Mkakati gani thabiti kuwakomboa vijana wasio na ajira? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati gani thabiti kuwakomboa vijana wasio na ajira?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KANJARA, Jan 12, 2012.

 1. K

  KANJARA Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vijana mnaowategemea wanasiasa kufikiri kwa ajiri yenu mnawakati mgumu. Serikali tayari imewatenga wako tayari kuwatumia wakati wa uchaguzi ukiisha vinakuja visingizio kuwa vijana wanapenda utajiri wa haraka, hawajitumi ,hawana uzoefu na wanakurupuka. Nimekuwa nikifatilia mitizamo mbalimbali ya baadhi ya vijanma wanaopata fursa ya kutoa maoni yao kuhuisu changamoto zavijana. Wengi wao fikra zao hazina utofauti na za watawala wao lakini si shangai kwani hata kupata fursa ya kutoa maoni kwenye baadhi ya vyombo vya habari ni mchakachuo mtupu. Wahitimu na vijana wote unganeni kuuliza vipi mfuklo maalumu wa wahitimu kwenye kilimo kwanza kwa wale wanaotaka kujiajiri? au pesa hizo ziliwekwa wapi au ilikuwa porojo ya kuwaadaa na kuwapumbaza wananchi? Kuhusu swala la uzoefu kwa kijana aliyetoka masomoni uzoefu ataupata wapi? Na je ni nani wa kulaumiwa kwa sera mbovu zinazozalisha wasomi wasio0na uzoefu? Je, ni kwanini mfumo wa elimu unaolalamikiwa kila siku habadilishwi?
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  MKUU SWALA LA KUJIAJIRI AU KUAJIRIWA HAPA TANZANIA LINA HISTORIA NDEFU SANA, HAPA KUNA MAMBO MENGI SANA.

  1. TATIZO LA KUAJIRIWA HAPA TANZANIA.
  tatizo la ajira hapa tanzania lina mlolongo mkubwa sana na lina sababishwa na vitu mbalimbali. MFANO

  a. UCHUMI WA TAIFA LETU

  Uchumi wa Tanzania kwa sasa ni mbaya sana na kama unavyo jua nchi yetu ni masikini sana ingawa tuna rasilimali za kutosha. Tumeshindwa kujenga uchumi imara ambao utavutia investors wakubwa wa ndani na nje walete mitaji yao ili ajira zipatikane kwa wingi.

  2. TRIENDS YA UWEKEZAJI TANZANIA

  kama ukifuatilia uwekezaji wa tanzania umejikita katika secta ya utalii kwa wingi sana, secta ya habari, madini kwa wingi sana, kilimo, na viwanda kwa uchache
  TATIZO LA AJIRA TANZANIA LINGEWEZA KUPUNGUZWA NA UWEKEZAJI KATIKA VIWANDA NA SI KATIKA CHOCHOTE KILE
  Vi wanda ndo suluhisho pekee la ajira Tanzania, Na Wawekezaji wengi hawawekezi kwenye viwanda, wanawekeza kwenye utalii ambao un ajiri watu wachache sana,
  - Nchi nyingi sana duniani hupunguza tatizo la ajira kupitia viwanda,
  - Mfano kiwanda kama cha A to Z arusha kimeajiri watu zaidi ya 4000, pamoja na kwamba masilai si mazuri ila inasaidia sana hebu fikilia tungekuwa na viwanda aina ya A to Z kama 10,000 hapa tanzania ingekuwaje?

  3. KUFA KWA VIWANDA VILIVYO KUWEPO

  Viwanda vyote vimekufa na yamebaki magofu baada ya hata mashine kuchuliwa na kwenda kuuzwa kama chuma chakavu
  Hivi viwanda kama vyote vingekuwa hai vingeweza kutupunguzi tatizo kwa kiasi fulani

  4. MABADILIKO YA SAYANSI DUNIANI

  Kwa sasa Computa zinachukua nafasi ya binadamu, chukulia mfano benk zamani na sasa, zamani benki moja ilikuwa na si chini ya wafanyakazi 20 ila kwa sasa benk moja inawafanyakazi 8 hadi 10
  makampuni mengi sana yanatumia komputa badala ya binadamu ili kupunguza cost na kuongeza ufanisi, chukulia mfano kwa sasa TBL walikuwa na mpango wa kufungu ROBOT ZA KUPANGA CRETI ZA BIA, HAPO UNATEGEMEA NINI?

