Mkakati wa upinzani kuhamia CCM ili kumpinga Rais Magufuli ndani ya CCM unazidi kushika mizizi!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Kuna msemo wa kiingereza kwamba "if you cant fight them join them". Usemi huu umekuwa wazi baada ya Raisi Magufuli kuanzisha kampeni kubwa ya kuua siasa za upinzani nchini, na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa,. Lakini jambo ambalo CCM hawakutambua ni kwamba kwa kila mwanasiasa wa upinzani aliyejiunga na CCM kwa madai ya "kumuunga mkono Raisi Magufuli" walikuwa wakijichimbia kaburi wenyewe. Wale vipofu wenzangu walishangilia wapinzani kuingia CCM bila kuelewa kilichokuwa kikiendelea.

Matunda ya mkakati wa kumpinga Magufuli ndani ya CCM yenyewe yameanza kuonekana. Kundi linalompinga Magufuli ndani ya CCM limeongezeka na kuimarika. Vuguvugu la kumchimba Raisi Magufuli chini chini ndani ya CCM limepamba moto. Hili limefanya Raisi Magufuli aanze kubadilika na hata kuonekana kama anapunguza ukali kwa wale walio ndani ya CCM, na kutaka sana kuonyesha kwamba "tuko pamoja". Lakini labda sasa amechelewa mno.

Mara kadhaa Raisi Magufuli ameonyesha kuwaamini zaidi wale wanaotoka upinzani kuliko wale walio ndani ya CCM, akidhani uaminifu wao kwake ni mkubwa zaidi, jambo ambalo linazidi kumbomoa kwa upande wa walio ndani ya CCM. Katika hali ya kutaka kuwafurahisha kundi la "Lowasa ndani ya CCM" siku hizi ameanza kumsifia Lowasa ambaye wakati wa kampeni alifurahia kusikia akitukanwa na hata wakati fulani kumsema aache kuropoka. Jambo hili pia kaagiza lifanywe na viongozi wakuu wengine wa CCM. Mashambulizi ya hadharani dhidi ya Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu amepunguza kama sio kuacha kabisa. Ni wazi Raisi Magufuli ameanza kuingiwa na woga wa kupingwa au kutoungwa mkono ndani ya CCM. Jambo hili limeathiri hata hatua zilizochukuliwa katika ulinzi wake kama Raisi.

Kisichojulikana kwa sasa ni je, ikiwa upinzani dhidi ya Magufuli ndani ya CCM utafanikiwa kumuondoa Magufuli, wale waliohamia CCM toka upinzani watarudi tena nyumbani kwenye vyama vya upinzani? Wengi wanasema hapana, kwamba kwa kuwa lengo ni maendeleo ya nchi, wanaweza kufanya kile walichokuwa wanapigania ndani ya CCM.

Siasa za Tanzania ni wazi zitakuwa za kuvutia sana katika miaka saba ijayo, kama siyo miwili.
 
Kuna msemo wa kiingereza kwamba "if you cant fight them join them". Usemi huu umekuwa wazi baada ya Raisi Magufuli kuanzisha kampeni kubwa ya kuua siasa za upinzani nchini, na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa,. Lakini jambo ambalo CCM hawakutambua ni kwamba kwa kila mwanasiasa wa upinzani aliyejiunga na CCM kwa madai ya "kumuunga mkono Raisi Magufuli" walikuwa wakijichimbia kaburi wenyewe. Wale vipofu wenzangu walishangilia wapinzani kuingia CCM bila kuelewa kilichokuwa kikiendelea.

Matunda ya mkakati wa kumpinga Magufuli ndani ya CCM yenyewe yameanza kuonekana. Kundi linalompinga Magufuli ndani ya CCM limeongezeka na kuimarika. Vuguvugu la kumchimba Raisi Magufuli chini chini ndani ya CCM limepamba moto. Hili limefanya Raisi Magufuli aanze kubadilika na hata kuonekana kama anapunguza ukali kwa wale walio ndani ya CCM, na kutaka sana kuonyesha kwamba "tuko pamoja". Lakini labda sasa amechelewa mno.

Kisichojulikana kwa sasa ni je, ikiwa upinzani dhidi ya Magufuli ndani ya CCM utafanikiwa kumuondoa Magufuli, wale waliohamia CCM toka upinzani watarudi tena nyumbani kwenye vyama vya upinzani? Wengi wanasema hapana, kwamba kwa kuwa lengo ni maendeleo ya nchi, wanaweza kufanya kile walichokuwa wanapigania ndani ya CCM.

Siasa za Tanzania ni wazi zitrakuwa za kuvutia sana katika miaka saba ijayo.
NI rahisi kuanzisha vita lakini ni ngumu SANA kuimaliza
 
Hakuna upinzani mkubwa ndani ya ccm unaoweza kumuondoa Magufuli.

Katumia tril. 1.5 kutununua wacha tujazane huko tumpindue, hela tumelamba na vyeo katupa mwenyewe,

mwanafizikia Issac newton alisema "to every action there is equal and opposite reaction"

Namuona magu ametoa mimacho anasoma hii comenti , siyo Mimi hiyo ni kanuni ya kifizikia
 
Kuna msemo wa kiingereza kwamba "if you cant fight them join them". Usemi huu umekuwa wazi baada ya Raisi Magufuli kuanzisha kampeni kubwa ya kuua siasa za upinzani nchini, na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa,. Lakini jambo ambalo CCM hawakutambua ni kwamba kwa kila mwanasiasa wa upinzani aliyejiunga na CCM kwa madai ya "kumuunga mkono Raisi Magufuli" walikuwa wakijichimbia kaburi wenyewe. Wale vipofu wenzangu walishangilia wapinzani kuingia CCM bila kuelewa kilichokuwa kikiendelea.

Matunda ya mkakati wa kumpinga Magufuli ndani ya CCM yenyewe yameanza kuonekana. Kundi linalompinga Magufuli ndani ya CCM limeongezeka na kuimarika. Vuguvugu la kumchimba Raisi Magufuli chini chini ndani ya CCM limepamba moto. Hili limefanya Raisi Magufuli aanze kubadilika na hata kuonekana kama anapunguza ukali kwa wale walio ndani ya CCM, na kutaka sana kuonyesha kwamba "tuko pamoja". Lakini labda sasa amechelewa mno.

Kisichojulikana kwa sasa ni je, ikiwa upinzani dhidi ya Magufuli ndani ya CCM utafanikiwa kumuondoa Magufuli, wale waliohamia CCM toka upinzani watarudi tena nyumbani kwenye vyama vya upinzani? Wengi wanasema hapana, kwamba kwa kuwa lengo ni maendeleo ya nchi, wanaweza kufanya kile walichokuwa wanapigania ndani ya CCM.

Siasa za Tanzania ni wazi zitakuwa za kuvutia sana katika miaka saba ijayo.
1543835483951.png
 
Back
Top Bottom