Mkakati wa Kuwafelisha Waislam Kidato Cha Sita Wabainika

Status
Not open for further replies.
Hacha hizo waambie wakasome.Kama unazo unazo tu hata kama watatunga mtihani mgumu kiasi gani utafaulu tu.
 
Baraza la Mitihani la Taifa linafanya kazi kwa umakini sana.

Inapotokea kuna suala lolote la udanganyifu katika mitihani ambao unaweza kupelekea kufutiwa matokeo au kufungiwa kituo, huwa hawakurupuki.
1. Wanafungua faili, na wanalipeleka kwa wataalamu wa upelelezi wa makosa ya kughushi na udanganyigu. (Polisi Makao makuu)
2. Kitengo hiki kinafanya uchunguzi na kikikamilisha uchunguzi wake kinashauri Baraza kama kuna udanganyifu au la.
3. Baraza linachukua hatua.
4. Baraza linatunza mafaili ya upelelezi kama ushahidi kwa watakaodhani haki haikutendeka.

Vielelezo hivyo na mafaili vipo, na endapo Shule yoyote au kikundi chochote kinadhani kina sababu za kutosha za kupinga hatua za baraza, kuna utaratibu unaoweza kufanyika wa hata wao kwenda pale na kuoneshwa ushahidi huo.

Tume nyingi tu zimeshaundwa kushughulikia malalamiko kadhaa yaliyokwisha tolewa kuhusu utendaji wa baraza, lakini zote zimetoka zimeridhika na utendaji huo.

Hivi karibuni, Wanasiasa na wanaharakati wa Zanzibar walikaribishwa na Baraza kujionea udanganyifu uliofanywa na watoto wa Sekondari za Zanzibar ambao ulipelekea kufutwa kwa matokeo ya wanafunzi 1200. Wanasiasa hao na wanaharakati walitoka wameridhika, kama inavyoonesha kauli hii ambayo Waziri wa Elimu wa Zanzibar aliitoa kwenye Baraza la Wawakilishi: Kumbuka Waziri wa Elimu wa Zanzibar ni Muislamu na anawakilisha maslahi ya Wazanzibar ambao walikuwa na jazba sana baada ya matokeo hayo kufutwa.

SMZ yakubali wanafunzi 1,200 wafutiwe matokeo
Imeandikwa na Khatib Suleiman, Zanzibar; Tarehe: 4th April 2012


HabariLeo | SMZ yakubali wanafunzi 1,200 wafutiwe matokeo


SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imekubaliana na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), kwa hatua yake ya kuwafutia matokeo ya mitihani ya kidato cha nne wanafunzi 1,200 kutoka Zanzibar baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwa kushirikiana na wasimamizi wa mitihani.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ramadhan Abdalla Shaaban alisema hayo wakati akijibu hoja za wajumbe waliopitisha Muswada wa Kuanzishwa kwa Bodi ya kufanya tathimini ya vipimo vya elimu Zanzibar.

Shaaban alisema SMZ iliwasiliana na NECTA kuhusu kuwepo kwa taarifa za kuvuja kwa mitihani pamoja na wanafunzi wengi wa Zanzibar kufutiwa mitihani yao ya kidato cha nne waliofanya mwaka jana.

"Tulifanya mawasiliano na kupeleka mjumbe wetu huko, lakini baada ya utafiti ilibainika kwamba wanafunzi wamefanya udanganyifu mkubwa wa mitihani yao baada ya kupata vielelezo mbalimbali," alisema Shaaban.

Alisema hata hivyo SMZ imeunda chombo kuchunguza suala hilo la kufutiwa kwa wanafunzi wa Zanzibar mitihani ya kidato cha nne, lakini taarifa za awali pamoja na uthibitisho wake unaonesha kwamba wanafunzi wamefanya udanganyifu ambao ni kinyume cha maadili ya mitihani.

Alisema hivi sasa wanafunzi wengi wanakabiliwa na dhana potofu ya kusubiri kununua mitihani ya taifa ya kidato cha nne na sita na kuacha kusoma kwa bidii.

Aidha, Shaaban aliwataka wazazi nao kuacha kabisa tabia ya kushawishiwa na watoto wao kununua mitihani ya taifa, kwani kufanya hivyo madhara yake ni makubwa ikiwemo kufutiwa mitihani ya taifa.

Akijibu hoja za wajumbe, Shaaban alisema SMZ haina mpango wa kujiondoa katika Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwani chombo hicho kipo kwa mujibu wa sheria kikiwa ni taasisi ya Muungano.

"Hatuna mpango wa kujiondoa katika chombo cha NECTA......tumeunda Bodi ya kuangalia tathimini ya vipimo vya elimu, lakini haina maana kwamba tunajiondoa katika Baraza la Mitihani la Taifa," alisema.

