Mkakati wa kina Ponda waanza kukwama Dar

Nadhani, wanaoweka mabango nje ya nyumba zao kuwa hutaki kuhesabiwa ndio wanarahisisha kazi ya kujua idadi kamili ya akina Ponda...:hat:.
 
551633_279319032169526_1913081750_n.jpg
 
Duh, hii safi sana.
Serikali yetu tukufu na sikivu ni halali na ipo kisheria.
Mtu anayepingana nayo huyo ana nia ya ku-disrupt maisha ya mtz ambaye hana hili wala lile ambao wengi wao ni maskini wa kutupa. Next mi nashauri wote waliotutumia SMS za kipuzi watafutwe na kupelekwa mbele ya pilato, ifike mahali serikali ioneshe mabavu yake, maana lele zimezidi.

Naunga mkono mia kwa mia mkuu.Asiyehesabiwa ni mhalifu na anatakiwa kufungwa.Chezeya serikali weye?
 
Mimi ni karani wa sensa huku tandika kaya nyingi za waislamu nmezhesabu na zilizogoma ni kaya 5 nmesharipoti na hizo kaya zmekuwa noted kwa hatua kali zaidi

Ilitakiwa mpewe Radio call mkuu,Ukikutana nambishi unaitumia!!
 
Ule mkakati unaoratibiwa na Sheikh Ponda Issa Ponda wa kushawishi waislam wasishiriki zoezi la sensa lililoanza leo linaelekea kutopata mafanikio baada ya waislam walioweka mabango majumbani kwao ya kutokuhesabiwa kukubali wenyewe kuhesabiwa bila kikwazo.

Shuhuda wa habari hizi ambaye ni mimi mwenyewe nimeshuhudia makumi ya waislam wakihesabiwa kuanzia ubungo jirani na mitambo ya umeme ya Aggreco hadi mabibo ambapo waliohesabiwa walisema wanahesabiwa kwakuwa hawataki 'maneno' na serikali.

Walidai kuwa wanaunga mkono hoja za wenzao za kutokuhesabiwa lakini wakasema serikali ikiamua jambo haishindwi hivyo wanaepuka kitakachofuata baada ya huo mgomo.

Maeneo ya Mburahati, kigogo nq Luhanga mwitikio wa kuhesabiwa umekuwa mzuri, ingawa wapo wachache waliogoma lakini zimesikika lawama kutoka kwa baadhi ya Maustaadh wakilalamika KUSALITIWA na wenzao ambapo wamelia na WOGA wa waislam kwenye mambo aliyoyaita ya msingi.

Karani wa Sensa aliyekuwepo Mabibo -Sahara na Mabibo Muleba hadi jirani na Mabibo External wamesema hadi muda huu zoezi liko vizuri na wachache waliogoma watashughulikiwa.

Wamesema jukumu lao ni kuandikisha na kaya itakayogoma itapelekwa kwa mwenyekiti wa serikal za mtaa ambaye naye atawahesabu, wakimgomea huyovndipovwatakapochukuliwa na polisi kwenda kuhesabiwa kinguvu rumande wakati huo wakisubiri vifungo.

Afisa mtendaji wa kata ya Mabibo amesema kama waislam wataendelea na mchezo huu wa kijinga watakuwepo wengi watakaopoteza ajira maana serikali imejipanga kuwafunga wote watakaogoma kuhesabiwa

551633_279319032169526_1913081750_n.jpg
Qwatakao hesabiwa ni MISUKULE yaani wafu wanaotembea.. Ujinga mwingine lazima kuupima kwani swala hili sio la Waislaam bali usahihi wa zoezi la SENSA. Takwimu zinazohitajika ktk sensa ni lazima ziwe na tofauti zote za wananchi ambazo zinaweza kuwasaidia kujipatia maendeleo na serikali kupitisha policies ambazo zinatazama mahitaji ya wananchi wote ktk jumuiya zao.
 
unatudanganya kutuambia kuwa kuwa watafungwa watu kwa kutohesabiwa.
Hakuna kitu kama hicho.
Kama ni hivyo wangeanza kumkamata ponda na wenzake na serekali ingekuwa haiwaombi waliogoma kushiriki badala yake ingewaambia ni lazima na ambaye atagoma atashtakiwa.
Haujasikia hotubo ya raisi jana?
Alikuwa anaomba na sio kuagiza.
Mi nawapongeza wote walio hesabiwa na wale ambao hawakukubali nao nawapongeza kwani kila mtu ana uhuru wa kufanya anacho amini kuwa ni sahihi zaidi.

KWENYE MOVIE HUWA WANASEMA "WATCH ME"

Kwahiyo Subiri uone,nadhani umewasahau masheikh wa tanga,kilimanjaro na kigoma
 
Kuwafunga nadhani ni mkwara tu. Ila kwa muislam yeyote mwenye ajira inayoeleweka na mstakabali wa maisha yake na familia yake unategemea ajira hiyo, hawezi kufanya upumbavu wa kugoma sensa halafu ahatarishe kibarua chake kwa kufunguliwa jalada polisi na usumbufu mwingine.
Watakaogoma ni wale 'kenge' ambao hata wakifunguliwa mashtaka au kuwekwa ndani hawatakuwa na kitu cha kupoteza. Watu kama shehe ponda and co ambao wana uhakika kupata chochote kutoka kwa wafadhili wao hata wakiingia kwenye misukosuko na dola.

Ni vizuri ukatumia akili na uhuru wako vizuri, kumwita Shekh Ponda kenge unajidhihaki wewe mwenyewe. ACHA.
Haikuwa lazima kugoma kuhesabiwa hata hivyo shekh Ponda and Co walikuwa na hoja zenye mantiki na ambazo ni endelevu kwa hiyo bado mapambano yataendelea.

Ikumbukwe waislam hawajawahi kusema hawajui maana na faida za sensa ila kero za mabedui ndani na nje ya serikali ndizo zilizosababisaha mgomo uitishwe.
 
Mimi ni karani wa sensa huku tandika kaya nyingi za waislamu nmezhesabu na zilizogoma ni kaya 5 nmesharipoti na hizo kaya zmekuwa noted kwa hatua kali zaidi

ACHA KUTISHIA WATU KWA KIVULI KARANI WA SENSA, ANGALIA STATISTICS ACT ya mwaka 2000, ukurasa wa 351.
 
Mtukane mtakavyopenda mwisho mtachoka na mwisho wa siku, zoezi hili litakuwa failure nyingine na upotezaji wa fedha za walipa kodi. Huwezi kuwalazimisha watu waliokuwa Huru kufuata myatakayo kila siku..Nasema zoezi hili litashindwa na hakuna mtakacho fanikisha maana nchi hii sii yenu pekee..
 
Mimi nakupa hali halisi nikutishe ili iweje, taarifa zimeshafika kwa mkuu wa polisi wilaya
ACHA KUTISHIA WATU KWA KIVULI KARANI WA SENSA, ANGALIA STATISTICS ACT ya mwaka 2000, ukurasa wa 351.
 
Mtukane mtakavyopenda mwisho mtachoka na mwisho wa siku, zoezi hili litakuwa failure nyingine na upotezaji wa fedha za walipa kodi. Huwezi kuwalazimisha watu waliokuwa Huru kufuata myatakayo kila siku..Nasema zoezi hili litashindwa na hakuna mtakacho fanikisha maana nchi hii sii yenu pekee..

Na sisi wahaya hatuhesabiwi mpaka mtuletee senene ,wengine wanataka pundamilia ,wengine wanataka kipengele cha dini .serikari itashika wapi? mimi binafsi siwezi kukubali kenge kama shehe ponda awe policies maker wa nchi yangu .hata nchi kama misri wameanza kuondoa dini kwenye vitambulisho vyao vya uraia.Rwanda nako wameondoa kabila sisi bado tunataka kwenda kulekule .narudia tena shehe ponda ni kenge.
 
Kama umetumwa na serikali bac umedoda,waislam wengi msimamo ni uleule,uliza huko tanga,mtwara,lindi hata hapa dar yenyewe usìkie madudu,sensa imeshashikana bora makarani wapumzike tu kuliko kusumbuliwa
 
Back
Top Bottom