Mkakati wa CCM kujivua gamba ni zao la Utafiti kweli au Majungu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati wa CCM kujivua gamba ni zao la Utafiti kweli au Majungu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uwezo Tunao, Apr 28, 2011.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WILISONI, KATUPE MBALI HIYO RIPOTI KABLA HAIJAANGAMIZA ZAIDI CCM NA TAIFA KWA UJUMLA MAANA HATA KIDOGO HAIKUA ZAO LA LILE JINA LA UBATIZO LA 'SCIENTIFIC RESEARCH' ULIOIPA LA SIVYO CCM MTAJIKUTA MKITOA TIBA YA GOTI KWA UGONJWA WA KICHWA!!!

  [​IMG]

  Mr Archimedes & the Scientific Research

  [​IMG]

  Mr Ndiamukama & the Scientific Research

  Ama kweli la kuvunda halina ubani. Inakuaje Wilson NdiaOmukama na timu mpya ya CCM ianze safari ya kujivua gamba kwa hatua ya kuzua maswali kiasi hiki??

  Willisoni NdiaOmukama kaanza kazi CCM kwa guu baya tena la hatari LA KUBUNI, KUANDIKA NA KUPELEKA MBELE YA KAMATI KUU NA HALMASHAURI KUU ya chama chake uongo takatifu juu ya Jamii Forums na WAMILIKI WA KUCHONGA kukiingizwa humo CHADEMA shauri ya kupendwa na vijana wengi wenye umri wa DOTI KOMU nchini.

  Hakikakwa wale watu wanaojua kitu 'SCIENTIFIC RESEARCH' inavyopashwa iwe basi mpaka sasa hivi watapendekeza bila ajizi Mzee NdiaOmukama akajipeleke mwenyewe jela Ukonga kwa kuidhalilisha fani ya watafiti na wasomi nchini. Ni Scientifi Reseach gani hiyo isiweza kuhimili Test of Time wakati hata mwezi haujaisha tangu watangaze matokeo yake???

  Mzee Achemidis, mwanasayasi aliyebobea duniani, siku alipoona ameruka na kupiga mbizi ndani ya kijibwawa chake cha kuogelea nyumba kuja kuibuka na kuanza kujipangusa pangusa maji usoni ili aweze kuona vizuri mandhari yanayozunguka bwawa lake huku akiendelea kufurahia maisha ndani ya bwawa hilo, ghafla alishangaza kila aliyekwepo (wanafamilia) maeneo hayo hapo pale alipochomoka toka ndani ya bwawa huku akipiga kelele kwa kujishangilia kwamba 'LEO HII NIMEGUNDUA UKWELI, JAMANI LEO NIMEVUMBUA JAMBO ZITO LITAKALOCHANGIA KUBADILISHA KABISA SURA YA ULIMWENGU NA JINSI TUNAVYOENENDA'.

  Mara mama Archemidis naye akachomoka jikoni na mwiko mkononi kwa shauku ya kutaka kufahamu kitu gani kimemsibu mumewe ndani ya bwawa lao la kifahari. Kule kuingia tu sebuleni mara anamkuta baba huyu yuko kifua wazi, kalamu na karatasi mkononi huku mwili mzima ukichuruzika maji na akili kama imeruka vile kiasi cha kutoweza kutambua uwepo wa mkewe pemeni mwaka.

  Mara mama akaona Mzee Archemidis akipima uzito mdoli kwenye mzani mara akitubukiza huo mdoli kwe maji aliyoyaleta sebuleni kwenye karai karibia kujaa pomoni lakini kwa kuacha japo kanafasi kwa juu. Katika kutumbukiza kule huo mdoli mara maji yakamwagika chini pale sebuleni na hata kumfanya mama akasirike dalili za kuhitajika kurudia kupiga deki.

  Ghafla tena Mzee wa watu akalipuka kwa sauti kuu akisema 'Hakika leo Nimefanya Uvumbuzi wa miaka nenda rudi dumu daima' itakayochangia kuboresha hadhi na ubora wa maisha ya binadamu. Mara kaanza kuangusha maandishi micharazo kibao mfululuzi hata maji yote mwilini yakakauka kau!!

  Ni tangu siku hii ndipo kitu KANUNI ZA MZEE ARHEMIDIS (Mgiriki huyu) zilipozaliwa zikisema kwamba mwili na au kitufe chochote kikizamishwa kwenye karai iliyojaa maji siku zote husababisha kipimo cha maji yale kwenye karai kumwagika kwa kadiri sawasawa kwa ulinganifu wa uzito wa mwili au kitufe husika!!!

  Na kwa wale wadadisi wa mambo mnajua kwamba kwa msaada wa Kanuni za mzee huyu leo hii tunaona chombo kikubwa zaidi ya Meli Duka-la-Vitabu-laDunia MV Dulos likitia nanga hapo Magogoni Dar es Salaam na watu kibao kumiminika ndani kujinunulia vyakusoma LAKINI BILA CHOMBO HICHO KUZAMA - ajabu ilioje hiyo; ni ule 'ukichaa' na nusu kurukwa akili kwa yule Bahari Mgiriki Mzee Archemidis kwenye raha zake tu pale nyumbani.

  Ninachosema hapa ni kwamba ugunduzi ule ulikua ni zao la kile kinachoitwa SCIENTIFIC RESEARCH: UTMOST CURIOSITY & INQUISITIVENESS ambayo hadi leo imechangia kweli kufanya sura ya ulimwengu kubadilika, mifumo na ubora wa maisha ya binadamu kuwa nzuri zaidi.

  Jambo hili lasadikiwa kutokea zaidi ya miaka 2000 iliyopita lakini Uvumbuzi huo bado unabeba ukweli usiopingika hata leo - THE FACTS OF THE MATTER HAS SINCE STOOD GROUNDS THE TEST OF TIME.

  Sasa je huu utafiti wa Mzee Wilsoni NdiaOmukama na Profesa Mmoja wa Dodoma naomba sana watu mnijulishe kama kweli ulikua SCIENTIFIC RESEARCH kweli au majungu ya mfamaji baada ya kuona Watanzania tunakikataa CCM en masse??

  Kama Jamii Forums huenda ilitajwa visivyo kwenye ripoti ile ambayo hivi sasa inatumika kama a Working Document ya CCM na serikali yake je kuna mtu yeyote atakayeendelea kuamini chochote kingine kilichoandikwa mle kuwa na ya haki na haki mtupu na kwamba gamba la CCM kuvuliwa ni zao lake na wala si matokeo ya shinikizo toka CHADEMA???

  Mzee NdiaOmukama hebu kaa chini na huyo li-Nape lako mkatafakari juu ya huo Waraka wa Magamba kabla hamjaadhirika zaidi kwenye kuendelea kunadi hicho kinachodhihirika hivi sasa kuwa ni Uozo na Majungu ya watu waliojimulia kukaa chini ya mti mahala na kujiandikia kifurahishacho roho na mitazamo binafsi na hatimaye kulibatiza jina SCIENTIFIC RESEARCH iliyoshindwa kuhimili mikikimikiki ya nyakati hata kabla ya mwezi kwisha.

  Hebu kajifunzeni kwanza kutoka huyo Mgiriki hapo juu ili CCM ije na mkakati mwingine maana huu wa Magamba na kusingizia JF ndio hiyo tayari wengine tunaisoma KULE KUDODA hata kabla ya utekelezaji wake.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Haingii akili mtu kusema kafanya utafiti lakini asiweze hata kufika tu BRELA pale barabara ya Lumumba Jiji Dar es Salaam kujua wamiliki wa kweli wa Jamii Forums ni akina nani hasa badala ya kuendeleza hii hulka ya CCM kutafuta kupachisha kila baya kwao kuwa kisababishi chake ni CDM.

  Isitoshe, kule watu kujiunga na au kujiondoa katika huu mtandao wa JF ni kwa hiari tu ya mtu na wala si kwa utaratibu wa kukaribishana mle watu wa chama au rika fulani tu hapa. Kwa mtindo huu inamaani kuna ripoti ngapi zimewahi kuandikwa na baadhi ya wana-CCM wakipenyeza tu maoni binafsi na kuyaita matokeo ya SCIENTIFI RESEARCH hapa nchini???

  Hebu tupeni mbali hiyo ripoti kabla haijaiangamiza milele CCM maana huko mbele ya safari sisi vijana tungependa kukiona kikiwa ni chama imara cha upinzani.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Siku zote kitu chochote mkakati ukijengwa juu ya misingi potofu na maoni binafsi yenye majungu ndani yake basi yale yooote yatakayofuatia kiutendaji baada ya hapo ni kupoteza tu muda na rasilmali hadimu bila sababu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Mpiga porojo mwingine kaingia huyo,hamna jipya hapo.
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Bila kueleza baada ya kuua Azimio la Arusha sasa wanasimama wapi. The triplets are standing in Zanzibar Declaration. Muakama and the company are standing to loose. they dont have a declaration that they are standing for. Hovyo kabisa.:noidea:
   
 6. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama aliyekuja na hilo wazo ni yule jamaa wa Chalinze, basi ni majungu mara mia.
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Maana kila kitu kinapuaya na kauli kukinzana humo na cha zaidi tunaona tu chuki binafsi za mtu hasa dhidi ya JF na kuamua kuzunguka nayo nchi nzima eti huko ndio kujivua gamba huko!!!

  Sawa tu na kipindi kile niliposhinwa kuielewa serikali ya CCM ilipoibuka na dhana ya SABABU ZA KIINTELIJENSIA kuzuia maandamano ya wapinzani nchini, hata sasa bado nasubiri kuridhishwa juu ya kitu gani hasa ni SCIENTIFIC RESEARCH katika hii ripoti ya NdiaOmukama na Profesa wa Dodoma.

   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu nadhani kikundu fulani ndani ya CCM haikujali kufanya Homework yake vya kutosha na wala hawakujiuliza maswali yooote mgumu katika mazingira kabla ya kuundwa kwa Mkakati Gamba inayo-demonise JF, mazingira wakati wa utekelezaji wake na mazingira baada ya yote.

  I can see CCM emerging weaker than one can imagine with this Vangeful Gamba Strategy on sauti huru nchini na hasa kwa wana-JF. Everything gonna be counterproductive and even more difficult is a realistic and most liberal minds are NOT brought to work, Full STOP!!!
   
 9. I

  ISIMAN Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  msingi mbovu hauwezi kuhimili jumba hata kidogo kujivua gamba kumeleta mabadiliko gani zaidi ya kiinimacho kamawatu niwale wale miongozi ileile na mazingira ya kiutendaji ni yaleyale
   
 10. I

  ISIMAN Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm iliteleza mara baada ya kufifisha azimio la arusha na kutoweka misingi mingine ya kimaadili ndani ya chama sasa tumtake nani amfunge paka kengele labda watanzania
   
 11. I

  ISIMAN Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nilini viongozi watakuwa waadilifu sasa nadhani nivema viongozi wote wajiuzuru na watanzania wajipange kwa kupata safu mpya ya viongozi kwa mikataba mipya ya kazi hatuwezi kuwa na viongozi wanoa kiuka maadili kila kukicha na tukawaacha haiwezekani sisi twaumia na maisha magumu wao wanakula kwa umaskini wa migongoni mwetu
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mzee Wilsoni unayasoma vema maoni haya?? Chonde jihadhari na tiba ya goti kwa maradhi ya kichwa hapo kwani hutokaa usikie mgonjwa wako kapona kitu chochote kile!!!

   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Je, siku 90 hizo CCM kitatoboa????????????
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM KAVUENI HARAKA HILI GAMBA LA KUGEUZA KEKI YA TAIFA KUWA KEKI YA CHAMA CHA MAPINDUZI PEKE YAKE ILI TUKAFAIDI SOTE HAKI ZETU SAWA TU NA VILE TUNAVYOSHIRIKI KWA PAMOJA KULIPA KODI BILA UBAGUZI!!!!

  Kama kuna gamba mojawapo kubwa linalotukera sisi wananchi ile mbaya ni kule Watanzania kushiriki sote kwa pamoja kama taifa kulipa kodi kuiendeshea serikali yetu.

  Lakini mwisho wa siku kero zinaanzia pale ambapo wenzetu ndani ya CCM wanageuza kwa makusudi kabisa mali ya pamoja na kuwa mali yao binafsi, Maslahi ya Umma inageuka kuwa Maslahi ya Chama ambayo inalindwa kinafiki kweli kweli.

  Nasema CCM hugeuka KUFANYA KINACHOTAKIWA KUWA KEKI YA TAIFA KUWA KEKI YA CHAMA na kwenda mbele zaidi kututmbia kwa kutumia dhana kama vile 'chama kimeshika hatamu' na wala sisi wananchi hatumo kabisa kwenye ramani yao.

  Hili ni gamba sugu sana kuweza kuvuliwa na CCM pale wanapogeuza nafasi za ajira katika ngazi zote za maamuzi kuwa ni haki na hifadhi maalum siku zote kwa wana-CCM tu.

  Hebu fikirieni tu kwamba bila hata aibu, baada ya kuhama mfumo wa chama kimoja bado CCM kihodhi ajira zote za taifa tangu nafasi za balozi wa nyumba 10, kata, wilaya, mikoa na ubalozini na mashirika mbali mbali ni haki ya wana-CCM tu kiupendeleo badala ya kutumia ushindani wa wazi kwa wote. Kimsingi ni nafasi za ajira ni za taifa zima bila kujali tofauti zetu za kiitikadi kisiasa, kidini, kijinsia na kiumri.

  Cosequently, this most unadmirable situatio logically leads an even more serious socio-political and economic most nagging issue in the country for which we the youth are just prepared to die fighting to undo - an official exclusive political system entrenching a deliberate unequal distribution of national resource!!! Hili kamwe halikubaliki hata kwa dawa hivyo ama mjivue hili gamba mapema au tuje tukawavue wenyewe Nguvu ya Umma.

  [​IMG]
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Archimedes of Syracuse
  (Greek: Ἀρχιμήδης)

  [​IMG]

  Archimedes Thoughtful
  by Fetti (1620)

  Hapo ni vile Mzee Archimedes alivyokua 'anabundi' kufanya Scientific Research ambayo matokeo yake yanaheshimika hadi leo hii kote duniani; sasa hiki kinachodaiwa na CCM kufanya sijaelewa bado.
   
 16. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280

  Dah mkuu umenikumbusha mwanazuoni huyu nguli.THANKS...,kitufe wapi?
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KAMA VILE KUNA MATATIZO YA KIFAMILIA KWA HUYU MAMA KOMBANI HIVYO KUANZA KUTAPIKIA SHIDA BINAFSI KWENYE MASUALA MAZITO NA NYETI SANA KITAIFA.

  Katiba ya nchi si mali ya CCM wala serikali yake kujipangia wanachokitaka wao. Hakika tunaweza kuivumilia hii serikali ikamalize muda wake itupishe tukaweke serikali mpya hapo 2015 LAKINI ikija kwenye suala la KUUNDWA KWA KATIBA YA WALALAHOI nchini; hapo lolote lawezekana kwa Nguvu ya Umma wakati wowote ule bila silaha bali maandamano ya kufa mtu!!!

  Sasa naanza kuhisi kwamba huyu mama yetu huenda hana kabisa AMANI YA KIFAMILIA ndani ya maisha yake. Siku zote hakuna mbolea safi ya roho ya binadamu kama mtu kubahatika amani ndani ya familia yake.

  Hakika inashangaza jinsi alivyo reckless huyu mama hivyo kupelekea kwake kuwa ni mtu wa kukurupuka na kuchezea masuala nyeti kiasi hiki kitaifa hata bila kutambua kwamba suala la katiba ni wembe mkali sana unaoweza kumkata si yeye tu bali hadi bosi wake kama ambavyo tunavyoona dalili zote mara baada ya bunge la mwezi Juni.

  Wanaomjua vema Mama Kombani vipi maisha yake ndani ya familia huyu????
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hadi hapo ambapo hili Gamba la Kimfumo la CCM kuja kuweza kuvuliwa ...!!!!!!!!!!!!

   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Vijana CCM Arusha mapande mapande

  Paul Sarwatt, Arusha​
  Aprili 27, 2011 [​IMG]
  [​IMG]Mwenyekiti wa zamani adundwa, ajeruhuwa
  [​IMG]Yadaiwa ajikweza kwa watuhimiwa ufusadi
  [​IMG]Mwenyewe ang'aka, ashitaki Polisi

  HALI ya mambo ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV-CCM) mkoani Arusha imezidi kuwa mbaya kutokana na hatua ya viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo kutiana makonde hadi Mwenyekiti wake wa zamani Ally Bananga kujeruhiwa vibaya.

  Kuvurumishiana huko kwa makonde kulitokea wiki iliyopita katika Mtaa wa Bondeni katikati ya mji wa Arusha baada ya kundi la viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo kutoka Kata ya Kati, kumshambulia Bananga kwa makonde na mateke na kumjeruhi vibaya hadi akapoteza fahamu kabla ya kuokolewa na wasamaria wema.

  Baadaye Mwenyekiti huyo wa zamani ambaye pia ni kada maarufu wa CCM mjini hapa alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha kwa matibabu kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani kuendelea kuuguza majereha yake.

  Tukio hilo limekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya kuitishwa kwa mkutano wa vijana zaidi ya 50 katika ofisi ya Kata ya Unga Limited uliotoa tamko la kuunga mkono kuvuliwa ujumbe wa Baraza la Wilaya ya Arusha mjini Mrisho Gambo Machi 28 mwaka huu.

  Wanachama hao wa UV-CCM walichukua uamuzi huo wakimtuhumu Bananga kuwa anatumiwa na kundi la mafisadi kuvuruga hali ya amani ndani ya Jumuiya hiyo hasa baada ya Mwenyekiti wa huyo wa zamani kuitisha kikao kisichotambulika akishirikiana na vijana wapatao 30 na kutoa tamko lililolenga kuwasafisha mafisadi.

  Bananga anatuhumiwa kuwa yuko katika mradi wa kumsafisha waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, na mara kwa mara amekuwa akionekana kuwa pamoja na mtoto wa kiongozi huyo, Fred Lowassa, katika "shughuli za kisiasa zisizo rasmi".

  Habari zinadai kuwa mradi wa kumsafisha na kumsadia Lowassa ni wa muda mrefu lakini sasa umeanza kujengewa sura mpya baada Halmashauri ya Taifa (NEC) katika kikao chake cha wiki mbili zilizopita mjini Dodoma kuazimia kutaka kuwatosa chamani Lowassa na watuhumiwa wengine wa ufisadi Andrew Chenge na Rostam Aziz.

  Inadaiwa ya kuwa kutokana na tishio hilo jipya la kutaka kuondolewa ndani ya chama, kundi la Lowassa sasa linapanga mikakati mipya ambayo ni pamoja na kuwatumia baadhi ya wanachama kutoa matamko yanayolenga kuwatetea na pia kuwatumia viongozi wa dini na taasisi nyingine kutoa kauli zinazoashiria kuwaunga mkono.

  Gambo anadaiwa kuvuliwa nafasi yake ya ujumbe wa Baraza Kuu Wilaya Arusha Mjini katika mazingira ambayo hadi sasa hajawekwa wazi kwenye mkutano wa Baraza Kuu uliofanyika wilayani Longido mwishoni mwa Machi.

  Tayari Bananga ambaye aliyejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili, amefungua taarifa za tukio hilo katika Kituo cha Polisi cha Kati na kupewa hati ya Taarifa Polisi namba AR/RB/4697/2011 mashitaka ya kutishia kuua kwa kisu na shambulio la kudhuru mwili.