Wajumbe wengi wa Baraza la Wawakilishi waliochangia muswada huo waliitaka Zanzibar kujiondoa NECTA baada ya kuwepo tuhuma za kufutiwa mitihani yao taifa kidato cha nne wanafunzi wengi kutoka Zanzibar.


Mimi ningekushauri ndugu yangu kama unadhani una malalamiko ya msingi, uende pale na mbunge wako au Mwakilishi wa Taasisi inayokutetea, utaoneshwa vielelezo vyote ujiridhishe kuwa haki imetendeka. Maneno matupu kama haya ni kupandikiza chuki za kidini ambazo hazitakusaidia wewe wala yeyote yule Tanzania hii.
 
"Tulifanya mawasiliano na kupeleka mjumbe wetu huko, lakini baada ya utafiti ilibainika kwamba wanafunzi wamefanya udanganyifu mkubwa wa mitihani yao baada ya kupata vielelezo mbalimbali," alisema Waziri wa Elimu wa SMZ Mh. Ramadhani Abdallah Shaaban.
 
Habari ambazo nimezipata kutoka katika Chanzo nachokiamini ambacho kina uhusiano na Baraza la Mitihani (NECTA) ni kua ulikuwepo mkakati wa kuwafelisha wanafunzi wa Form six waliofanya somo la ISLAMIC KNOWLEDGE ambao matokeo yao yametoka hivi karibuni lakin mkakati huo UMEKWAMA.

Kukwama huko kwa mkakati huo kunakuja huku matokeo yakiwa yashatoka, na kuna habari kua kwa mara ya kwanza katika historia ya Board, wanafunzi hao wa kiislam watapewa upya matokeo yao badala ya yale ya awali ambayo iligunduliwa "yamechakachuliwa"

Uchakachuaji huo umekuja kwenye somo la "Islamic Knowledge" ambalo kawaida hua Lina "paper" 2.

Kuna tetesi kua Katika usahihishaji wa somo hilo, uchakachuzi umefanyika kwa kujumlisha paper zote mbili lakin "wastani" ukapatikana kwa kuchukua jumla ya alama na "kugawa kwa 3" jambo ambalo limepelekea wastani uwe mdogo kuliko uhalisia.

Hii imekuja baada ya kutopatikana angalau A moja tu.

Simply ukipata 80 na 82 wastani utakuja 81 tu.
But kama jumla (162) inagawanywa kwa 3 badala ya 2 ni wazi kua wastani utashuka kua 54 badala ya 81 (27 less).

Inaelekea huna elimu ya elimu. Inaonyesha hujui hata taratibu za usahihishaji mitihani zinavyokwenda. Ni hoja ya kipumbavu sana, hujui taratibu za usahihishaji kimsingi hata mtu aliyehitimu elimu ya chekechea hawezi kutoa hoja kama hii, sijui mnatatizo gani nyie watu maana hapa duniani HAKUNAGA KAMA NYIE!!!:der:
 
Habari ambazo nimezipata kutoka katika Chanzo nachokiamini ambacho kina uhusiano na Baraza la Mitihani (NECTA) ni kua ulikuwepo mkakati wa kuwafelisha wanafunzi wa Form six waliofanya somo la ISLAMIC KNOWLEDGE ambao matokeo yao yametoka hivi karibuni lakin mkakati huo UMEKWAMA.

Kukwama huko kwa mkakati huo kunakuja huku matokeo yakiwa yashatoka, na kuna habari kua kwa mara ya kwanza katika historia ya Board, wanafunzi hao wa kiislam watapewa upya matokeo yao badala ya yale ya awali ambayo iligunduliwa "yamechakachuliwa"

Uchakachuaji huo umekuja kwenye somo la "Islamic Knowledge" ambalo kawaida hua Lina "paper" 2.

Kuna tetesi kua Katika usahihishaji wa somo hilo, uchakachuzi umefanyika kwa kujumlisha paper zote mbili lakin "wastani" ukapatikana kwa kuchukua jumla ya alama na "kugawa kwa 3" jambo ambalo limepelekea wastani uwe mdogo kuliko uhalisia.

Hii imekuja baada ya kutopatikana angalau A moja tu.

Simply ukipata 80 na 82 wastani utakuja 81 tu.
But kama jumla (162) inagawanywa kwa 3 badala ya 2 ni wazi kua wastani utashuka kua 54 badala ya 81 (27 less).

You are a victim of your own imagination; Waislamu na dhana ya kuonewa itawaponza sana katika hii globalized world. kazeni buti mtakwama sana kisha mkimbilie sera za UAMSHO au UTALIBAN!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Taahira ni yule anae amini Mungu alikuja Duniani akaendesha mikutano ya hadhara !

Kuna ujinga unaopita wa kununua picha ya mzungu kwa pesa zako kisha ukasema ni Mungu!

