sasa maprofessa wa chuo kikuu pamoja na council wapewe rungu la kupiga kura as to who awe VC. Hii mambo ya mtu kupewa U-VC na presidaaa, ndio inaleta maswala ya mtu kutetea maslahi ya serikali na ya kwake binafsi instead ya wanafunzi. Ila hii ya Mukandala imezidi. Manake wakati wa papaa Luhanga, jamaa alikuwa anatetea serikali ila kidesign kiasi watu walikuwa hawashtukii kirahiiiiiiiiisi. Na pia mshikaji alikuwa anakaa kimya, hakurupuki. Sasa huyu jamaa sifa zimemjaa sana, anataka ubishi usiokuwa wa msingi badala ya kusolve matatizo ya wanafunzi.

Haka kaprofessa katoke tu..!! Kanakera..!!
 
na sikia kuwa sio kwamba rais aliamuka tu na kutangaza jina la VC. aripigiwa kura mbona nasikia hapo chuo, then wanapeleka majina 2 kwa JK kuchukua moja, sijui kama irikuwa kula ya wazi na alifanya kampeni au irikuwaje
 
Tulia upewe siri ambayo inaelekea huijui hata kidogo..!!

Kwa madai ya wadau wa ndani, selection ya VC ilifanywa na kampuni moja inayoitwa Deloitte. Katika selection hiyo, jamaa alipigwa chini..!! Na ndipo selection ikarudiwa..!! Una habari hiyoo..!! ..??

Fanya uchunguzi..!! Na kama nimedanganywa, unifafanulie..!!
 
Sijui maana hata mimi nirisikia kutoka kwa mutu wa hapo yeye ndi alipata nafasi ya 2, nasikia arikuwa na uhakika wa kupata hiyo nafasi kwani arikuwa kiongozi hapo kwa mda mrefu ingawaje anasema watu warimchukia eti na kumwita dikteta katika enzi yake na anaamini hiyo nafasi ingekuwa yake mambo yangekuwa tofauti.
 
Mkandara anasikitisha sana.Ni aibu kuona mtu ambaye alikuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanyonge akifanya ubabe pale UDSM.
Nilitarajia mabadiliko makubwa pale UDSM wakati Mkandara alipopewa nafasi ile,ila kwa sasa inatia hata huruma.Hakuna jipya,mambo ni yaleyale tena hata mazuri yaliyofanywa na Prof.Luhanga yanaelekea kupotea.Mkandara kaacha kutumia taaluma yake na ameweka siasa na maslahi ya chama badala ya maslahi ya Taifa.
Ni aibu kuu kwa chuo chetu kikuu kukosa maji safi.Picha tunayoipata kutoka chuo kikuu ni kwamba serikali na Mkandara wake haioni tena umuhimu wa kuwa na wataalum wa ndani kutoka nchini mwetu.Kama serikali yetu kweli imedhamiria kuleta mabadiliko ya kiuchumi inabidi kuwekeza kwa vijana wetu na siyo kutumia ubabe na kutuwekea watu kama Mkandara kuongoza kitengo hicho nyeti kwa Taifa letu ambao kila kukicha wanaendesha magari ya mamilioni ya fedha wakati chuo chetu kikuu hakina maji safi,madarasa ya kutosha na mbaya zaidi bado hawaoni kama kuna matatizo yoyote na kuyakubali na kuyafanyia kazi.

Mkandara jiuzulu mara moja!
 
Mi naona viwango vya ku-judge utendaji wa mkandara vinatofautiana lakini turudi katika hali halisi na hadhi ya UD, KIDZOGOLAE ungekuwa wewe ndio VC pale UD ungekuweza kukaa na kujadiliana matatizo ya wale wanafunzi pasipo wao kuyawasilisha through proper channels???

Kama wanafunzi wame-opt kufanya fujo kushinikiza mambo wanayodai hatimaye kusababisha uharibifu na kifo hiyo nafasi ya dialogue iko wapi?? Unajua unapokuwa mwanafunzi wa Chuo kikuu inabidi ujitofautishe sana na mwanafuzi wa sekondari hata kama atakuwa yuko A'level.

Vijana wetu wamekuwa viherehere wa mambo ya hovyo lakini hatujawahi hata siku moja kuwasikia wakifanya fujo kwa hoja za msingi zenye maslahi kwa taifa na watu wa kujenga taifa hili tunategemea watoke pale and other high learning institutions. Sasa nadhani tuwe makini kidogo na mambo haya may be ni vizuri wakati mwingine kuvisaidia hata ushauri hivi vitoto vinavyokwenda kusoma UD huenda havijui nafasi yao katika jamii wakiwa pale. Acheni Mkandala afanye kazi yake kwa taratibu zinazotakiwa huyo anaedai kuwa ni mkabila aweke ushahidi hapa tuufanyie kazi.

Na pia kama aliomba awe-invited kwenye huo mdahalo kwenye TV it was right na ingekuwa nafasi nzuri kwa wa-tz kusikia both sides katika huo mgororo then tungekuwa na nafasi nzuri ya ku-judge. Sasa kama wewe umewasikiliza wanafunzi tu walichosema wakati upande wa pili hujasikia then unatoa hukumu then you have serious problems..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom