Mkakati wa CCM kuchelewesha katiba mpya huu hapa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati wa CCM kuchelewesha katiba mpya huu hapa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpemba mbishi, May 20, 2012.

 1. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Chama cha mapinduzi kimepanga mbinu tofauti kuhakikisha katiba mpya inayotarajiwa kutungwa na watanzania haitoweza kutumika wakati wa uchaguzi mkuu ujao (2015).

  Kwa mujibu wa wajumbe wa CCM (zanzibar) waliorudi tanzania bara hivi karibuni, wamenukuliwa wakisema kuwa mikakati hiyo ni ya aina mbili:

  1) KUISHINIKIZA TUME YA KATIBA KUINGIZA MAMBO AMBAYO YATAWAKERA WAZANZIBAR KUHUSU MUUNGANO JAMBO AMBALO LITAPELEKEA KUPIGA KURA YA KUIKATAA KATIBA MPYA WAKATI ITAKAPOITISHWA KURA YA MAONI. Katika kufanikisha hili tayari mapendekezo ya awali yapo mbioni kuwasilishwa tume ya katiba ili yaingizwe kwenye katiba. Moja ya pendekezo hilo ni KUWEPO KWA MFUMO WA MUUNGANO WA SERIKALI MBILI jambo ambalo linapingwa vikali na wazanzibar.

  2) Mkakati mwengine ni KUWATUMIA BAADHI YA WANASIASA AU VYAMA VYA SIASA KUWEKA PINGAMIZI MAHKAMANI ILI MUDA WA KUKAMILISHA MCHAKATO HUO USIFANIKIWE. Katika hili serikali na CCM imepanga kujitetea kuwa ilikuwa na nia njema lakini vyama vyenyewe vya upinzani ndio vilivyochelewesha mchakato huo.

  Pia wamedai watatumia mkakati mwengine iwapo mbinu hizo hazitofanikiwa. Hata hivyo mwandishi wa habari hii hakufanikiwa kupata mkakati wa tatu iwapo njia hizo hazitozaa matunda, lakini bado ninaendelea kutafuta kujua ni njia gani hiyo wanatarajia kuichukua.

  Kwa mujibu wa wajumbe hao kutoka zanzibar wamesema kuwa wana ccm wenzao kutoka bara sasa hivi hofu yao ni chadema, hivyo basi iwapo katika mpya itatumika katika uchaguzi mkuu ujao (2015) inaweza kuhatarisha wao kubaki madarakani kwa vile tume huru ya uchaguzi itakuwa ni pigo kubwa kwa ccm.

  Mmoja ya wajumbe hao Alipoulizwa iwapo ni mkakati gani ambao anategemea kuwa utafanikiwa alidai kuwa ni ule mkakati wa kwanza wa kuweka vipengele na vizuizi ambavyo vitawafanya wazanzibar kuichukia katiba mpya na kupelekea kuikataa wakati wa kura ya maoni jambo ambalo litakuwa ni pigo kwa chadema ambacho kimepanga kutumia tume huru ya uchaguzi kujikita madarakani.

  Habari hizi huenda zikawa na ukweli fulani kwa vile uvumi umeenea hapa zanzibar kuwa kama HAKITOWEKWA KIPENGELE CHA KUJADILIWA MUUNGANO (KUWEPO AU KUTOKUWEPO) basi wazanzibar watahamasishwa kupiga kura ya hapana wakati ukifika jambo ambalo litafanikiwa kwa kura nyingi.

  (WAKATI NDIO AMBAO UTATHIBITISHA UKWELI AU UONGO WA TETESI HIZI.)

  TUJADILI NA NINI KIFANYIKE KUZUIA MBINU HIZI CHAFU.
   
 2. S

  STIDE JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana nawe, ccm wanambinu za kipumbavu!! Nawaonya ccm wasituchezee akili!! Hawawezi zuia mvua kunyesha!!!
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  hii habari ina-make sense
   
 4. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Wanatafuta balaa eti?hatuta kubali kirahisi patachimbika hapa.
   
 5. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1. Nafikiri kuwa chadema tumewaamini ccm kuwa wanaweza kuleta katiba mpya ya Watanzania, kitu ambacho siyo cha kweli kwa sababu hoja ya katiba mpya siyo sera ya ccm, hivyo watafanya wawezavyo kupindisha mchakato ili waendelee kubaki madarakani...
  2. kuna haja ya kutumia njia mbadala....kufanya marekebisho ya katiba ili kuruhusu uanzishwaji wa tume huru ya uchaguzi kabla ya katiba mpya....
  3. Kushinikiza serikali kuanzisha mchakato wa kura ya maoni juu ya muungano, muundo wake na uwepo wake...
  4. Kuishinikiza serikali kuweka wazi juu ya msimamo wake kuhusu mahakama ya kadhi......

  Nafikiri kwa haya machache tunaweza kupiga hatua....lakini kuitegemea tume ya Kikwete juu ya katiba mpya kuwa italeta hiyo katiba, ni kupoteza muda na mwisho wa siku...uchaguzi ujao tusishangae tukafanya yaliyotokea Kenya na pengine hata zaidi.....believe me or not...!!!!!
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka zamani komba wa TOT alivyokuwa na mvuto kwenye kampeni na bendi yake lakini sasa anaonekana ni taktaka machoni kwa watanzania kwahiyo hata wakichelewesha lazima kieleweke
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Kwenye swala la kupiga kura wapiga kura wote wa Zanzibar ni sawa na wapiga kura wa jimbo moja tu la Ubungo. kwahiyo Wazanzibar hawana ubavu wowote kwenye kura ya maoni.
   
 8. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kasome tena sheria na kanuni. Wazanzibari hata wawe laki moja, ujue kwamba wana kura ya Veto. Usikurupuke. Asiyejua maana usimwambie maana.
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Unaweza kusupport kauli yako kwa kuweka link ya hiyo kura yao ya Veto? maana wewe ndio umekurupuka na mapovu kibao mdomoni.
   
 10. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mkuu Matola nilishasema kwamba 'asiyejua maana usimwambie maana'
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Then hapa unahitaji nini hasa!!.....Facebook is safe place for you.
   
 12. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  kumbe wanaogopa katiba mpya?
   
 13. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Kama wanaogopa katiba basi ccm byebye.maana mikakati yao hakuna hata moja litafanikiwe time has come at its right sight
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Wajumbe wa kamati ni kikwazo tosha, tusitegemee kuvuka Katiba nzuri kwenye ile mkusanyiko unaoitwa tume. Pale ni maslahi ya chama twawala tu, hakuna cha zaidi.
   
 15. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa I belive you.
   
 16. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi nina mashaka na hii tume teule ya Jk kuwa watafanya kwa maslai ya mkuu wa kaya anayejitahidi kuwapa donge nono kama rushwa ili wafanye kwa maslai yao ccm. Niliona thread iliyozungumzia laki tatu kwa siku kwa hii tume ya katiba na je ni halali?
   
 17. c

  cray Senior Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 172
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nachoweza kusema nikwamba nguvu ya umma hata upepo hauwezi kuizuia, watabana lakini wataachia tu. So tusubiri muda tu. Wafanye wanavyoaka lakini jibu ni CDM kushika Nchi hii mnamo uchaguzi ujao.
   
 18. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kama tunaitakia nchi hii mema tuachane na uhaini na hila.
   
 19. n

  nyalubanja Member

  #19
  May 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kumwambia jamaa yangu kuwa ilikuepushavita kwa tuanze na tume ya uchaguzi.ili tukipata rais safi ndiyotuundekatiba mpya kamasihivyo jiandaenikwavita maana ccm hawakotayari kuundakatiba mpya.
   
 20. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Inauma eeehh. Asiyejua maana usimwambie maana.
   
Loading...