Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Ziko taarifa kwamba, wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya ‘unga’ nchini wamekuwa wakimiminika mkoani Lindi kwa lengo la kumnasua gerezani, mtuhumiwa wa biashara hiyo, Ali Khatibu Haji ‘Shkuba’ (45).
Kwa mujibu wa chanzo makini, wauza unga hao wamekuwa wakiweka vikao vya siri vya mara kwa mara jijini Dar es Salaam na Lindi lengo likiwa kuhakikisha mtuhimiwa huyo anatoka gerezani lakini bila kujulikana mbinu wanazotimia ili kufanikisha azma yao hiyo.
“Naamini mnajua kuwa, Shkuba bado yupo mahabusu ya Gereza la Mkoa wa Lindi kwa yale madai ya kuuza unga. Sasa nataka kuwaambia kwamba, wauza unga wenzake wamekuwa wakienda Lindi ili kumnasua jamaa.
“Kuna wakati wanafanya vikao hapa Dar, hasa maeneo ya Kinondoni mara nyingine kulekule Lindi. Lakini sijafahamu wanataka kumtoa kwa staili gani!
“Halafu pia, inawawia vigumu kufanikisha lengo kwa sababu wao wenyewe wengi wao ni vimeo, wanasakwa na jeshi la polisi,” kilisema chanzo hicho.
Shkuba alinaswa saa sita usiku wa Februari 23, 2014 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar akijiandaa kwenda nchini Afrika Kusini na kuhusishwa na unga aina ya heroin kiasi cha kilo 211 yenye thamani ya shilingi bilioni 9.4 yaliyokamatwa Januari, mwaka jana mkoani Lindi.
Baada ya kukamatwa, alisafirishwa usiku huohuo kwenda Lindi chini ya ulinzi mkali wa polisi ambapo Februari 27, mwaka huo aliunganishwa na watuhumiwa wengine na kufikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kusini.
Watuhumiwa hao wengine ni pamoja na binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, Maureen Liyumba.
Source: Mnyetishaji