Mkakati kuvuruga uagizaji mafuta waandaliwa; Mbunge wa CCM ashiriki mchezo mchafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati kuvuruga uagizaji mafuta waandaliwa; Mbunge wa CCM ashiriki mchezo mchafu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]IJUMAA, AGOSTI 17, 2012 07:30 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

  *Makampuni matatu makubwa yahusishwa
  *Mbunge wa CCM ashiriki mchezo mchafu

  MPANGO wa Serikali wa kudhibiti bei ya mafuta kupitia utaratibu wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (bulk procurement) upo hatarini.

  Hatua hiyo inatokana na makampuni makubwa matatu yanayojishughulisha na biashara ya mafuta nchini kuandaa mkakati wa kuvuruga mpango huo wa Serikali.

  Kampuni zinazodaiwa kuendesha mkakati huo ni Puma Enegy, Oraxy Enegy na Gapco ambazo zinataka kuubadili mfumo huo ziweze kudhibiti soko la mafuta nchini.

  Taarifa za ndani kutoka kwa wadau wa mafuta zimeweka wazi kuhusu mkakati huo na kuitaka Serikali kuwa makini na kampuni hizo kulinda bei ya mlaji.

  Kampuni hizo zinadaiwa kuendesha mkakati wa siri unaolenga kumng’oa Mwenyekiti wa Bodi ya Petroleum Importation Coordinator (PIC) ambayo inasimamia zabuni za mafuta.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Mwenyekiti wa bodi hiyo ambaye ni Mbunge wa Kwimba, Mansoor Shanif Hiran, anaonekana kikwazo kwa makampuni hayo.

  Mkakati mwingine unaofanywa ni kutaka kubadili mwongozo uliounda utaratibu huo wa kuagiza mafuta kwa pamoja kuzifanya kampuni hizo ziwe na nguvu kinyume na sasa.

  Bodi hiyo inayosimamia zabuni ya uagizaji wa mafuta kwa pamoja unaundwa kwa mujibu wa sheria na kuzihusisha kampuni za Puma, Orxy, MGS, Moil, Camel Oil na Gapco.

  Kwa mujibu wa muundo ulioandaliwa na Serikali bodi ya zabuni (PIC) inaundwa na makampuni sita ya mafuta. Kampuni mbili kati ya hizo zina zaidi ya asilimia 10 ya soko lote la mafuta nchini.

  Kampuni hizo mbili ni Puma Enegy na Orxy, wakati kampuni kampuni za kati ni MGS, Camel Oil na Gapco na kampuni ya Moil, ambayo ina mtaji chini ya asilimia 5, ambayo kisheria ndiyo inayotoa mwenyekiti.

  Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage (CCM) anadaiwa kuratibu mkakati huo kutokana na kuwa na uhusiano na kampuni ya mafuta ya Puma.

  Mwenyekiti wa bodi hiyo zabuni ambaye pia ni Mbunge wa Kwimba, Mansoor Shanif Hiran (CCM) anawakilisha wafanyabiashara wadogo wa mafuta akipitia Kampuni ya Moil.

  Makampuni hayo matatu yanadaiwa kutaka kuzinyang’anya kazi ya kuagiza mafuta kampuni ndogo zinazoshinda katika tenda, jambo ambalo limekuwa likipingwa na mwenyekiti wa bodi.

  Makampuni hayo yamekuwa yakiipiga vita kampuni ya Agusta Enegy ambayo imeshinda zabuni kwa vipindi vitatu mfululizo kwa kuwa waagizaji wa bei ya chini.

  MTANZANIA imebaini kutokana na hali hiyo kampuni hizo kubwa zimekuwa zikifanya mawasiliano na baadhi ya wasambazaji na kufanya uchakachuaji mafuta kwa lengo la kutaka kuiondoa sokoni kampuni Agusta Enegy.

  Hata hivyo, utaratibu ambao umekuwa ukielezwa na EWURA, unaeleza kuwa baada ya mafuta hayo kuingizwa nchini watalaamu wa maabara kutoka EWURA na TBS hufanya ukaguzi kabla ya mafuta kuingizwa katika depoti za wafanyabiashara.

  “Meli inapoweka nanga bandarini, kabla mafuta hayajashushwa, wakaguzi kutoka TBS na EWURA wanakuja kupima mafuta.

  “Wakijiridhisha kuwa mafuta ni mazuri wanatoa cheti cha kuruhusu mafuta yashushwe, wakibaini mafuta ni machafu wanazuia, huu ndiyo utaratibu.

  “Sasa makampuni haya yanafanya mchezo mchafu, mafuta yakipelekwa katika depoti wanayachakachua yakifika kwa walaji wanalalamika EWURA ili kampuni iliyoagiza mafuta ionekane haifai inaleta mafuta machafu, hizi ni hila,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

  “Kampuni ya Agusta Energy mara zote imekuwa ikishinda zabuni kutokana na bei yake kuwa ndogo wakati wao wanataka bei ya mafuta iwe kubwa.

  “Sasa kumekuwa na hali ya mizengwe dhidi ya kampuni hii hasa kutokana na hizi kampuni kubwa kuona kuwa zinakosa maslahi.

