Mkakati wa Kuihujumu CHADEMA kabla ya 2015 na Kuwabambikia Kesi Viongozi Wake Ulishaanza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati wa Kuihujumu CHADEMA kabla ya 2015 na Kuwabambikia Kesi Viongozi Wake Ulishaanza.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Sep 16, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana-JF niliwahi andika huko nyuma kwamba CCM (chaka la mafisadi) limeunda mkakati wa kuhakikisha CHADEMA hawachukui dola kwa gharama zo zote. Thread ile ilibezwa na baadhi ya wana JF; na huo ndio uhuru wa kimtazamo kwa kadiri ya mtu awezavyo kupembua mambo na kuzitafakari hisia zake.

  Nilijulisha kwamba kuna mkakati wa aina mbili: moja ni kukifanya CHADEMA kionekane ni chama cha shari kilichojikita katika vurugu na mauaji. Mkakati huu umetengenezwa na vyombo vya usalama, watekelezaji wakiwa polisi. Mathalan, hebu soma nukuu hii kutoka gazeti la " Mtanzania" la Septemba 10, 2012,

  CHADEMA WAONESHA PICHA ZA VIDEO JINSI ALIVYOUWA MWANGOSI
  ".....Pia picha hizo, zilionyesha askari polisi mmoja akiwa amevaa kiraia, huku shingoni akiwa na skafu ya CHADEMA lakini baada ya vurugu kuanza, askari huyo alionekana akiivua skafu hiyo na kuiweka mfukoni.

  Alipoivua na kuiweka katika mfuko wa nyuma wa kaptula aliyokuwa amevaa, mwenzake mmoja akampa kofia ya kujikinga na moshi kisha askari huyo akachomoa bastola kwa ajili ya mapambano."

  Nukuu hii inabainisha kuwa askari huyo alijifanya shabiki au mpenzi wa CHADEMA wakati haikuwa hivyo. Askari wenzake walijua yeye alipewa jukumu gani pale. Bastola aliyokuwanayo ilikuwa ya nini yeye akiwa raia na shabiki wa CHADEMA. Kama angeitumia silaha hiyo akiwa amevaa skafu ya CHADEMA, hapana shaka CHADEMA wangehusishwa na mauaji au madhara ambayo angeyafanya askari huyo kwa kutumia silaha yake na askari hawa wako wengi.

  Mkakati wa ni wakubuni kesi na kujenga mazingira ambayo viongozi wa CHADEMA watatumbukizwa ili kuwakatisha tamaa ama kuwafanya wasiaminike tena mbele ya jamii. Kwa kesi hizo, baadhi watafungwa muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015.

  Ikumbukwe kwamba mbinu namba moja ilitumika kukidhoofisha CUF huku kikipachikwa sera za udini pia. CUF walikuja na kauli mbiu yao ya "ngangali" na polisi chini ya IGP Mahita wakaja na mkabala wa ngangali wao wakawa "ngunguli" (katika kabila fulani, ngunguli maana yake shanga za kuvaliwa kiunoni). Kwa hiyo, hapa ni suala la kuangalia na kutafiti uelekeo wa hali ya upepo wa kisiasa unaovuma ndani ya jeshi la polisi. (polisi limekuwa taasisi ya kisiasa kwa sasa tangu mfumo wa vyama vingi uanze nchini. Kwa jumla,(chaka la mafisadi)CCM hataachia dola kirahisi kama wengine wanavyofikiri. "When tough gets going it gets rough" W. Sharkspeare.
   
 2. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Mkuu ahsante kwa kutukumbusha kwani chadema sasa inapigwa vita ndani na nje ya chama ila tunaiman katika Epolpes power na Mnyezi Mungu....... Tutashinda tu...
   
 3. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  cdm wawe makini ktk kila hatua wanayopiga na kila kazi wanayofanya
   
 4. t

  tenende JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mtu anayeshiriki mapambano hawezi kukubishia. Nina ushahidi unaoelekeana na huu. nakusanya picha za mikoa angalau mi5 ndipo nami niwashirikishe!.
   
 5. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Tumebaini.ENZI YA CUF mwamko ulikuwa hakuna.WASUBIRI SANA TUISUSE CDM..WATAKAA SANA
   
 6. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Kumbe "ngunguri" ni chachandu??
   
 7. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Umesababisha jamaa ndani ya Tax watake kunipiga kwa kicheko nilichokitoa!! Kuanzia sasa sisemi Shanga bali nitasema NGUNGURI!
   
 8. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Nakwambia kuna elimu nyingi hapa, acha tu.
   
