Mkakati wa CHADEMA Kugomea Viti Maalumu ni 'Political Maneuver' isiyokuwa na tija yoyote

Ni andiko la ovyo kabisa.

Bila shaka uwezo wako wa kuona mambo hauzidi umbali wa mita 2. Kama wote wangekuwa na fikra za kiopuuzi kama hizo zako, bila shaka Afrika isingepata uhuru. Ubaguzi wa rangi usingeisha Afrika Kusini.

Hivi unajua Mandela alipewa offer ngapi za kushiriki katika serikali ya weupe lakini alikataa? Unajua Jaramogi Odinga alipewa options ngapi za kushiriki kwenye madaraka ya weupe Kenya lakini alikataa?

Mandela alikaa jela zaidi ya miaka 20. Akina Sisulu, Mzee Mbeki (mwanaye alikuja kuwa Rais) walipigania haki za weusi kwa zaidi ya miaka 40, na wengine hawakuweza hata kuiona Afrika Kusini ya usawa kwa wote.

Wewe kwa vile huna maono, ukiona mtu hakupata anachokipigania ndani ya miaka 5, basi kwa fikra zako duni unadhani amepoteza.

Haijalishi itachukua miaka 10, au hata 20, Tanzania ni lazima ibadilike, itoke kwenye utawala wa kishetani wa leo na kuingia kwenye utawala wa kistaarabu. Tunaweza kuiona au tusiione Tanzania ya namna hiyo lakini ndoto zetu kwa kuwa ni sahihi, zitadumu na zitashinda. Uovu hauwezi kudumu milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani umebugi BIG TIME.
Maamuzi ya vyama vya upinzani, hasa CHADEMA , huko nyuma ni wazi yamewasaidia. CHADEMA wamekuwa wakiongeza viti vya ubunge na idadi ya kura za urais, consistently kwa chaguzi zote, at the expense of ccm. Graph ilivurugwa na umafia wa Magufuli , na sio ushindi halali.

Ushindi wa 99% serikali za mitaa 2019 wala sio ushindi. Kutumia polisi, kuengua wagombea, maafisa wa uchaguzi kukimbia ofisi, ndio "mikakati" ya ushindi ya ccm. Huu wa 2020 nao mambo ni yaleyale. Kama unahesabu huo ni ushindi, basi una matatizo.

Kugoma kwa CHADEMA kuteua wabunge viti maalum ilikuwa mkakati mzuri sana. Umetoa fursa kwa ccm kujikaanga kwa operesheni mbovu kabisa, in desperation. Swali la msingi ni kwa nini ccm is so desperate CHADEMA waweke hao wabunge, hadi kufikia ccm wenyewe "kuwasaidia" CHADEMA kuwaweka?

Ongezeko la wabunge halikuletwa na kususa na kufanya migomo. Wabunge walikuwa wakiongezeka kwa sababu ya agenda mliyoisimamia hadi kufikia katikati ya mwaka 2015. Tangu mlipobadili gia angani, chama kimeingia rasmi kwenye rollercoaster kujifuta kutoka kwenye electoral map.

Madai ya kudhulumiwa ushindi yanatoka kwenye playbook ya narcissists ambayo hata Trump anaitumia. Huo ni utamaduni wa narcissists wote popote walipo!
 
Ni kitambo sana wananchi hawajapewa fursa ya kuchagua viongozi wao.Ni tangu uchaguzi wa serikali za mitaa.
Viongozi wanachaguliwa na Mahera.

Maamuzi ya CHADEMA sio mepesi ni magumu sana
 
Usiwe kama Boss wa NEC anaesahau kuwa tarehe 20 alisema kuwa hajapokea orodha ys majina kutoka Chadema.

Amandla...

Kwa hiyo kusema ninaipinga Chadema kwa mambo yake mengi ni sawa na kusema I am always against Chadema? Hii ni tafsiri ya aina gani, mkuu?
 
Ni andiko la ovyo kabisa.

Bila shaka uwezo wako wa kuona mambo hauzidi umbali wa mita 2. Kama wote wangekuwa na fikra za kiopuuzi kama hizo zako, bila shaka Afrika isingepata uhuru. Ubaguzi wa rangi usingeisha Afrika Kusini.

Hivi unajua Mandela alipewa offer ngapi za kushiriki katika serikali ya weupe lakini alikataa? Unajua Jaramogi Odinga alipewa options ngapi za kushiriki kwenye madaraka ya weupe Kenya lakini alikataa?

