A
Anonymous
Guest
Mpango mkakati wa viongozi wa Chama cha mawakala wa Bima Tanzania(IAAT) kubakia madarakani baada ya muda wao kupita maradufu.
Uchaguzi wa viongozi wa chama cha mawakalla wa bima Tanzania (IAAT) ilibidi ufanyike tangu 2022 lakini umekuwa unapigwa danadana na hatimaye utafanyika Oktoba/23 mwaka huu ila kuna mpango kabambe wa kwenda kuipiga chini katiba ya chama na badala yake kutumia “kanuni za uchaguzi” zilizo kinyume kabisa na katiba ya chama.
Kamati ya uchaguzi ilivunjwa bila kufata utaratibu ulioainishwa kwenye katiba na bila wanachama kupewa maelezo ya kutosha. Wakiuliza - hakuna majibu.
Baada ya kuvunja Kamati ya uchaguzi, Sasa wanaambiwa Kamati Kuu( viongozi waliopo madarakani) ndio inaratibu uchaguzi mkuu unaopangwa kufanyika mwezi Oktoba/23 na hao hao viongozi waliopo madarakani na ambao pia ni wagombea mwaka huu. Kizungu hapo wanaita ‘conflict of interest’. Yaani, KANUNI UTUNGE WEWE, UCHAGUZI URATIBU WEWE, NA MGOMBEA NI WEWE!!!!!! Kali ya kufungia mwaka hii.🤣🤣
Twende kwenye fomu za maombi sasa. wameweka kigezo cha mgombea kupata wadhamini toka kanda mbali mbali za nchi wasiopungua 15. Cha kusikitisha muda wote wa miaka 6 wamekaa madarakani hawajaweza kuwaunganisha wanachama hata kwa kufanya semina, makongamano nk ili wanachama wafahamiane. Na zaidi ya hapo wameunda magroup mengi tofauti ya whatsapp kikanda, ili kucontrol wanachama wasijuane au kuwa na umoja. Ila wao magroup yote hayo wapo. Hivyo hii inawapa wao nafasi ya kupata wadhamini wengi na kirahisi kuliko wengine.
Hili ndio zito zaidi. Msimamizi wa uchaguzi wanachama hawajui aliteuliwa lini na ni nani. Hakuna taarifa rasmi yoyote kuhusu hili.
Haifahamiki kama huyo msamizi wa uchaguzi asiyefahamika ndiye atakaye hesabu kura zote peke yake maana hana kamati!!!! Jeshi la mtu mmoja. Au na Kamati Kuu = Wagombea nafasi za uongozi watahusika!!??
Kingine cha kustaajibisha & kushangaza zaidi kwenye hizo “kanuni za uchaguzi”, hakuna bodi ya usuluhishi/arbitration board. Hivyo, endapo wanachama hawataridhika na matokeo ya uchaguzi hawana pa kwenda, labda mahakamani. Kwa maneno mengine matokeo hayapingiki na uhakika wa uhalali wake umeshapasishwa.
Kwa kifupi, hizo “kanuni za Uchaguzi” na katiba havina uwiano hata kidogo kuhusu uchaguzi unavyopaswa kufanyika. (Viambatanishi vipo hapo chini)
Wanasheria tunaomba mtujibie SWALI:
Hivi kanuni za uchaguzi na katiba ya chama, kipi cha kuzingatiwa zaidi? Maana kwa maamuzi ya Mwenyekiti wa Chama hiki Bwana Sayi Daudi na katibu wake Esta Mwamafupa, mwaka huu uchaguzi utaongozwa na Kanuni walizotunga wao sio Katiba ya Chama inavyosema na ikumbukwe wao wenyewe ni wagombea tena mwaka huu. Kuna nini nyuma ya pazia?