Mkakati wa JK kumrithisha urais January Makamba utafanikiwa au itakuwa kama Moi na Uhuru Kenyatta? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati wa JK kumrithisha urais January Makamba utafanikiwa au itakuwa kama Moi na Uhuru Kenyatta?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanga, Jun 7, 2012.

 1. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ndg wanaJF kuna mkakati wa chinichini wa JK kumuandaa January Makamba Mbunge wa Bumbuli kuwa mrithi wa Urais kupitia chama chake cha CCM kwenye uchaguzi wa 2015.

  Moja ya mikakati hiyo ni pamoja na kumuondoa Mzee Makamba baba wa January kwenye nafasi ya utendaji wa chama ili January achaguliwe kwenye Kamati kuu na Sekretariati ya chama ili kuondoa mgongano wa maslahi na malalamiko kwa wanachama endapo Makamba Sr na Jr wangeendelea kufanya kazi za chama kwa pamoja.

  Pia kauli ya JK kuwa wazee kama yeye au wenye umri kama wake zaidi ya miaka 60 wasahau kuwa maraisi wajao wa JMT kupitia CCM, akiwalenga zaidi akina Sitta, Lowassa na wengineo wenye nia ya kugombea urais.

  Kauli ya January akiwa na Zitto kutamka wazi kuwa umri wa kugombea urais upunguzwe kutoka miaka 41 hadi 35 ilikuwa ni njia ya awali kupima upepo wa wananchi kama watakubaliana na maoni hayo maana kikwazo kinachoonekana kwake ni umri maana mwaka 2015 Makamba Jr atakuwa hajafikisha miaka 41.

  Kikwete kumteua na kumpangia idara ya siasa na mambo ya nje kwenye sekretariati ya CCM ilikuwa nikumpa exposure kwa nchi marafiki na kujenga ushawishi kwa mataifa ya nje kwa njia zote za kimsaada na maelewano ya kimataifa.

  Makamba Jr kuendelea na wadhifa wa Naibu waziri na ujumbe wa Sekretariati ya chama kama mkuu wa idara ya mambo ya nje na siasa, wakati Mwenyekti wa chama Raisi JK aliwahi kusema nafasi hizo ni za kudumu na kiongozi anatakiwa kufanya kazi muda wote hivyo kama alivyofanya kwa akina Chiligati alikuwa waziri alipopewa unaibu katibu mkuu wa chama akaachia nafasi ya uwaziri. Nape alikuwa mkuu wa wilaya naye alipopewa nafsi ya uenezi akatemwa kwenye UDC, Mwigulu yeye ni mbunge tu hana nafasi nyingine katika Serikali hivyo kundelea na nafasi ya mkuu wa idara ya fedha ya CCM.

  Kumteua Makamba Jr hivi karibuni kuwa naibu waziri katika baraza lake pia ni mbinu ya kumpa exposure na kumuandaa kuzoea ofisi za juu na serikali na utendaji wake.

  Kuendelea kushikilia cheo cha chama tofauti na maagizo ya Mwenyekiti na Raisi JK mwenyewe badala ya kuachai cheo cha chama. Vikao vya chama mwezi uliopita wanachama wengi walitegemea kuwa nafasi ya Makamba Jr kwenye chama ingejazwa na mwanachama mwingine lakini mpaka sasa nafsi Makamba Jr ameshikilia na kuwa mwanachama pekee (exceptional) hii ni kwa sababu ya double standard za Mwenyekiti JK.

  Kama JK amezamilia kweli kumhandaa Makamba Jnr kuwa mrithi wake wa urais inabidi ajue kucheza kete zake kwa ustadi makini la sivyo atajikuta anakuwa kama Raisi mstaafu wa Kenya, Mzee Moi alivyozamilia kumuandaa Uhuru Kenyatta mtoto wa Rais wa zamani wa Kenya kuwa Rais bila ya kuwa na nguvu ya chama chake na makundi na wakati wa uchaguzi chaguo lake likasambaratishwa na muungano wa vyama vya upinzani wakati wa PNU kati ya Mwai Kibaki na Raila Odinga mwaka 2,000, na mWAI Kibaki akachaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Raisi wa Kenya na KANU chama tawala kikao ndio mwisho wa historia yake hadi sasa.

  Pengine tutegemee kama hayo kutokea Tanzania baada ya uchaguzi 2015 chama tawala kikiwa na makundi hasimu ya kuwania urais na CHADEMA ikizidi kujiimarisha siku kila siku.
   
 2. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,398
  Likes Received: 6,585
  Trophy Points: 280
  imekula kwao this time..makamba hatakuwa rais..mambo kama haya ya kipuuzi tunazidi kuyalea sasa..to hell with the system kura kwa EL kama sio EL Chadema..hata mbuzi akigombea chadema kura yangu napeleka chadema
   
 3. t

  tara Senior Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sio Asha Migiro tena...?
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,907
  Trophy Points: 280
  waache wazikane
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani ana mpango wa wa kuhamia CDM?
   
 6. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ndo hapo chacha...
   
 7. Msaranga

  Msaranga JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  yetu macho lakini mwaka 2015 ndio mwisho wao
   
 8. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Siasa za ndani ya ccm ni kama mchezo wa kuigiza.No matter what,Nguvu ya umma ndo mpango mzima!
   
 9. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  makamba akiwa Rais mi najivua utanzania
   
 10. J

  JULIUS MBIAJI Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa uchambuz wako.Hivi hakuna kabisa mtu mgumu,mkomavu na aliyewah kuonja chungu ya maisha?J Makamba mbona laini sana.Ila kwa kwel kuna ukwel ndanimwe maon yako.Ila mpango huo hautafanikiwa.
   
 11. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,842
  Trophy Points: 280
  kweli bana JANUARY MAKAMBA is too soft to be a president... ni kama BENARD MEMBE

  bora hata lowasa kuliko hawa ma NICE BOYZ
   
 12. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Absolutely PIPE DREAM.
   
 13. n

  ng'wabuki Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yale yale ya uamsho
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi bado January Makamba yuko CC? Nilidhani CCM walishaamua kuwaondoa mawaziri CC na ndio sababu Membe akaondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na January, sasa wamebasili tena kanuni au? Pia ningependa kujua nani mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Nishati maana January sasa ni Naibu Waziri?
   
 15. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  halafu mke wake sio mtanzania
   
 16. b

  bumes Senior Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  CCM sio mali yamtu ili walisishane, hayo nimaoni tu.
   
 17. S

  Selemani JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2013
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Bado relevant?
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,578
  Trophy Points: 280
  Kuna watu niliwaeleza humu EL ni Yohana Mbatizaji tuu, akiyanyoosha mapito ya yule yuajaye!.
  Pasco.
   
 19. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #19
  Dec 7, 2013
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ukitaka mpasuko utokee ndani ya chama basi makosa hayo yafanyike
   
 20. h

  hakisoni JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2013
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 429
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hivi hicho nacho ni kipingamizi cha uraisi? Ni wa wapi huyo??
   
Loading...