Mkakati wa Kumuondoa Kheri James Mkt UVCCM Taifa waiva; Makonda ndio Mratibu Mkuu

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,395
Kuna Mkakati maalum wa kumuondoa madarakani Mkt mpya wa Vijana wa CCM Mdg. Kheri James aliyechaguliwa November, mwaka Jana. Maandalizi yote yashafanyika na mkakati na ni rasmi katika kikao cha Baraka Kuu la vijana linalofanyika mwezi ujao Kheri James anang'oka.

Mratibu wa mkakati huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Paulo Makonda akishirikiana na baadhi ya viongozi wa sasa wa UVCCM, kama ifuatavyo.....

Kikao cha kwanza kilifanyika nyumbani kwa Mkonda na kuhudhuriwa na wajumbe wote, na kikao cha pili kilifanyika Masaki inasadikika ni nyumbani (kwao) moja wa mjumbe aliyeko kwenye makakati huo..


1. Shaka H. Shaka (Kaimu Katibu Mkuu UVCCM)
2. Tabia Mwita (Makamu Mkt wa sasa)
3. Rose Manumba (Mjumbe Baraza)
4. Chidabwa (Mkt UVCCM Dodoma)
5. Mashango (Mkt UVCCM Mbeya)
6. Keisha (MNEC, Bara)
7. Joan (Mjumbe baraza, Taifa)
8. Na Mkt wa vijana Mkoa wa Dar es Salaam..

Hoja zitakazosimamiwa ni kama ifuatavyo
1. Mkt kuidhinisha matumizi ya fedha bila idhini ya kikao chochote

2. Fedha za Mkt kukaa hoteli ghali akiwa Dar es Salaam (Collesium Hotel, Karikaoo) laki 160,000 kwa siku zinatoka kwenye jumuiya bila kuidhinishwa na kikao chochote

3. Mkt kufanya maamuzi bila kufata misingi ya kanuni na taratibu. Kwa mfano, Shaka anasema Mkt alipoteuwa kamati ndogo ya kuhakiki mali za Jumuiya hakufata kanuni. Kwani alitakiwa apeleke majina kwenye kamati ya utekelezaji ndio wathibitishe

4. Mkt kufanya mambo bila kumshirikisha Makamu Mwenyekiti.

5. Fedha nyingi zimetumika kwa hii miezi 3 bila hesabu zake kuwa clear

Na tuhuma nyingine kadhaa walizojiandaa nazo. Taarifa zinasema maandalizi yako tayari, na Makonda kafanikiwa kupandikiza baadhi ya watu kwa Kheri James. Watu hao ni vijana kinda kinda wa Makonda, kwa sasa ndio rafiki mkubwa wa Kheri... Wamewekwa kwa kazi maalum...

NB:naombeni msaada wa kuambatanisha video.

Nimeattach na piture. Huku nikisubiri kuelekezwa namna ya kuattach video.
IMG-20180219-WA0047.jpg
 
Hizo ni hadithi tu. Mtoto wa Mtu atolewe na nani ( tizama picha yake kisha chukua ya Bwana Mkubwa linganisha). Uliza kilichompata Sadifa kwa kumuunga mkono mtu mwingine kwenye uchaguzi Mkuu, katoka juzi tu hapa baada ya kufunguliwa kesi ya rushwa kwa kugawa soda kwa wajumbe.
 
hivi masisiemu yakitafunana na kubamizana yenyewe kwa yenyewe mimi inanihusu nini kwamfano?
 
Bashite ana nafasi gan kwenye chama? Je vikao vyao vipo kikatiba au majungu tu kama wake wenza? Je ni siri au? Umepigaje hako kapicha bila kuomba kibali? Ila kama mwnykit amekiuka taratibu mbona hukumu inasukwa kwa siri? Au hayanihusu nitulie? Ila bando c langu? Nina stress sana...... Aqwilin wangu
 
Back
Top Bottom