Mkakati wa CCM ni kuwaondoa Mh W.Slaa na Mh. F. Mbowe kwenye Kinyang'anyilo cha Urais 2015

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Ndugu wana jamvi leo nakuja na mada hii ili nipate kuthibitishiwa. Mada ni kwamba, CCM wana uhakika wa kupoteza utawala wa nchi ifikapo 2015. Sasa ili kuhakikisha kwamba hilo halitokei(kupoteza utawala) ccm na serikali yao wakitumia idara ya Usalama wa Taifa na Vyombo vya Ulinzi ni kusuka zengwe ambalo litahakikisha mh. W. Slaa, F. Mbowe na viongozi kadhaa wa Chadema wanatiwa hatiani kabla ya 2015. Hili litafanya chadema wakose watu imara wa kushindana na ccm.

Aidha, kuna madai kwamba, mkakati wa pili wa ccm ni kuhakikisha kwamba iwapo chadema watashinda mwaka 2015; ccm wataanzishavurugu na machafuko nchini. Kupitia machafuko hayo watu kadhaa watauwawa (kama ilivyofanya Pemba chaguzi za nyuma). Kwa machafuko hayo, jumuiya ya kimataifa na Afrika watataka iwepo serikali ya mseto baina ya ccm na chadema. CCM watachukua urais na Chadema watapewa umakamu ama uwaziri mkuu. Kwa mfumo huo chadema itajiishia kimkakati kitabaki kuwa kama chama cha CUF huko Zanzibar.

CHANZO cha Taarifa hizi: Viongozi kadhaa wa taasisi za dini na kutoka Usalama wa nchi.
 
Hienda nikawa wa kwanza na wa mwisho kuiona hii thread! Na wala siichangii.
 
Hilo sio la kupuuza, ingawa hukuonesha ni namna gani watawatia hatiani hawa makanda.

Lakini hata wakiwa gerezani still both are and will always be our chosen leaders. CDM is more than few individuals anyway.
 
Mbowe aligombea 2005 akaburuzwa mbaya

Slaa akagombea 2010 akatupwa mbaya

Sasa CCM itawaogopaje hao watu ambao uzoefu unaonyesha walishindwa?

Hatutaki uongo na umbea hapa Jamvini.
 
Naomba muisome hii hoja vizuri. Tanzania ina Uranium! serikali ya mseto is ideal kwa wazee wa vyandarua!
 
Hadithi yako inatufundisha nini?

Hii inaweza ikawa ni fundisho zuri sana kwa kila mpiga vita ufisadi ktk Nchi yetu!

Hakika hili siyo la kupuuza hata kidogo.
Hawa mafisadi siyo mchezo ni JANGA kwa Taifa letu!
 
Mbowe aligombea 2005 akaburuzwa mbaya

Slaa akagombea 2010 akatupwa mbaya

Sasa CCM itawaogopaje hao watu ambao uzoefu unaonyesha walishindwa?

Hatutaki uongo na umbea hapa Jamvini.
Jackson michael alikwishakufa,je na wewe ni mfu rasmi usiyejielewa?
 
Ndugu wana jamvi leo nakuja na mada hii ili nipate kuthibitishiwa. Mada ni kwamba, CCM wana uhakika wa kupoteza utawala wa nchi ifikapo 2015. Sasa ili kuhakikisha kwamba hilo halitokei(kupoteza utawala) ccm na serikali yao wakitumia idara ya Usalama wa Taifa na Vyombo vya Ulinzi ni kusuka zengwe ambalo litahakikisha mh. W. Slaa, F. Mbowe na viongozi kadhaa wa Chadema wanatiwa hatiani kabla ya 2015. Hili litafanya chadema wakose watu imara wa kushindana na ccm.

Aidha, kuna madai kwamba, mkakati wa pili wa ccm ni kuhakikisha kwamba iwapo chadema watashinda mwaka 2015; ccm wataanzishavurugu na machafuko nchini. Kupitia machafuko hayo watu kadhaa watauwawa (kama ilivyofanya Pemba chaguzi za nyuma). Kwa machafuko hayo, jumuiya ya kimataifa na Afrika watataka iwepo serikali ya mseto baina ya ccm na chadema. CCM watachukua urais na Chadema watapewa umakamu ama uwaziri mkuu. Kwa mfumo huo chadema itajiishia kimkakati kitabaki kuwa kama chama cha CUF huko Zanzibar.

