Mkanda wa jeshi (HERPES ZOSTER/SHINGLES), Dalili na tiba yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkanda wa jeshi (HERPES ZOSTER/SHINGLES), Dalili na tiba yake

Discussion in 'JF Doctor' started by Shine, Dec 29, 2011.

 1. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wakuu muu hali gani naomba kujua kinachosababisha mkanda wa jeshi na indicator zake pia madhara yake na kami huu ugongwa una tiba
  Nawakilisha

  ===========================================================================================
  ===========================================================================================
   
 2. ldd

  ldd JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 792
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mm, in most cases hiv!
   
 3. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  unatokana na ngoma a.k.a ukimwi
   
 4. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  swali la nyongeza:mkanda wa jeshi unaitwaje kwa lugha ya kiingereza/medical language?nataka ni google ili nijielimishe zaidi juu ya hili gonjwa au sijui ni dalili ya ugonjwa?
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  NgumiJiwe, inaitwa herpeszoster (sina hakika na spellings) . Google.
  Mkanda wa jeshi ni shambulio la nerves by virus. Hii inatokana mostly na upungufu wa kinga mwilini either baada ya kuugua muda mrefu au baada ya stress ya muda mrefu. Magonjwa ya virusi hayana tiba zaidi ya kuu-boost mwili ili uweze kupambana zaidi. Hebu google kwa maelezo zaidi
   
 6. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  shukrani mkuu King'asti na ubarikiwe.Wacha nikajielimishe!
   
 7. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,183
  Trophy Points: 280
  Ukipata mkanda wa jeshi,kapime VIH.Haraka iwezekanavyo
   
 8. s

  stun Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ugonjwa wa mkanda wa jeshi (herpes zoster aka shingles) unasababishwa na virus anayeitwa Varecella zoster, huyu huwa anaingia mwilini mapema sana katika umri mdogo, anasababisha ugonjwa wa "chiken pox". Ugonjwa ambao huambatana na homa na vipele, ambayo huisha vyenyewe. Kuisha kwa chicken pox hakumaanishi kuwa Virus wameisha, bali huwa wanaenda kwenye sehemu za mwisho za mishipa ya fahamu (nerve endings) na huwa wanakaa humo na kuwa dormant, kwa maneno mwngine, kwa kuwa kinga ya mwili ingali juu, basi hawa wadudu hawana madhara, na ndo maana wanakimbilia kule kusikofikiwa kiurahisi na seli za kinga. Ikiwa kinga ya mwili inapungua kwa sababu yeyote ile ama kutokana na HIV/AIDS, advanced cancer, lishe duni, na nyingine,..basi hawa wadudu wanapata nguvu na kujitokeza from nerve endings walipokuwa. Wanasababisha painful blisters, na wanatambaa na mishipa ya fahamu,..ndio maana hizo blisters ama vidonda vinakuwa kama vinafata mstari, ama eneo husika. Mara nyingi mgongoni, kiunoni, kifuani, ama mabegani,..kwa kiswahili "mkanda wa jeshi" kwa kuwa ipo sehemu ambazo wanajeshi hufungia mkanda.

  Matibabu: mkanda wa jeshi hauna dawa,..bali huisha wenyewe ikiwa kinga inarejea, kwa hiyo dawa wanazopewa huwa ni kwa ajili ya maumivu tu,..wakati mwingine kuzuia infections za bacteria ambazo husababisha usaha, ama kupunguza tu idadi ya virusi kuzuia visizaliane zaidi.

  Madhara,..zaidi ya mabaka yanayodumu, sifahamu madhara mengine ukiacha maumivu makali. mara chache hushambulia macho na huweza kukufanya kuwa kipofu, ama kushambulia nerves zinazosaidia misuli, na kufanya ushindwe kutuimia kiungo husika
  Kupata mkanda wa jeshi hakuna maana kuwa Una UKIMWI,..ila wengi wanaopata haswa kwa mazingira yetu basi ni kweli wanakuwa na ukimwi, maana hiyo ndio sababu kuu ya kupunguza kinga ya mwili Tanzania

  Stun
   
 9. P

  PENCO New Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jitahidi kupima hiv
   
 10. salito

  salito JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  dah kazi nzuri sn brother,kwa upande wangu umenifungua mambo mengi ambayo sikuwa na ufahamu nayo,safi sn.
   
 11. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mimi niliambiwa mtu mwenye mkanda wa jeshi ana ngoma.
   
 12. s

  stun Member

  #12
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama by definition ngoma ni upungufu wa kinga mwilini, then yes..mkanda wa jeshi unahusiana na ngoma,..ila hausababishwi na ngoma
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu nashukuru kwa maelezo yako mazuri
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Inamaana ni kweli mtu mwenye mkanda wa jeshi atakuwa na ukimwi?
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Siyo wewe tu hata mimi na naamini tutakuwa wengi tuliyo elimika kutokana na yeye
   
 16. M

  Mbilimbili Senior Member

  #16
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni na majukumu wadau, nina kitu kinanisumbua akili yangu. Iko hivi: kwa muda wa karibia wiki mbili kuna mstari ulijitokeza juu ya kitovu, na unakua kila kunapokucha kukatiza kwenye tumbo. Je wataalamu huu ndio mwanzo wa kuwa na hili tatizo, au niondoe shaka juu ya hili?
   
 17. B

  BARRY JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  jionsia gani wewe?
   
 18. M

  Mbilimbili Senior Member

  #18
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanamme.
   
 19. ldd

  ldd JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 792
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  uo mkanda unawatokea wajawazito!!
   
 20. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  je una dalili gani zaidi? andika zaidi upate kueleweka! ni tovuni tu? ni vipelevipele au la! au umenenepa kitambi kinakutoka?:thinking:
   
Loading...