  Ingawa hadi mwishoni mwa wiki iliyopita hakuna mwachama wa UV-CCM aliyekuwa ametiwa mbaroni kuhusiana na tukio hilo, Polisi mkoani hapa tayari wameanza uchunguzi wa tukio hilo.

  Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zinaeleza kuwa vijana walichukua sheria mkononi kumpiga Bananga ni wale wanaomwunga mkono Gambo ambao wana msimamo wa pamoja na wanaunga mkono hatua zilizochukuliwa na Mwenyekiti wao Taifa Rais Jakaya Kikwete ya kutaka kukisafisha chama hicho katika harakati zake za kujivua gamba.

  "Kwanza Bananga si mjumbe wa kikao chochote cha vijana katika Wilaya na Mkoa wa Arusha, sasa hatua yake ya kuitisha mkutano wa vijana ilikuwa na maana gani kama si anatumiwa tu na mafisadi. Tunamfahamu vizuri sana.

  Anaganga njaa tu na anatumia jukwaa la siasa kujipatia riziki lakini si kwa ajili ya maslahi ya chama chetu na ndiyo maana watu hawafurahishwi naye," anasema mmoja wanachama aliyekuwapo kwenye tukio lililozaa Bananga kupigwa.

  Mwanachama huyo wa UV-CCM alidai kuwa kinachofanyika kwa sasa katika jumuiya hiyo ni baadhi ya wanachama wao kupewa fedha na mafisadi ili watoe matamko yanayolenga kuwasafisha mafisadi hao mbele ya jamii ili waonekane kuwa ni viongozi safi na mfano halisi ni tamko lililotolewa na Bananga na wenzake.

  "Bananga alikuwa Mwenyekiti wa UV-CCM aliyemaliza muda wake na hana nafasi yoyote ya kisiasa zaidi ya kuwa mjumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa wa chama sasa inashangaza ameingiaji katika masuala ya vijana wakati kiuongozi alishamaliza muda wake? Hapo utagundua kuwa ni wazi anatumiwa na kundi la watu kwa maslahi yao ya kisiasa, " alisema mwanachama huyo wa UV-CCM.

  Lakini akizungumza na Raia Mwema mwishoni mwa wiki, Bananga alithibitisha kuwa alishambuliwa na kujeruhiwa na kundi la vijana wanachama wa jumuiya hiyo ya vijana katika Mtaa wa Bondeni katikati ya ya mji wa Arusha baada ya kundi hilo kumtuhumu kuwa anashirikiana na mafisadi kukihujumua chama hicho.

  "Ni kweli ndugu yangu nimepigwa na kudhalilishwa hadharani wakinituhumu kuwa nashirikiana na mafisadi kuhujumu chama. Lakini mimi nahoji hao mafisadi ni akina nani ndani ya CCM?.....ni jambo la kushangaza sana kuwa hatua tuliyofikia ni hatari kwani inaweza kupoteza maisha ya mtu," alisema Bananga kwa masikitiko.

  Aliongeza: " Katika tamko letu tulieleza kwa uwazi kuwa hatujatumwa na mtu wala kiongozi yeyote, bali tunataka ukweli ufahamike kuhusu Gambo juu ya hatua ya Baraza kumsimamisha uongozi wa Baraza la Wilaya ya Arusha Mjini."

  Kuhusu madai kuwa amekuwa katika harakati za kumsafisha Lowassa, mwenyekiti huyo wa zamani wa UV-CCM alikanusha madai hayo na akaeleza ya kuwa urafiki wake na mtoto wa Lowassa (Fred) ni wa muda mrefu kabla hata hawajiaingia katika masuala ya siasa.

  "Nimefahamiana na Fred Lowassa tangu tulipokuwa tunasoma sekondari, yeye akiwa Ilboru Sekondari mimi nikiwa Arusha Sekondari mwaka 1992. Tulikuwa tunakutana katika michezo ya shule za sekondari na tumekuwa marafiki hadi leo," alisema.

  Aidha hali ni tete zaidi baina ya makundi yanayosigana ndani ya umoja huo baada Katibu wa UV-CCM Mkoa wa Arusha, Abdalah Mpokwa, kumwandikia Gambo barua mbili tofauti ndani ya siku moja.

  Katika barua ya kwanza yenye kumbukumbu namba UV/M15/2/376 ya Machi 29, 2011, Katibu huyo wa UV-CCM amwemwandikia Gambo kuwa umoja huo umepokea malalamiko dhidi yake kuhusu kukihujumu CCM na mgombea ubunge wake wa Jimbo la Arusha Mjini Dk. Batilda Burian na kumpigia kura mgombea wa CHADEMA, Godbless Lema.

  Katika barua ya pili, ambayo ina kumbukumbu namba UV/M15/2/377 yenye kichwa cha habari: Kuvuliwa ujumbe wa Baraza Kuu la Wilaya, Katibu huyo anaandika kuwa Baraza hilo limemsimamisha nafasi ya ujumbe wa Baraza kwa mujibu wa kanuni namba 78 kutokana na tuhuma zilizoelekezwa kwake.

  Haikufahamika mara moja ni utaratibu upi uliotumika kumwandikia mjumbe huyo barua ya tuhuma zake na siku hiyo hiyo akaandikiwa barua nyingine ya kumsimamisha uongozi wa jumuiya hiyo. Alipoulizswa juu ya barua hizo mbili Katibu Mpokwa alishindwa kutoa maelezo.

  " Siko katika nafasi ya kutoa ufafanuzi kwa sasa. Nitafute ofisini pindi nitakapokuwa na nafasi," ndivyo alivyojibu Mpokwa alipoombwa na Raia Mwema kufafanua ujumbe wa barua hizo mbili alizomtumia Gambo na kisha akakata simu.

  Hata hivyo, katika hali ya ambayo inaonyesha kuwa kuna mpasuko mkubwa ndani ya umoja huo, uongozi wa Wilaya ya Arusha Mjini umekataa kutambua barua hizo na unasisitiza kuwa unamtambua Gambo kama mjumbe halali wa Baraza la Vijana Wilaya ya Arusha.

  Aidha, katika hali inayoonyesha kuwa uongozi wa jumuiya hiyo u vipande vipande, Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Mkoa wa Arusha pia linadaiwa kutoa maazimo mawili tofauti katika mkutano uliofanyika wilayani Longido Machi 28 mwaka huu hasa kuhusu suala la Gambo.

  Katika hatua ya kwanza tamko linalodaiwa kuandaliwa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, James Millya, lenye maazimio matano, linatangaza kumchukulia hatua Gambo kutokana na tuhuma zilizotajwa na zinazoelekezwa kwake.

  Katika tamko jingine, lililotolewa na Katibu wa Mkoa, linalodaiwa kuwa ndilo tamko sahihi la Baraza Kuu, jina la Mrisho Gambo halitajwi, na badala yake Baraza linaeleza kuwachukulia hatua viongozi wote wa jumuiya waliokiuka nidhamu na maadili kwa kuzingatia taratibu na kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

  Lakini habari za ndani ya jumuiya hiyo zinaeleza kuwa kutofautiana kwa maazimio ya kikao hicho kunatokana na hatua ya Millya kuandaa maazimio ya kwanza na kuingia nayo ndani ya ukumbi huku tayari mkutano ukiwa umekwishakuanza baada ya kufunguliwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Arumeru, Esther Maleko, baada ya Millya mwenyewe kuchelewa
  kufika.

  Inadaiwa kuwa lengo la Millya kuandaa maazimio hayo lilikuwa ni kuweka mazingira ya kumwondoa Gambo chamani kwa maslahi ya viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi ambao Gambo anadaiwa kuwashambulia mjini Dodoma katika kikao cha Baraza Kuu Taifa kwa kutoa kauli kuwa CCM inachukiwa na wananchi kwa sababu ya ufisadi.