CHANZO cha Taarifa hizi: Viongozi kadhaa wa taasisi za dini na kutoka Usalama wa nchi.

Unachokisema haiwezekani, Chadema sasa hivi hata asimame Dogo Janja, anashinda hata asimame nani kupitia Chadema anasimama..

Kuna watu wengi sana CDM, wengine wako CCM na wengine wako Jeshini na wengine wako UWT.

Hakuna hujuma zozote zitakazofanikiwa.

Tatizo la CCM ni waTZ wamewakataa sasa hata waifanyie nini CDM bado watashindwa tu...
 
Hayo mawazo yako kawaelekeze wanafunzi wa chekechea, ccm wafanye hivyo hawajipendi? Ccm wote wenye akili wanaufahamu muziki wa cdm ulivyoutamu. Chadema ni zaidi ya unavyoielewa, je, waweza kuzuia mafuriko kwa mchanga? 2015 ni green light Ikulu.
 
Mbowe aligombea 2005 akaburuzwa mbaya

Slaa akagombea 2010 akatupwa mbaya

Sasa CCM itawaogopaje hao watu ambao uzoefu unaonyesha walishindwa?

Hatutaki uongo na umbea hapa Jamvini.

2005 ni tofaut na 2010 pia 2010 itakuwa tofaut na 2015..huhitaj elimu ya darasa la saba kulijua hili..
 
Jamani kuliko kumkejeli mleta hoja, ni vizuri kutilia maanani ayasemayo na kuyachambua. Katika kupanga mikakati hapa duniani hupaswi kupuuzia kila kitu, zaidi sana kumbukeni usemi huu - Never underestimate your opponent.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Watu wanapopuuzia thread kama hii unaelewa ni jinsi gani watu wanavopuuzia hali halisi ya kisiasa sasa hivi. Hivi watu wanafikiri ccm itaachia madaraka kilaini tu. Lazima kutokea misukosuko, watu kuuawa na hasa viongozi ndio hatua inayofatia sasa hivi.
 
Jamani mleta mada sio wa kupuuzwa hata kidogo kwani ni wakufiliwa sana pia inabidi chama kisipuuze mawazo kama haya kwani tunatakiwa kujua kwamba ccm nao wapo vitani wakibuni njia usiku na mchana jinsi ya kuimaliza chadema so ni vyema watu tujadili content halisi ya jambo lenyewe kuliko kuleta kejeli humu ili kwa pamoja 2015 tuweze kuiweka CDM madarakani.
Peoples..........!
 
Watu wanapopuuzia thread kama hii unaelewa ni jinsi gani watu wanavopuuzia hali halisi ya kisiasa sasa hivi. Hivi watu wanafikiri ccm itaachia madaraka kilaini tu. Lazima kutokea misukosuko, watu kuuawa na hasa viongozi ndio hatua inayofatia sasa hivi.
Swala siyo kupuuzia, swala kwamba kuna watu Ubongo wetu haturuhusu kuingiza vitu vya kijinga na kusadikika, Usalama wa Taifa unaripoti kila kitu kwenye Intelegence ya Chadema na ndio maana hata mawasiliano ya Zitto Kabwe na Deputy Director wa Idara ya Usalama wa Taifa yalianikwa hadharani.

Sasa msidhani kila mtu ambaye yupo hapa JF ni mtu wa kulishwa habari za kusadikika, hao Usalama wa Taifa unaowaogopa wewe ndio hawaitaki hata kuisikia CCM ikirudi madarakani, wamebaki vibaraka wachache sana kwenye hiyo Idara ndio wanatumika na CCM kwa sababu hata wao siyo wasafi ni mafisadi pia.
 
Mbowe aligombea 2005 akaburuzwa mbaya

Slaa akagombea 2010 akatupwa mbaya

Sasa CCM itawaogopaje hao watu ambao uzoefu unaonyesha walishindwa?

Hatutaki uongo na umbea hapa Jamvini.

Lisemwalo lipo na kama halipo basi lipo njiani si ajabu ukajakutana nalo unapoendelea kufikilia kuwa nchi iko shwari!
 
hata kama habari chanzo chake si sahihi ila mawazo ya mleta mada hayapo mbali sana na ukweli.
 
Back
Top Bottom