Mandela alikaa jela zaidi ya miaka 20. Akina Sisulu, Mzee Mbeki (mwanaye alikuja kuwa Rais) walipigania haki za weusi kwa zaidi ya miaka 40, na wengine hawakuweza hata kuiona Afrika Kusini ya usawa kwa wote.

Wewe kwa vile huna maono, ukiona mtu hakupata anachokipigania ndani ya miaka 5, basi kwa fikra zako duni unadhani amepoteza.

Haijalishi itachukua miaka 10, au hata 20, Tanzania ni lazima ibadilike, itoke kwenye utawala wa kishetani wa leo na kuingia kwenye utawala wa kistaarabu. Tunaweza kuiona au tusiione Tanzania ya namna hiyo lakini ndoto zetu kwa kuwa ni sahihi, zitadumu na zitashinda. Uovu hauwezi kudumu milele.

Sent using Jamii Forums mobile app

Andiko langu halikulenga kukufurahisha wewe. Jukwaa lipo; jipe furaha mwenyewe kwa kuleta andiko lako!

Kuwalinganisha SA freedom fighters na postindependence political thugs wa EAC ni kuwakosea heshima kulikopitiliza!
 
Kwa nini sisi CCM tunahangaika na masuala ya CHADEMA, kama wamegomea viti maalumu si juu yao. Hawa ndio walitucheleweshea maendeleo kwa kupinga pinga kila kitu, acha wakae nje tujenge nchi. They are useless and full of drama.
Ndugai anakosa $900m kwa mwaka bro
 
Ni kitambo sana wananchi hawajapewa fursa ya kuchagua viongozi wao.Ni tangu uchaguzi wa serikali za mitaa.
Viongozi wanachaguliwa na Mahera.

Maamuzi ya CDM sio mepesi ni magumu sana

Hiyo ni perception yako ambayo pengine imesababishwa na wewe kutokumpata kiongozi uliyemtaka. Hata hivyo, hiyo ndiyo democracy yenyewe; you don’t always get to install the leader you wanted!

Mgogoro wa viti maalumu haukupaswa hata kuwepo kama viongozi wa CDM wangetumia busara mapema kabisa.
 
Kwa hiyo kusema ninaipinga Chadema kwa mambo yake mengi ni sawa na kusema I am always against Chadema? Hii ni tafsiri ya aina gani, mkuu?
Ni tafsiri sahihi. Unataka ku split hairs, Mkuu. Au ulitaka niseme " you are often against Chadema"?

Amandla..
 
Ni tafsiri sahihi. Unataka ku split hairs, Mkuu. Au ulitaka niseme " you are often against Chadema"?

Amandla..

“Always” and “often” evoke time frequency, but “mambo mengi” evokes the quantitative degree of our disagreement! So they aren’t members of the same family!
 
“Always” and “often” evoke time frequency, but “mambo mengi” evokes the quantitative degree of our disagreement! So they aren’t members of the same family!
There you go again, comparing apples to oranges.
Intellectual pompousity won't get you anywhere with me.

Amandla...
 
Ulichokiandika ni uchambuzi wa hovyo na usio na maana yoyote.

CCM wanasema wapinzani wanachelewesha maendeleo, walitaka washinde viti vyote majimboni ili kuharakisha maendeleo, sasa viti maalum vya chadema vya nini?

Lazima chama cha siasa kiwe na msimamo, kiwe na misingi. Ni utaahira kusema nyama ya kitimoto huli ila mchuzi wake unakunywa, hiyo ni utaahira wa kiwango cha juu.

Tuwaache CCM peke yao watuletee maendeleo ya haraka kwa miaka 5 ijayo, mnateseka nini wakati mnasema mkiwa wenyewe mnaleta maendeleo haraka?

Siku zote chama ni lazima kiwe juu ya mtu na sio mtu kua juu ya chama.

Muda wa kupeleka viti maalum ulikua bado sana, hadi vikao 3 vya bunge vipite ndio muda unakua umeisha.

Chama kimetoka kwenye uchaguzi wa kihuni juzi, bado watu wanauguza majeraha bado mabichi, hiyo haraka ambayo hao wanawake walikua nayo ya kwenda bungeni ni ya nini? Kama ni kwenda bado wangeenda.

Huu uhuni walioufanya umekihuujumu chama, wameshirikiana na serikali kuhujumu chama, hao huhitaji elimu ya chuo kikuu kuwashughulikia hata wakiwa 9900.
Excellent, good comment;Siongezi kitu wala kupunguza kitu
 
Kama ndivyo aida kihongosi anafanya nini bungeni kwa nini asifutiwe uwanachama
 
Mimi inaniwia vigumu sana kuamini kwamba viongozi wa vyama vyetu vya upinzani wana uwezo wa kujifunza kutokana na makosa yao ya nyuma. Wangekuwa na huo uwezo, leo hii CHADEMA wasingekuwa wanajiuguza majeraha makubwa yaliyoletwa na dhoruba la Viti Maalum vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sio siri, kufukuza makada waandamizi 19 ni msiba mkubwa sana kwa chama, ambao haukuwa wa lazima!.