 9. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Chadema kitakufa kifo cha kwaida kabisa wala hakuna mkakati wowote wakuwabambikia kesi Chadema siyo chama cha siasa ni kikundi cha watu fulani kama NGO.
   
 10. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  You are right mleta hoja. Siku zote tumeonya kuwa polisi wote ni wana CCM hatukueleweka. Majaji, hasa wale wa kuteuliwa kishikaji na kutumiwa kama Tendwa, ni CCM damu. Wakuu wa polisi Saidi Mwema na mtangulizi wake Mahita wanajulikana walivyo ngunguri damu. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na watendaji wake nao ni CCM. Bila kubadili huu mfumo jambazi CDM haiwezi kuchukua nchi. Badala ya kujikita kwenye kampeni, CDM inapaswa kupeleka kesi kwenye vyombo husika hasa balozi za nje na wale wote wanaogharimia uchaguzi kuhakikisha anomalies hizi zinarekebishwa kabla ya kuingia kwenye kipute.Hata hivyo, CCM lazima iondoke kwa namna yoyote iwayo. Watanzania wamechoka. Ikibidi tukope toka Libya.
   
 11. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,456
  Trophy Points: 280
  Kila taarifa yenye kuashiria na/au kuelekea kwenye kupata ukweli basi hiyo ni taarifa muhimu, na sio ya kupuuzwa hata kidogo.

  CHADEMA tafadhalini msipuuze haya. Chukueni tahadhari stahiki kwani haya na mengine mengi tunayojua yamepangwa kwa lengo moja tu la kuidhohofisha CHADEMA ili CCM waendelee kuifisadi nchi hii. Tumekataa na hatutarudi nyuma mpaka nchi hii ikombolewe na kuwa nchi ambapo kila raia wake atakuwa na fursa na haki sawa mbele ya sheria na katika keki ya Taifa.
   
 12. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hizo ni njama wala mkuu hujaongopa huo ni ukweli lakini ccm wajue haya KANU walitumia ujinga kama huu lakini leo hii wako wapi? tusimameni imara kutetea haki ya nchi yetu iwe kwa damu hata kwa kufungwa ila mwisho tutashinda
   
 13. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  na wewe unajiita great thinkers ni kati ya walala hoi mnaotumika kujiona mko hai kumbe wafu
   
 14. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,456
  Trophy Points: 280
  Bosi wako Nape leo kakubali kuwa CHADEMA ndio watakaounda serikali ijayo. Both his words and body language subscribed to a hopeless pilot resignation.
   
 15. lakiwosha

  lakiwosha Senior Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 9, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  hata watumie njama gani tumewachoka hawana jinsi tena THE END IS NEAR
   
 16. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nape anakulipa shs ngapi?
   
 17. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Mfamaji siku zote haishi kutapatapa, CHADEMA ni kama marehemu ambaye taarifa yake ya kifo haijatangazwa, kwanza chama kizima kina sauti tatu tu, ukizitoa hizo chama hakisikiki. Hatupo tayari kuwapa nchi wahuni hata iweje, viongozi gani hawana nidhamu, hawana haya wala aibu kwa umma wa watanzania, wamiliki night clubs, casino na bar, watembea na wake za watu? chama kinaongozwa kwa ukanda, kimejaza wachaga katika nafasi zote nyeti ndani ya chama. CCM jenga nchi CCM tawala, wewe CCM ndio chama imara unastahili kuendelea kutawala dola, changamoto zilizopo tunaimani kwamba zitapatiwa ufumbuzi chini ya uongozi imara.
   
 18. C

  Chesty JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,350
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Nchi ipo hoi bin taaban bado unataka CCM watawale, wewe ndio unatuhamasisha tuwang'oe, utakuwa mwizi namba one.
   
 19. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,177
  Likes Received: 1,259
  Trophy Points: 280
  Mbona kuhusu tuhuma za ufuska mlishaonywa na mkanywea!?
  Usitake tukuambie ni akina nani wanasomesha mahawara kwa fedha za walipa kodi. usitake kuambiwa ni kiongozi gani anayebadilisha damu kila wakati na anaendelea kuambukiza watz VVU bila kujali. nyamaza tafadhali. taarifa ni nyingi mno za wakuu wa chama chako tukizitoa hapa hata wafadhili watatutesa.
   
 20. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  ukitaka kuing'oa ccm hakikisheni mnakipa chama ambacho kweli kina hadhi zaidi ya chama cha mapinduzi, sio hicho kikundi cha wavaa magwanda ambao wamejidedicate kutwaa dola kwa namna yeyote ile hata kwa umwagaji damu, ni hatari kwa taifa kuwafumbia na kuwaunga mkono watu hawa.
   
Loading...