  5. USHINDANI WA BIASHARA

  Ushindani huu unapelekea makampuni mengi kupunguza ghalama za uendeshi ili kuweza kupambana, na wanapunguza kupitia kuajiri wafanya kazi wa chache sana

  6. MFUMO WETU WA KIJAMAA

  Tulizoea kila kitu ni serikali, ajira serikali, biashara serikali, huu mfumo wa kinjamaa ungali upo vichwani mwetu, hatutaki kubadilika.

  7. WAZAZI WETU

  Wazazi wetu nao wanachangia sana walitulea vibaya sana, tulizoeshwa kila kitu, tuliambiwa kwamba tunasoma ili tuje kupata kazi nzuri, tunasoma tuje kuwa mameneja, tunasoma ili tuje kufanya kazi TRA, BANDARINI, NSSF, BENKI NA KAZALIKA

  TUMEKUWA TUKIAMINI TUKO SHULENI AU VYUONI ILI TUJE KUPATA KAZI NZURI SANA, HILI NI KOSA KUBWA SANA LA KUWALALUMU WAZAZI WETU, LEO HII KIJANA YUKO MTAANI AMEMALIZA CHUO ANASUBILI AJIRA, DEGREE YAKE HAOWEZI HATA MSAIDIA KUANZISHA BUSTANI YA MBOGA

  KWA KIFUPI KUNA MASWALA MENGI SANA YANAFANYA AJIRA ZIWE NGUMU, NA ZINAKUWA NGUMU KUTOKANA NA WAHITIMU WOTE KWENDA KUBANANA KWENYE KUAJIRIWA.


  KATIKA SWALA LA KUJIAJIRI HAPA KUNA UNAFIKI WA HALI YA JUU MNO, NA HAPA MIMI SI ILAUMU SERIKALI HATA KIDOGO.

  1. Hivi serikali ndo inajukumu la kutuanzishia biashara?

  2. Ni wangapi tuna culture ya kujiajiri tangia mwanzo?

  3. Ni wangapi wamemaliza chuo na kujairibu hata kuanzisha bustani? utazungumziaje kupewa mikopo ya kilimo wakati unaona aibu kuanzisha bustani eti utachekwa na ngudu, jamaa, rafiki, mchumba na kazalika?

  TUNA ILAUMU SERIKALI LAKINI SISI WENYEWE NDO TATIZO KATIKA KUJIAJIRI.

  1. MFUMO WA KIJAMAA TENA HAPA NI TATIZO

  Ndo kama hivyo tunasubiria serikali ituanzishie biashara, ituambie sasa vijana fanyeni biashara

  2. WAZAZI WETU

  walitufundisha kwamba tunasoma ili tuajiriwe na tumejijengea hivyo, hadi leo hii wanafunzi wa shule za misingi ukiwauliza wazazi wao huwa wana washauri nini kuhusu elimu utasikia haya. TUNAAMBIWA TUSOME ILI TUJE KUWA MAMENEJA, TUJE KUWA MARUBANI, TUJE KUAPATA KAZI NZURI
  Hakuna hata mazazi mmoja anaye mwambia kijana wake asome aje kuwa mjasirimali mzuri, Wale watoto tiyali wameisha haribiwa, wao wako shuleni ili waje kuajiriwa na si vinginevyo

  3. WALIMU WETU NAO WANACHANGIA SANA

  Hawa nao story wanazo wapatia wanafunzi shuleni ni kama za wazazi tu, SOMENI SANA MJE KUWA MAMENEJA

  4. EXTENDED FAMILLY

  Huu mfumo wa extended familly kwa huku kwetu naona nao ni kikwazo sana, tena sana
  LEO HII KIJANA ANAMALIZA CHUO/SHULE NA KAZALIKA ANAKAA KWA DAD, KWA SHENEJI, KWA MJOMBA, KWA SHANGAZI, KWA BIBI, KWA BABU, KWA MDOGO WAKE NA SHEMEJI, KWA BINAMU, KWA BABA WA UBATIZO, KWA MAMA WA UBATIZO.

  Leo hii huyi kijana ukimwambia jiajiri hawezi kukuelewa wakati huko kwa ndugu zake anaishi kwa raha sana ANAPEWA HELA YA VOCHA, AMENUNULIWA SIMU KARI SANA, ANAKULA VIZURI SANA MILO MINNE KWA SIKU, HIVI HUYI KIJANA UKIMWAMBIA TUKASHIKE POLI TUANZE UJASIRIAMLI ATAKUELEWA? ANASHIDA GANI?

  Ndugu wanachangia sana kufanya vijana wasiwe na ari ya kujijiri kwa sababau wanakuwa wanawatoa fedha, sheneji atampa, mjomba atampa na mama atampa,
  HUYU KIJANA HAWEZI KUWA NA MAWAZO YA KUJIAJIRI HATA SIKU MOJA.

  4. VIJANA WENGI KUAMNI KWAMBA NYUMBANI KUNA MALI ZA KUTOSHA

  Kama kijana anaamuka na anaona home kuna magari, kuna nyumba za kutosha kuna fedha za kutosha ya nini akajiangaishe na biashara? si bora akae nyumbani? Je anaweza anisha biashara ya Baba lishe?
  Hapa husubiri wazazi wafe ili wahike usukani

  5. UNAFIKI WA GRADUATE.

  Haya mambo ya kujiajiri huwa yanazungumzwa na graduate wakisha ingia mtaani na kuona mambo yote yamefeli ndo huanza kukurupuka.

  VYUONI HAKUNA UNDERGRADUATE WANAO PIGA STORY ZA KUJIAJIRI, PALE WATU WANAPEANA MATUMAINI YALIYO PITILIZA, WANAWAZA JINSI WATAKAVYO AJILIWA TRA, NSSF, BANDALINI, BENKI NA KAZALIKA

  Na ushajiuriza ni kwa nini wanawake/wnaume wengi sana wanapapatikia Undergaduates? au Graduate? Wanafahamu huyu akimaliza chuo tu atakuwa na kazi nzuri sana, atakuwa meneja, so kila mwanamke/mwanaume anataka awe na mchumba alie chuo kikuu kwa matumaini kwamba maisha kwake yatakuwa mteremko.

  HUYU KIJANA ALIOKO CHUONI NA ANAE MPA MATUMAINI MCHUMBA WAKE KWAMBA NIKIMALIZA CHUO TU NA NASA KAZI, HAWEZI MALIZA CHUO HALAFU AKAANZISHA BUSTANI YA MBOGA, MCHUMBA ATAMZARAU SANA NA MCHUMBA TANGIA MWANZO ALISHA JUA MCHUMBA WAKE AKIMALIZA CHUO ATAKUWA MENEJA, LEO HII AMUONE ANA KIBANDA CHA KUUZIA VOCHA,

  NATOA MFANO HAI.
  NIKIWA CHUONI, TULIVYO KUWA TUNAKARIBIA KUMALIZA CHUO, TULIKUWA TUSHA SOMA ALAMA ZA NYAKATI KWAMBA MTAANI SI SALAMA, NA TULIANZA MIKAKATI IFUATAYO.

  Tuliamua kutafuta tasisi za serikali zinazojihusisha na maswara ya biashara ili zije zituelimishe maswala mbalambali yahusuyo kujiajiri, tuliita
  -TRA
  - BRELA
  - TIC
  - SIDO
  - NA BAADHI YA BENKI
  WAKUU TULIBEZWA SANA, UNDERGRADUATE WENZETU WA KOZI ZINGINE TULIKUWA TUKIWAALIKA NA WALIVYO KUWA WAKIINGIA UKUMBINI KWELI WALIKUWA WAKISILIKIZA KWA UMAKINI SANA, ILA KWENYE KUULIZA MASWALI SASA, WAKATI WENGINE TUKIULIZA WATUPE MAUJANJA YA KUJIAJIRI WENZETU WALIKUWA WANAULIZA MASWALI KAMA WANAWEZA PATA CHANSI ZA KUAJIRIWA KWENYE HAYO MASHIRIKA
  Wakuu nazani mmepata picha, Undergraduate wengi sana wakiwa vyuoni wanawaza kuajiriwa wala hakuna wano panga mikakati ya kujiajiri. Ila wazo la kujijiri huja baada ya mtaani kuwa kugumu,

  7. MAWAZO POTOFU/ NAITA NI UJINGA

  Eti graduate ailiyesomea kilimo, hawezi anzisha hata busatni, eti atakuwa najiaibisha,
  Geaduate aliye somea mapishi hawezi anzisha biashara ya Mama lishe/ Baba lishe, kisa aibu, atachekwa na jamaa zake pamoja na mchumba wake
  KWA STAILI HII AJIRA ZITAENDELEA KUWA NGUMU, TUTABAKIA KUSEMA TUNAMAWAZO YA BAISHARA ILA TUMEKOSA MITAJI

  7. OVER EXPECTATIONS
  hii inatusumbua sana, na ni moja ya sababu ya graduate kushindwa kujijiri

  SO TUACHE KULAUMU SERIKALI WAKATI C C HATUJAONYESHA NJIA.

  1, Je tumeonyesha njia ya kujiajiri?

  2. Je tunaspirti ya ujasiriamali?

  3. Tusha anagalau anza? ili basi serikali ikija ikute tumefanya somthing?

  4. Je bado tuna story za kwamba tuna aidia nzuri sana ila tumekosa mitaji?

  5. Je hatuna unafiki?

  6. Je kama tumepenga kujiajiri na tulisha anza mikakati baadae tukaitiwa kazi tutaenda? au tutaendele na mikakati ya kijiajiri?

  LAZIMA TUBADILIKE VYUONI

  - KULE INDIA, KUNA CHUO KIMOJA CHA MASWALA YA AGRICULTURE NILIKUWA NA FUATILIA STORY ZAKE, NIKAKUTANA NA KITU CHA AJABU ASILIMI 45% YA GRADUATE HUANZISHA MAKAMPUNI YAHO/ HUJIAJIRI WENYEWE.

  - Turudi huku bongo
  - Je SUA ni asilimia ngapi wanajiajiri
  - Je UD
  - MZUMBE
  - DIT
  - UDOM
  - TUMAINI
  - SAINT AGASTINI
  Fanya research utakuta ni hakuna,

  Cha kusikitisha hata vyuo vya VETA badala ya walimu kuwandaa wanafunzi wajiajiri wao wanawapigia story za kuajiriwa

  TUACHE KULIALIA, TUBADILIKE KWANZA. TUONYESHE NJIA,
   
 3. K

  KANJARA Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asatnte sana kwa maono yako mjomba. Historia yako ni nzuri kwa maana ukitaka kufahamu au kutibu tatizo ni vyema kufahamu hisitoria. Unaposema huyu mtoto ana maadili ni vyema tukaangalia historia ya makuzi yake katika familia na hili linazibitishwa na ndugu zangu wachaga kwakuwa na monkali ya ujasiriamali kutokana na makuzi.

  Katika swala la elimu nadhani kauli za walimu ni matokeo ya mfumo uliowapa huo ualimu kwa hiyo kauli zao ni matunda ya mfumo ambao kila siku unapigiwa kelele. Nakumbuka mwalimu wakati anatunukiwa shaada ya eshima kutoka chuo kikuu HURIA CHA TANZANIA alisisitiza elimu bora yakumfanya mtu aweze kujitegemea na kuwa chachu ya changamoto zinazoikumba jamii. Pia alisisitiza kuwa na elimu ambayo inaendana na mazingira yetu nasdhani ni wakati muafaka sasa kukaa chini sote kwa pamoja kuangalia rasilimali tulizonazo na ni kwa jinsi gani tuwajenge vijana wetu kuanzia ngazi ya msingi mpakam vyuo vikuu wawe sehemu ya kuzitumia na kuzalisha mabo mbalimbali ambayo yataifanya nchi yetu kuwa na vijana na watanzania ambao wanavuna rasilimali kwa maendeleo ya chi.

  Lakini pia kuliko kutumia fedha kuendesha semina kwa watumishi badala yake uanzishwe mfuko maalumu ambao utasaidia kufadhili mawazobalimbali yanayoletwa na vijana, na mawazo hayo yawe ni ya kutengeneza fursa nyingi za ajira. Inashangaza sana fedha za uwezeshaji wananchi kutumika kutoa posho na semina kwa viongozi ambao mwisho wa siku hizo semina hazina tija kwa kundi hili la vijana.

  Pia dhana potofui iliyoingia tanzania ya kwamba kuwa na degree ndo kuwa na maendelleo si kweli tuwekeze zaidi kwenye ufundi ngazi ya cheti na stashahada tuwape vijana elimu yakuwa wazalishaji badala yakuwa ma meneja na mabosi
   
 4. b

  bagamoyo1 Member

  #4
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuna kitu kimoja ambacho sikielewi na huwa sipendi kudanganywa , serikali inatuambia kwamba asilimia 70 ya wananchi wake ni wakulima ,kwa muda mrefu tumedanganywa hivi , ili kuficha aibu ya Taifa ya takwimu halisi ya watu wasiokuwa na ajira
  niitafuta takwimu ya Tanzania (unemployment ) hakuna na kama kuna mtu anaijuwa atowe hiyo link , mimi ninachoamini watanzania wenye umri zaidi ya miaka 18 na kuendelea wako zaidi milion 10 ambao hawana ajira au ajira yao haina maslahi .
  Tanzania ni tajiri sana na kuna ajira nyingi sana zinaweza kubuniwa bila ya kutegemea wawekezaje wa njee wanatakiwa wabunifu wa miradi na serikali kusaidia miradi hiyo
   
 5. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Twende mbele na nyuma tuangalie!! Tatizo la ajira kweli lipo lakini hao waajiriwa wanaotaka kuajiriwa na wapate mishahara kwa kazi waliofanya wakowapi??!? Leo hii hapa ukiwa na ajira unataka kutoa utaajiri na kufukuza hata ishirini kabla hujampata mchapa kazi! Sisi wengi tunajiendekeza kwa kuweka tamaa za pesa mbele wakati jinsi ya kuzipata pesa hizo tunataka iwe kwa miujiza.
  nenda kijiweni kachomoe mtu mwambie twende shamba kuna ajira kama atakufata.
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kuna tatizo la ajira na kweli kuna furusa nyingi sana,
  - ILA SIAMINI KILA KITU NI MPAKA SERIKALI IFANYE, HIVI HATA BIASHARA NI MPAKA SERIKALI ITUAMBIE FANYA BIASHARA HII?

  - VIJANA WENGI WAKO VIJIWENI NI SAWA NA WENGINE WAMESOMA WANA DEGREE HATA ZA KILIMO NA UFUGAJI, WENGINE WANA DIPLOMA YA UFUGAJI NA KILIMO, ILA HAWA WOTE HAKUNA ILYE TIYALI KUSHIKA JEMBE AKALIME KISA AIBU,

  - UKIENDA NCHI ZINGINE KAMA INDIA, FILIPINE, MALAYSIA, THAILAND, VEITNAM NA KAZALIKA, WAKULIMA WADOGO NA WAKATI WEOTE WAMESOMA WANA DEGREE NA MASTER ZA KILIMO NA UFUGAJI NA WAMEAMUA KIJIAJIRI.