  “Wanataka kumtoa mwenyekiti wa bodi na kampuni ya Agusta waitoe sokoni ili makampuni haya yashike hatamu wapeane zamu ya kuagiza mafuta.”

  Naye Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage (CCM) anayetuhumiwa kuongoza mkakati huo, alisema yeye hahusiki na jambo lolote linalohusu PIC.

  “Nataka nikwambie kuwa sekta ya mafuta nchini kwetu imeingiliwa na ina matatizo sana na katika hili hata jana nilikuwa na Mwenyekiti wa PIC, Mansoor nilimueleza hili kwa kina.

  “Fitna na majungu kila kukicha mwongozo huandaliwa na EWURA na si PIC. Siku zote nasema muundo wa chombo hiki ni sawa na NGO’s ya watu fulani.

  “Hao wanaosema mimi naingilia mambo ya PIC hata kidogo sina maslahi nayo zaidi ya kushauri sekta nzima ya mafuta hasa kupitia Bunge letu tukufu,” alisema Mwijage.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kila Mahali kwenye pesa; Mbunge wa CCM macho hayooo... kuvuruga Ufanisi na Kuiba...
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  tushawazoea...hakuna linalotushtusha
   
 4. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Huyu Mwijage kwenye kila dili chafu ya mafuta yupo tu!
  Hata kwenye hili la kutaka kuwapiga zengwe waziri wa nishati na katibu mkuu wake yumo! Siku zake zinahesabika bungeni.
   
 5. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Nilisoma na Huyu Bwana mwijage Manchester university , amespecialize kwenye oil and gas management anatumia taaluma yake kuiba sasa,
   
 6. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,847
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Huu ni uwongo mtupu!! Kampuni hiyo ya agusta imeshinda zabuni zote kutokana na kubebwa!! Washindani wake hutolewa kwa sababu ambazo hazina msingi!! Mara hajaweka lakiri mara hili au lile!! Hii kampuni ya agusta nadhan ndio inajitahidi kutugilibu akili!! Hii kampuni wanasema imetoka uswiss ila inamilikiwa na watanzania kwa njia hiyo hiyo ya kampuni za kutafuna nchi!! Lets be careful hawa puma na wengine wametolewa kwa njia ile ile ya "maswi na tanesco kwa mafuta mazito, quotation 1460 kwa lita malipo 1860!!"
   
 7. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,847
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Naomba Mwenye Taarifa za Bidders Comparison Quotation ya suppliers ambao wamefanya ushindani kwenye Bulk supply Uone hao wengine walivyokuwa Cheap na kutolewa kwa sababu ambazo hazina Msingi!! Please Mwenye Hizo Data Aziweka Hapa!! we are not fools any More!! Nikizipata nitaziweka!! Nadhan ni Agusta wanataka kutugilibu hapa!!
   
 8. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,956
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Bila kuchukua hatua kali dhidi ya wahujumu uchumi haya mambo yayawezi kukoma. It is just too bad, mtu anaweka masalahi yake mbele bila kujali athari kwa taifa zima. Imefika wakati wakutoa fundisho japo kwa kutoa wachache kuwa mfano.
   
 9. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Hawa wasukuma wa kwimba na mbunge wao muhindi wananichanganya kweli. Halafu huyu mwenyekiti wa bodi iweje nae awe na kampuni ya mafuta? yaani hii nchi hii! tunategemea only good faith kumuokoa mlaji, kwanini? too tired!
   
 10. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Sijui ni kwanini huwa siamini sana. Wabunge wengi wa ccm ni wezi tu, ndio maana waligombea ubunge kwa nguvu kubwa za pesa ili waje waibe kila kitu kitakachokatiza mbele yao.
   
 11. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,315
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Tuliambiwa PUMA Energy inamilikiwa kwa 50% na serikali, iweje tena wapange kumhujumu mmiliki wao!
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kwa Tanzania hii lolote linawezekana maana ndani ya serikali wote ni vigeugeu na wanafiki watupu wanazungukana kuharibiana tu fitna na unafiki kwenda mbele
   
 13. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Dhana waliyonayo wabunge wengi wa ccm ni kuchuma na sio kusaidia maendeleo ya nchi. we jiulize, hivi ni kwa nini kila inapotokea wabunge wa upinzani wakatoa hoja za kusaidia nchi, ccm huwa wanawabeza??? nilichokigundua ni kwamba, kwa mbunge wa CCM, muhimu ni kula na kulinda chama, wananchi watajijua wenyewe, halafu ukiwa jukwaaani jifanye unapenda kuwatumikia wananchi. wanakera sana, ILA WATANZANIA TUJIPANGENI TUIONDOE CCM MADARAKANI, HAWA WATU SIO WALE WA ENZI ZA NYERERE TENA, HAWA WA SASA NI CHAMA CHA MAJAMBAZI NA MAFISADI HUMOHUMO.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,378
  Trophy Points: 280
  ...Haya yote ni matokeo ya Serikali iliyoshindwa katika utendaji wake na ambayo haistahili kabisa kuendelea kuwepo madarakani.
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  C CM na wabunge/viongozi wake oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

  Chukua Chako Mapema juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
   
Loading...