Kuna upumbavu unaopita ule wa kuamini Mungu alipigwa ili akusamehe wewe aliyekuumba ! Sasa wale waliompiga wako peponi !?
Mkuu Ally hapa hujengi, unazidi kubomoa, Acha kabisa hii habari ya kukashifu imani ya mtu maana hata Allah(sw) hapendi. Hata kama umekasirishwa vipi ni bora ukakaa kimya kuliko kuanza kujibu kwa lugha ya kukashifu( Rejea kisa cha Umar(ra) wakati alipotukanwa sana akakaa kimya na mtume (saw) akawa anacheka lakini Umar(ra) alivyoanza tu kujibu, mtume alikasirika sana, kwa sababu tu Umar alishindwa kuzuia hasira zake).

Tukirudi kwenye mada, mimi ninaamini ni busara zaidi tukimuomba mtoa mada atupe ushahidi kuliko kuanza kumshambulia na kuwadhihaki waislamu. Kuna mtu hapo juu amedai kuwa shule zilizoko chini ya taasisi za kiislamu zina matatizo, huenda hili ni kweli lakini haliwezi kuondoa ukweli kuwa kuna hujuma kama kweli hizi hujuma zilifanyika na ushahidi upo. Ifike mahali tuache ushabiki, suala hapa ni kuwepo au kutokuwepo kwa hujuma, haijalishi kama malengo ya hujuma hizo ni nini, maana kwa hakika kama kuna hujuma mwenye kujua kwa hakika malengo ya hujuma hizo ni yule mwenye kutekeleza hujuma hizo.

Mnapokuwa wakali na dhihaka nyingi, mnawafanya hata wale wanaoweza kuona hili kama jambo jepesi basi wajiulize mara mbili kuna nini kinaendelea.

Ni vyema busara zikatumika katika majadiliano yetu.

Ijumaa kareem.
 
Mtoa mada ni mhariri wa gazeti la ALNUUR. Hivi JK umeishia kukemea habari zinazochochea chuki tu? si wewe wala waziri wako anayechukua hatua.

ALNUUR( kama nimepatia) linatoka ijumaa na leo limeandika kuna mchungaji baraza la mitihani kulinda maslahi ya Wakristo!!. Maamuma wameshalibeba wanakuja nalo humu JF

Lingekuwa gazeti lingine mhariri angeshakamatwa, kama ilivyotokea kwa Said Kubenea, na kupata msukosuko mkubwa. Haya mambo si ya kuyalea, au kama ni kweli tujue ama kama ni ujinga uleule tujue. Maana wanasema KIGHOMA MALIMA ndiye aliyekomesha hujuma kwa kuanzisha utaratibu wa kutumia Number badala ya majina. Sasa Wanaibua mapya. Nakumbuka wimbo wa Twanga kwamba "elimu ya mjinga ni majungu"


 
unaparta div. 1 kwa alama za dini? halafu unategemewa uje uwe mtaalam kwenye jamii? Mi nadhani tujipongeze kwa kupata alama nzuri kwenye masomo yenye msaada kwa jamii siyo haya ambayo hata kama utapata A, havina uhusiano wa kufika kwa MUNGU.
 
Kwa hiyo udini umeingia NECTA!!!??? aibu kubwa hiii!!!!
Kama ni kweli kuna kosa la kiufundi lililofanyika ktk kugawanya hayo matokeo kama mwanzisha thread anavyosema,huo ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa baraza ambao hufanyika kwa mwanafunzi yoyote yule na wala usionekane kuwa ni special kwa kuwa umewagusa waislam kama thread yenyewe inavyoonekana kuegemea.. Ingekuwa ni somo la Bible Knowledge kwa upande wa wakristo wala isingekuwa issue maana ni procedure ya kawaida na wahusika wasingepoteza muda kuleta uzi kama huu hapa jukwaani..... tusipende kila kitu kukipeleka kwenye udini....
 
Ni wastani wa wanafunzi wangapi waislam wamefanya uwo mtiani kwa sababu unaposema wanafunz wakiislam mi ninamdogo wangu yeye akufanya hilo somo.vipi kwenye masomo mengne wameakiki upya.
 
Hii ni Aibu, wanafunzi wote walohitimu kidato cha sita mwaka huu andamaneni kulaleki.
Uzembe wa maana huu
 
Kuna form six shule inafundisha masomo mawili tu. Kwa maana nyingine hiyo shule inafundisha somo moja la kawaida na pili Islamic knowledge?
 
Kwa hiyo udini umeingia NECTA!!!??? aibu kubwa hiii!!!!

si udini. rufaa hukatwa kwa somo lolote lile na kama kuna makosa hurekebishwa. kosa lenyewe ni baada ya papers za somo hilo kuwa mbili mwaka huu badala ya tatu za mwaka jana. wakati wa ukokotoaji hiyo factor haikubadilishwa kutoka 3 (sio 4) hadi 2!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom