Mkakati mbovu wa kutawala na kampeni babaishi kumgharimu JK Uraisi hivi punde....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati mbovu wa kutawala na kampeni babaishi kumgharimu JK Uraisi hivi punde.......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 23, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Jk alifikiri ya kuwa watanzania watamchagua kwa sababu ya ahadi za miaka mitano ijayo......Hilo lilikuwa ni kosa lake la kwanza...........Watanzania walitaka tathmini ya miaka mitano iliyopita ambayo Jk hakuwapa...........sasa bila kujua CCM na JK wake walikwama wapi ni vigumu kwa wapigakura kuendelea kuwaamini na ahadi zao lukuki ambao utekelezaji wake umethibitika ni wa kusuasua.

  Wapigakura walitaka kujua mikakati ya JK kupambana na ufisadi ambao ndicho kiini kikubwa cha umasikini wetu na huduma za umma kudorora lakini JK hakutaka kushibisha shauku za wapigakura kwenye maeneo haya!!!!!!!!!!!

  JK alifikiria uongozi ni kufanya utakavyo lakini hivi karibuni atajifunza ya kuwa uongozi ni kufanya yale ambayo wapigakura wanataka na ukija na ajenda zako za siri na wapigakura wakizijua basi umekwisha watakukataa...

  La kushangaza zaidi ni kwa nini Jk hakutaka kutumia muda mwingi kuzungumzia mafanikio ya serikali yake kwa miaka mitano iliyopita? Ungelitegemea ya kuwa kama kazi tuliwatuma waliifanya vizuri basi wangelikuwa na mengi ya kujigamba lakini Jk aonekana kama ndiyo anaomba kwa mara ya kwanza ridhaa ya kuongoza nchi...wakati siyo kweli .......Hili litamgharimu sana

  Kiongozi uliyeko madarakani kwa miaka mitano hupaswi kuwa unatoa ahadi ila unapaswa kuwakumbusha wapigakura kile ulichokifanya na kukaa kimya juu ya kile alichokifanya wapigakura watafikiria ya kuwa JK na CCM pengine hakuna walilolifanya na kuwaadhibu kwa kura zao.........Haitoshi kwa JK kung'aka ya kuwa kuna mengi tuliyoyafanya....wapigakura watauliza ni yepi mkuu siku ya kupiga kura.....na hicho kitakuwa ni kilio na kusaga meno kwake JK na CCM yake........Hivi sasa tunaita CCM ni mali ya JK kwa sababu hakutaka kuimilikisha kwa wananchama wa CCM au hata viongozi wake pale aliposema suala la Uraisi ni la kifamilia..........na ndiyo maana kwenye kampeni zake ni yeye, mkewe na wanawe ndiyo wanahangaika kutafuta kazi ya umma...na wapigakura wanajiuliza hivi hawa wanafamilia ya JK wakikipata hiki kibarua tena watamhudumia nani kama siyo kujihudumia wenyewe?

  Eneo ambalo Jk alitakiwa atumie muda mwingi kuwahabarisha wapigakura lilikuwa ni matatizo ya kiuchumi lakini yeye ametumia muda wake mwingi kuvijenga vyama vya upinzani kwa kuviita "photocopy" na vya muda tu. Wapigakura wanaujua uwezo wa vyama vya upinzani hivyo hawakuhitaji JK kuwafundisha somo hilo....

  Jk hakuzungumzia matatizo ya kiuchumi na kuwaacha wapigakura kuamini ya kuwa yupo mbali nao na hivyo haguswi na adha kadha wa kadha zinazowakabili na mshahara wake ni kumfuta kazi J2 ijayo.......Kwa lugha ya kimombo husema: "JK is out of touch, insulated and out of reach to commoners......."

  Jk baada ya kufilisika kisiasa akaanza kushutumu vyombo vya habari, viongozi wa dini na baadhi ya waumini wa madhehebu zisizokuwa zake ya kuwa wanamchukia kwa sababu ya imani yake ya kidini akisahau ya kuwa miaka mitano tu iliyopita watu hao hao anaowakosea adabu leo ndiyo wengi wao waliompa hiyo dhamana ya kuliongoza taifa hili.

  Shukrani ya JK sasa ni kuwaita wadini kwa minajili ya kuficha udhaifu wake wa kuwa kiongozi mdhaifu....Kwa hali hii, Jk amewanyima wapigakura mwanya wa kumsaidia kumrekebisha na hivyo kuwahamasisha kumfukuza kazi kiongozi huyu dhaifu mwenye malalamiko na visingizio visivyokuwa na mwisho......

  Badala ya Jk kuhubiri udini na ukabila mambo ambayo bado hayajaota mizizi hapa nchini angeliwauliza watanzania kwa unyenyekevu sana hivi ni wapi nimekosea?