CHADEMA ilipaswa kuteua Wabunge wa Viti Maalum mapema iwezekanavyo na kulimaliza hilo swala kwa amani. Mkakati wa kugomea Viti Maalum ni 'Political Maneuver' ambayo haikuwa na tija yoyote, kwa sababu kadhaa:

1. Historically, vyama vyetu vya upinzani vimewahi kususia mambo mengi na kufanya migomo ya aina mbalimbali, ambayo matokeo yake sote tunajua yalikuwa ni hasara zaidi kuliko manufaa kwa upinzani. Mifano ni mingi sana, lakini nitataja miwili tu mikubwa. Kwanza, mwaka 2015, Maalim Seif alisusia uchaguzi wa marudio Zanzibar akiamini kwamba kuna siku angepewa ushindi wa mezani na kuapishwa kuwa Rais wa Zanzibar.

Alisubiri mpaka muda wa uchaguzi mwingine ukafika bila kupewa ushindi wa mezani kama ndoto yake isiyokuwa na mbele wala nyuma ilivyomtuma. CUF paid a heavy price kwa sababu ya poor judgment ya viongozi wake. Pili, mwaka 2019, wapinzani walisusia uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Matokeo yake, CCM swept all seats. Hiyo ilikuwa poor judgment nyingine ya viongozi wa vyama vya upinzani.

2. Kuchukua viti maalumu hakuzuii chama kuendelea na mapambano yake yoyote yale. Chama bado kinaweza kupinga mahakamani matokeo ya uchaguzi kwenye majimbo na kata zote ambako wagombea wake walishindwa uchaguzi.

3. Kufikiria kwamba, kwa kususia viti maalumu, Tanzania itakuwa na general election do over ni uzembe mkubwa wa kufikiri. Kama Bob Amsterdam, Lissu’s foreign political mercenary, ameiambia CHADEMA kwamba kuna jumuiya ya kimataifa inayoweza kushinikiza nchi fulani kufuta matokeo ya uchaguzi wake na kufanya uchaguzi mwingine, amekidanganya chama mchana kweupe. National elections zinafanywa kwa mujibu wa sheria za nchi husika. Michakato ya kufuta matokeo ya uchaguzi nayo lazima ifanyike kwa kufuata sheria hizo hizo na mahakama za nchi husika. Hakuna international law inayoweza kutumika badala yake!

4. Kufikiria kwamba kugomea viti maalumu kutasaidia kuzishawishi jumuiya za kimataifa kuiwekea nchi vikwazo ni uzembe mwingine mkubwa wa kufikiri. I am not aware of any country that was slapped with economic and other sanctions because of election disputes. Hata kama hilo lingewezekana, effectiveness ya huo mkakati ni questionable. Ipo mifano mingi ya nchi ambazo zimeishi na vikwazo vya kimataifa kwa miaka kumi, ishirini. Nina uhakika Tanzania pia haiwezi kukubali kuacha kusimamia uhuru wake na sovereignty yake ili kutimiza matakwa ya mabeberu. So, if Tanzania weathers a five-year economic sanctions period, for example, how does that help resolve the 2020 election dispute?

Politics ni art ambayo haihitaji hasira. Viongozi wetu wa vyama vya upinzani inabidi wajifunze kuucheza huu mchezo bila kuumiza vyama vyao. A safe strategy ni kuchukua chochote kinachopatikana immediately kisha unaendelea kupambana kukitafuta kile kinachoweza kupatikana baadaye. Kwa kuwa viongozi hawasaini settlement agreement na mtu yeyote ambayo itawafanya washindwe kuendelea na mapambano, hakuna sababu ya kuwa na misimamo duni kama hii ya kususa na kufanya migomo.
Uchaguzi ule ulikuwa huru na wahaki??? Unaelewa tunaposema uchaguzi huru na wa haki??? Hatutaki matokeo tunataka mchakato. Kama mchakato wa kuwapeleka kina mdee bungeni haikuwa sahihi mf. Kufoji barua na kumtoa nusrat gerezani usiku... basi yote yatokanayo ni haramu. Ningekuwa najua dini yako ningeeleza zaidi haramu
 
Back
Top Bottom