  Habari zinadai kuwa katika kile ambacho wajumbe Baraza Kuu walishindwa kuamini macho na masikio yao ni hatua ya Mwenyekiti huyo kusoma maazimio hayo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huku mengi yaliyojadiliwa akiwa ameyaacha na mengine yakiwa hata hayakujadiliwa kikaoni.

  "Hapo ndipo wajumbe walipogundua kuwa maazimio hayo ya Millya yalikuwa yameandaliwa kabla ya kuanza kikao na hiyo ilikuwa kinyume na utaratibu wa uendeshaji mambo ndani ya CCM na kwa bahati mbaya wajumbe walishindwa kuhoji maazimio hayo yalitoka wapi kutokana na kuwa tayari usiku ulikuwa umeingia huku wengi wakiwa wanaanza kuondoka kurudi Arusha," alisema mmoja wa wajumbe wa mkutano huo.

  Hata hivyo, Millya alipoulizwa na gazeti hili alikanusha vikali kuwapo kwa maazimio mengine zaidi ya yale aliyoyasoma kwa waandishi wa habari baada ya mkutano huo na akaongeza kuwa binafsi hayatambui maazimio mengine yaliyotolewa.

  "Si kweli kuwa kuna maazimio mawili kama inavyodaiwa kuhusu kikao chetu cha Longido…maazimio yetu ni yale tu ambayo mimi Mwenyekiti niliyasoma hadharani na ndiyo yanayotambulika,"alisema Millya.

  Kuhusu madai kuwa amekuwa anatumia cheo chake cha Uenyekiti kuwasadia viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kupotosha maamuzi yanayotolewa na jumuiya yake, Mwenyekiti huyo alisema madai hayo ni ya uongo dhidi yake na hayana maana yoyote.

  "Nimefanya maamuzi mengi ndani ya UV-CCM bila ya kupata ushauri kutoka kwa Lowassa kama watu wanavyodai. Mimi ni msomi. Nina uwezo wa kufikiri vizuri yale ambayo ninadhani yana manufaa kwa Jumuiya ninayoiongoza na matunda ya maamuzi yangu mengi yanaonekana kwa macho tangu nilipoingia madarakani,"alieleza Millya.

  Aliongeza Millya: " Mzee Lowassa namheshimu kama kiongozi wangu wa ngazi ya juu ya chama. Lakini hawezi kuniingilia katika maamuzi ya ndani ya jumuiya yetu. Ila kama ana ushauri tunaupokea na kuufanyia kazi kama pia tunavyopokea ushauri kutoka kwa viongozi wengine.

  Na napenda kuwakumbusha Watanzania na wanachama wa jumuiya yetu kuwa hatukuwahi kutumika na wala hatutatumiwa na wanasiasa wenye maslahi yao binafsi ndani ya CCM yetu."

  Hata hivyo, pamoja na utetezi huo wa Mwenyekiti hali ndani ya UV-CCM hapa si shwari na wachunguzi wa mambo wanaeleza kuwa kujivua gamba kwa chama hicho kusiishie kwa viongozi wa ngazi juu bali hata wale wa ngazi za matawi, wilaya na mkoa ili kufufua uhai wa chama hicho kikongwe nchini ambacho kuna kila dalili kuwa siku za uhai wake zinaaanza kuhesabika.

  CHANZO: http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=3124.

  UJUMBE HUMU:

  Wana-CCM sasa waanza kumalizana kesh-uso-kutuna kwa magumi na mateke huku maelewano yao mengi yakiishia kituo cha polisi kuto mikoani.

  Kwa mtaji wa dhana mpya isiyofanyiwa Scientifi Research la Operation Vua Gamba, UVCCM kote nchini sasa chali; kila mmoja akiongea lwake tu. Mhe Wilsoni umeona lakini, huo ni mwanzo tu hata hivyo!!!
   
 20. Z

  ZenaTulivu Senior Member

  #20
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tusidanganyane, lengo la CCM kuvua gamba ni la kututema sie Waislamu tu.
   
Loading...