Mkakati wa CCM wa kusomba wapenzi ...waingia doa baada ya kuwatelekeza uwanjani.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati wa CCM wa kusomba wapenzi ...waingia doa baada ya kuwatelekeza uwanjani....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtu66, Oct 3, 2010.

 1. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kikwete apokewa na mpasuko Singida

  Sunday, 03 October 2010 09:18

  Ibrahim Bakari, Iramba
  MGOMBEA urais wa CCM, Jakaya Kikwete ameonja adha ya mpasuko wa chama katika jimbo la Iramba Mashariki baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo na baadaye kuondolewa na Nec, Mgana Msindai kumtaka akemea makundi yaliyoibuka wakati wa kura za maoni.Kikwete ambaye amekuwa akikutana na mgawanyiko ndani ya chama hicho iliyotokana na makovu ya kura za maoni ndani ya CCM wakati wa ziara za kampeni zake, Msindai alimwambia mgombea huyo wa urais kuwa chama hicho katika jimbo la Iramba Mashariki kimepasuka na inahitajika jitihada za haraka kukinusuru.

  Kikwete alikuwa katika Kata ya Nduguti inayounganishwa na wilaya mpya ya Mkalamo katika mkoa wa Singida kuomba ridhaa ya wananchi aweze kurudi tena Ikulu.

  NEC ililiondoa jina la Msindai na badala yake Salome Mwambu kutangazwa kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya CCM kuwania kiti cha ubunge katika Jimbo hilo.

  Msindai aliyempokea Kikwete kwenye Kijiji cha Gumanda hadi kwenye mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Nduguti, baada ya kupewa nafasi alisema: "Kura za maoni zimepita, nimekubali matokeo.

  Aliongeza: "Na barua niliandika NEC kuwaeleza kukubaliana na hayo yaliyotokea, lakini bado mheshimiwa kuna makundi hapa...bado walioniunga mkono
  hawakubaliani na matokeo. Vilevile, mgombea ubunge aliyeteuliwa ana kundi lake, naomba kuanzia leo tuvunje makundi, tuchague CCM...narudi nyumbani na nitashirikiana na ninyi".

  Kura za maoni za kuwapata wagombea wa ubunge wa CCM zimeongeza ufa zaidi ndani ya chama hicho baada ya wanachama wake walioshjindwa na kuenguliwa katika mchakato huu kupinga matokeo na wengine kuamua kuwapigia debe wagombea wa vyama vya upinzani.

  Baadhi ya mikoa ambayo CCM imekubwa na mgawanyiko mkubwa kutokana na matokeo ya kura za maoni ni Mwanza, Iringa, Arusha na Mara.

  Akizungumza baada ya kupewa nafasi, Salome alikiri kuwepo kwa makundi hayo, lakini akasema: "Mimi kama mama, nitayabeba makundi yote na nitahakikisha tofauti zote zinamalizika."

  Alisema atahakikisha makundi yanaondoka na kufanya kazi ya kukinadi chama kiweze kuibuka na ushindi hapo Oktoba 31.

  Hali hiyo ilimlazimu Kikwete kusema: "Acheni makundi, hayasaidii, ninyi mko katika wilaya mpya, mkianza vibaya mtamaliza vibaya, kaeni chini mmalize tofauti zenu."

  Mapema akiwa njiani kwenda Nduguti, Kikwete alisimamishwa katika vijiji vinne huku wananchi wakilia shida ya maji, umeme, barabara, shule na
  huduma za afya.

  Kijiji cha kwanza kuzuiwa ni Ulemo ambacho walimwambia kuwa wanahitaji mbali na maji na barabara, kilio chao kingine ni ukosefu wa soko la kuuzia mazao yao na Kikwete kuwaambia ataangalia uwezekano wa kusaidia.

  Katika Kijiji cha Kinampanda sehemu kubwa alilakiwa na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu cha Kinampanda na baadhi ya wakazi wa eneo hilo na kuelezwa matatizo ya maji licha ya kuwa yapo lakini hayatoshelezi.

  Pia ukosefu wa wauguzi wa afya, walimu, maafisa wa kilimo kwa ajili ya kilimo cha kisasa.

  Hata hivyo, Kikwete aliahidi kushughulikia matatizo yao na pia aliwataka wote wanaosomea ualimu katika chuo hicho kujitahidi wamalize na ajira zipo kwa asilimia 100.

  "Someni, ajira ni ya uhakika, haina taabu na maslahi yanaendelea kuboreshwa," alisema Kikwete na kushangiliwa na wanafunzi hao. Akisikiliza matatizo katika Kijiji cha Gumanga, Kikwete alilalamikiwa suala la maji, umeme hasa katika Sekondari ya Gumanga pamoja na ukosefu wa malambo ya kuhifadhia maji.

  Mbali na kuahidi kushughulikia suala la maji, Kikwete aliahidi kusaidia kuwekwa umeme wa mionzi ya jua ili kuwafanya watoto wasome vizuri pamoja na walimu wao waweze kuandaa mitaala ya masomo kwa umakini.

  Jana jioni alihitimisha kampeni katika mkoa wa Singida kwenye Uwanja wa Namfua na leo anaanza ziara ya kuomba ridhaa mkoani Dodoma kabla ya kwenda Songea katika mkutano wa walimu.

  Wakati huo huo, mkakati wa CCM wa kusomba wapenzi na wanachama wake kuwapeleka kwenye mikutano yake ya kampeni ulikuwa uligeuka shubiri kwa wagombea udiwani jimbo la Bunda, kufuatia watu hao kuwataka wawanunulie chakula baada ya kutelekezwa na chama.

  Awali wanachama na wakereketwa hao walidaiwa kuahidiwa usafiri na posho ya chakula na uongozi wa chama wilaya, ahadi ambayo ilitolewa hata kwa vikundi vya burudani toka maeneo mbalimbali jimboni humo.

  Wakizungumza na Mwananchi kwa sharti la kutotajwa majina yao, baadhi ya wagombea hao walisema kuwa walilazimika kubanwa na wapiga kura wao baada ya chama wilaya kuwatelekeza bila kuwapa chakula zaidi ya usafiri wa malori.

  "Tumelazimika kuingia kwenye madeni maana wapiga kura wanalia. Baada ya kuachwa
  walianza kutafuta namna ya kusaidiwa kwa kutubana sisi," alisema mmoja
  wa wagombea jina tunalo.

  Mmoja wa wagombea hao alisema wanachama hao walisombwa asubuhi, wengine hawakuwa wamekuwanya chai.

  "Baadhi tumelazimika kutumia laki moja (Sh100,000) kuwahudumia wanachama ambao waliletwa bila mpango maalumu. Hii ni hatari na wengine tumelazimika kukopa fedha ili kuwasaidia," alisema mmoja wa wagombea hao.

  Source: Wananchi
   
 2. u

  urasa JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  :decision:HAPA MANYONI WATU WANASOMBELEWA NA LORI T 307 AFL,
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Epa mwaka huu haipo inawezekana kwa sasa wanatumia ela za loan board kwa kuzipiga kwa fixed account pale CRDB ili angalau chama kisije filisika
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Nani kakuambia Epa mwaka huu hakuna. Wamefyatua sehemu nyingine na litakajokuja kujulikana baada ya uchaguzi, wewe subiri tu.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Dalili hizi ni mwanzo wa mwisho. Hivi Dr Slaa ataapishwa tarehe gani?
   
Loading...