  - Tanzania kuna Maeneo mengi sana yanafaa kwa kilimo tena unaweza pata hata bure, ila hakuna kijana aliye tiyali kufanya hivyo, kisa anataka kazi za mijini tu,
  - KWA SASA WAKIJA WAWEKEZAJI WAKAPEWA MAENEO TUNABAKI KULALAMIKA WAKATI YAMEKAA TU BILA KAZI.

  - MIMI NINA RAFIKI YANGU MMOJA NI MKENYA, KUNA SIKU ALINUILIZA NI KWA NINI VIJANA WENGI TANZANIA UTAWAKUTA WAKO VIJIWENI IETHER WANACHEZA POOL TABLE AU WAKO TU WANAPIHA STORY?

  - SIKUWA NA JIBU LA MOJA KWA MOJA, ILA KWA KWELI HILI NI TATIZO NA KUTATULIWA KWAKE KUNAHITAJI MAAMUZI MAGUMU SANA.
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  WANATAKAKAZI ZA OFISINI, KAZI ZA KWENYE IC.

  - Ila kuna kipindi kitakuja itabidi tuvijana waende mashambani, MFANO.
  - KUNA MTU MMOJA ALINIAGIZA NIMTAFUTIEKIJANA WA KAZI WA KUKATIA NGOMBE MAJANI, NILIZUNGUKA SANA VIJIJINI KUULIZIA NAKILA NI KIULIZA NAAMBIWA HAPA KIJIJNI HUWEZI PATA MEANS HAKUNA,
  ILA NILIKUWA NIKIZUNGUKA VIJINI NAONALUNDO LA VIJANA WAKIWA VIJIWENI WANACHEZA POOLTABLE KUTWA NZIMA, NILIKUWANAJIULIZA HAWA VIJANA MBONA KILA SIKU WAKO KIJIWENI NA NIMEULIZA KIJIJININIKAAMBIWA HUWEZI PATA KIJANA WA KAZI KWA SASA KWA SABABU HAWAPO.

  - TATIZO KUBWA LINASABABISHWA NAWAZAZI, KWELI WAZAZI PAMOJA NA NDUGU NI LAZIMA TUWALAUMU.
  1. Haiwezekani kijana anaamuka asubuhianakunywa chai anaondoka anaenda kijiweni anacheza pooltable baadae anarudimchana anakula nyumbani anaondoka tena anaenda kijiweni atarudi jioni kulala.

  2. Wazazi wana sababisha vijana wawelegelege, kijana hawezi kubali kwenda kulima wakati nyumbani hajafukuzwa.

  3. Kama wazazi wangekuwa wakali sana na kijana akishafikisha umuri wa kijitegemea ni razima ajitegemee kila kitu pamoja na chakulahakuna ambaye angekuwa nafanya mzaha.

  4. Nakumbuka nikiwa wilayani MONDULIkuna mzeee mmoja alikuwa na vijana wake na wale vijana wake walikuwa wanakulanyumbani kwa kufanya kazi, hakuna mtoto aliye ruhusiwa kula nyumbani kamahajafanya kazi labuda awe naumwa, ila kama ni mzima wa afya ni lazima afanyekazi za shamba ndo ale, na ilikuwa ni sheria na watoto wake wato walisha zoeaile hali na hakuna hata mtoto wake ambae ulikuwa unaweza kumpata kijiweniamekaa anapiga story na vijana wenzake, wote walikuwa bize sana, ILA MWANZONINILIONA YULE MZEE NI SULTANI LAKINI BAADAE NIMEKUJA KUGUNDUA YULE MZEE ALIKUWASAHIHI KABISA
  .
   
 8. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu umesahau na ile kauli iliyotolewa pale UDSM na mwanansiasa mmoja aliposema kuwa VIJANA MNAPENDA KULALAMIKA!
   
Loading...