Mkakati wa kurahishisha maisha ya watoto: Nawezaje kufanya mtoto apate uraia wa Zanzibar?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Sote tunajua Mzanzibari ni mtu mwenye nafasi kubwa sana nchi nzima ya kupata ahueni ya maisha.

Tukianza kazi Wazanzibari walioelimika hata kidogo tu wakija kuomba kazi bara huwa wanapewa kipaumbele kikubwa kwasababu ya kuwa Wazanzibar.

Ukija hata jeshini huku wazanzibar huwa wanapewa upendeleo wa hali ya juu sana, ila kwa kule kwao jeshi lao naskia hata kujiunga tu ukiwa wa bara ni ishu.

Nafasi za uongozi Serikalini nazo ni tele huko kwao, kuna wilaya 11 na mikoa mitano licha ya kwamba eneo lote hilo ni kama wilaya moja tu ya Dar, Ukija huku nako bara mzanzibari anapewa kipaumbele baadhi a nafasi za uongozi wamo.

Yani kiufupi uwezekano wa kuyapata maisha na mkubwa, watu wachache ila nafasi ni nyingi tena nzito tu.

Nakumbuka hata nilipokuwa nasoma chuoni walikuwepo wazanzibari, Leo hii kati ya wale wazanzibar ambao nawajua wengine ni wakurugenzi tayari.

Sasa nimeona ya nini wanangu wahangaike wakai oppurtunity ipo, Hata wakiwa wakubwa wakaja kujiunga jeshini au kuomba kazi au kuingia kwenye siasa itakuwa ni rahisi maana watapewa kipaumbele.

Je, nifanye nini wanangu wawe raia wa Zanzibar.
 
Ukija hata jeshini huku wazanzibar huwa wanapewa upendeleo wa hali ya juu sana
Hata kwenye Vita vya Kagera walionyesha ujasiri wa ajabu sana, sehemu ambayo Mkurya inampa shida Mzanzibari anasoma dua tu na kuipenya Ngome ya adui.

Kumbuka hao ni Watu ambao miaka ya sabini walikuwa wanaogopa Komba.
 
Hata kwenye Vita vya Kagera walionyesha ujasiri wa ajabu sana, sehemu ambayo Mkurya inampa shida Mzanzibari anasoma dua tu na kuipenya Ngome ya adui

Kumbuka hao ni Watu ambao miaka ya sabini walikuwa wanaogopa Komba
Ok sawa, Naomba turudi kwenye maada mkuu
 
Hoja yako inauzito sana mkuu mtu anaweza akapita juu juu na asipate Real Content..nikiwa sehemu moja ivi kuna jamaa alisoma gep akaona hapa mwendo wakutoboa ni uzenji tu najamaa alikua anabihev kama real mzenji nawengi tukijua jamaa ni mzenji kuanzia jina hadi ushikaji wa dini kumbe jamaa niwakisiwani Mafia,Hahaa sema vyeti ndo vilimuumbua
 
ILI MTOTO WAKO APATE URAIA WA ZANZIBAR
1. AWE ANAPENDA KULA MBATATA ZA UROJO KWA ADNAN AU KWA BI TUMAI.
2. AWE ANAPENDA KWENDA FORODHANI SIKU ZA WEEK END.
3. AWE ANAKWENDA FUMBA KWA BAKHRESA BAADHI YA WEEK END.
4. AWE HODARI WA KUPIGA MBIZI KAMA WA KIUME, AMA WA KIKE HODARI WA NAGE.
5.
NAKUJA
 
Sote tunajua Mzanzibari ni mtu mwenye nafasi kubwa sana nchi nzima ya kupata ahueni ya maisha.

Tukianza kazi Wazanzibari walioelimika hata kidogo tu wakija kuomba kazi bara huwa wanapewa kipaumbele kikubwa kwasababu ya kuwa Wazanzibar.

Ukija hata jeshini huku wazanzibar huwa wanapewa upendeleo wa hali ya juu sana, ila kwa kule kwao jeshi lao naskia hata kujiunga tu ukiwa wa bara ni ishu.

Nafasi za uongozi Serikalini nazo ni tele huko kwao, kuna wilaya 11 na mikoa mitano licha ya kwamba eneo lote hilo ni kama wilaya moja tu ya Dar, Ukija huku nako bara mzanzibari anapewa kipaumbele baadhi a nafasi za uongozi wamo.

Yani kiufupi uwezekano wa kuyapata maisha na mkubwa, watu wachache ila nafasi ni nyingi tena nzito tu.

Nakumbuka hata nilipokuwa nasoma chuoni walikuwepo wazanzibari, Leo hii kati ya wale wazanzibar ambao nawajua wengine ni wakurugenzi tayari.

Sasa nimeona ya nini wanangu wahangaike wakai oppurtunity ipo, Hata wakiwa wakubwa wakaja kujiunga jeshini au kuomba kazi au kuingia kwenye siasa itakuwa ni rahisi maana watapewa kipaumbele.

Je, nifanye nini wanangu wawe raia wa Zanzibar.
Kaoe Pemba
 
Back
Top Bottom