  Hapo wapigakura wangemwona kumbe ana nia ya kujirekebisha lakini mkakati wake wa kuwalaumu wapigakura kwa kubuni bila ushahidi wowote kuwa changamoto zinazotukabili ni udini na ukabila yaelekea JK hata hajui nchi hii inatoka wapi, iko wapi na inaeleka wapi...na kiongozi wa jinsi hii, namna ya kumuenzi ni kumstaafisha kwa nguvu za kura zetu siku ya J2 ijayo............hatuna namna nyingine ila hiyo.......


  Uongozi shupavu ni kujipima, kuuliza na kushirikisha wenzio na wala siyo kuwaonyesha ubaguzi, ulafi wa madaraka na ubinafsi hata kubinafsisha ofisi ya umma kuwa sasa ni miliki ya familia yako JK...........Lakini nina habari njema kwa JK ya kuwa baada ya kura kupigwa huo mzigo hautakuwa "headache" yake tena kwani wapigakura watamkabidhi raia mwingine ambaye safari hii anafahamu fika kuwa uongozi wa umma ni shirikishi na wala siyo suala la kifamilia..

  BYE-BYE JK..........BUT........ WELCOME DR. SLAA AND CHADEMA.........................


   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,603
  Likes Received: 4,708
  Trophy Points: 280
  JK na jeshi lako la majini yaliyokuwa yanakulinda hapo magogoni fungasheni virago.
   
 3. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  Hongera kwa kufikisha post 1000+ kwa kipindi kifupi keep it up................
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Oct 23, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli katika mwezi mmoja tu jamaa kafikisha post elfu moja zilizonichukua mimi zaidi ya mwaka mmja na nusu. Hongera sana ndugu Rutashubanyuma.

  Kwa upande mweingine, ndugu huyu Rutashubanyuma (nadhani ana maana ya asiyerudi nyuma) huwa anatoa post nzuri sana kuliko wengi wetu ingawa zinaweza kuwa zinawaudhi rafiki zangu wa upande ule.
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Kichuguu,

  Mkuu mimi imenichukua miaka miwili kufikisha post 1000.Ni kweli Ruta anatoa mabandiko yenye akili sana.   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  RUTA umeiandika vizuri sana hii....JK is out of touch kama unavosema....hakuna mtu pale ni blah blah tu..Si umemsikia mpaka Kinana anasema ahadi nyingine ni za kwake binafsi sio za chama
   
 7. d

  dotto JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jk kwa heri na asante kwa kutotutendea haki kwa miaka mitano tuliyokuajiri.


  Karibu Dr.Slaa Ikulu kwa ajira ya miaka mitano. Fanya mambo mkuu!
   
 8. Tai Ngwilizi

  Tai Ngwilizi JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2010
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Jk hawezi kuongelea mafanikio kwa sababu mafanikio ni zero au hayawahusu waliosimama mbele yake kumsikiliza
  Jk hawezi kuongelea ufisadi kwa sababu mafisadi wakuu wanapeta hata baada ya kujiuzulu kwa kutajwa wazi na ushahidi mbele ya bunge
  Jk hajaijua hii nchi, alidhani umaskini wa watanzania ume ingia hadi kwenye akili na macho yao, alidhani watanzania umaskini hauwamizi wala hawauoni wameuzoea na wana enjoy kukaa kwenye vile vibanda vya kuku wa kienyeji huku wakijitafutia wenyewe huduma za jamii kama wapo kwenye zama za kale za mawe -

  • kuzalisha mabinti zao nyumbani,
  • kuoga kunywa maji mtoni,
  • kutibiwa kwa mganga wa kienyeji na
  • kuparua parua upenuni na jembe la mkono ili wapate chakula ...
  yeye tu na wengine waliowiva kwa kukaa ndani ya magari na ofisi zenye viyoyozi ndio wana stahili kupata raha.
  Nasubiria tarehe 31 mimi!!
   
 9. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mwaka 2005 JK na mbunge wa jimbo la Mafia Abdulkarim Ismail Shaha waliahidi maji safi na salama kwa wakaz wa Mafia.Walewale walioahid miaka mi5 iliyopita bila kutelekeza ndio haohao wanaoahid leo mambo yale yale.
  Mafia 2005.Aliahid kujenga tuta kubwa kwa ajili yakutenganisha vijiji vya Jimbo na Banja ktk tarafa ya Kaskazin.Sasa amerudi na ahad hiyo akidai kiac cha Sh. 200 million kilitolewa lakin zilizotumika ni Sh. 20 million tu kwamba nyingine 'zimeliwa na wajanja.' Ni akina nan? Wamefanywa nin? Hakusema
   
 10. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapo penye red ni noma. Anakaa na wezi?
   
 11. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  duh hii imetulia!
   
 12. m

  matawi JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Jamani tusije tukajisahau kutunga nyimbo za kumwapisha Dr Slaa , mtafuteni Komba mahali alipo aanze kuandaa single mbili, tatu. Itakuwa ni siku kubwa sana maana huu ndiyo ukombozi wa Mtanzania kikwelikweli
   
Loading...