Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) naomba utufanyie tathmini ya SAFARI ZA JK katika uchumi wa TZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) naomba utufanyie tathmini ya SAFARI ZA JK katika uchumi wa TZ

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by everybody, Jan 27, 2012.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kipindi kirefu sana wananchi wamekua wakilalamikia safari za Rais Kikwete kwenda nchi za nje kwamba ni upotevu wa fedha za walipa kodi. Kwa upande wa pili Serikali imekuwa ikiiwaambia wananchi kwamba safari hizi zina manufaa kwa nchi bila kutoa tathmini halisi kwa kuangalia mfano ajira mpya zilizotokana na safari hizo, fedha iliyoongezeka katika kuondoa umaskini wa mtanzania, n.k.

  Kwa mawazo yangu, nafikiri kuna umuhimu mkubwa sana kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kuingia kati na kufanya tathmini huru ili kujua kama kweli safari hizi zina manufaa katika uchumi na maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla. Atusaidie kujua "value for money" kwenye safari hizi za Rais ambazo kila wakati zinatumia mamilioni ya fedha bila kufahamu faida zake.

  Nawakilisha
   
 2. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  We Vp?
  Mkaguzi wa serikali atawezaje kumkagua bosi wake!Ni jambo lisilo wezekana kama alimlinda Jairo atamliza aliempatia ulaji!
   
 3. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hiyo haipo kwenye political jurisdiction ya CAG...Mkuu ni mkuu bwana hizo technicalities haziingiliki.
   
 4. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  DG wa PPF husafiri nje ya nchi kwa zaidi ya 50% ya muda wake wa kuwa kazini kwa mwaka. Hata hivi niandikapo yupo Marekani na rundo la wakurugenzi. DG wa PPF hulipwa per diem ya zaidi ya shs. 1,700,000.00 kwa siku. Akiondoka saa tano na nusu usiku na KLM, basi hiyo nusu saa inalipiwa kama siku nzima (Tshs 1,700,000) Akirudi na British Airways inayotua saa moja asubuhi, hulipwa kama vile ni siku nzima (Tshs 1,7000,000.000)

  Kila mwaka CAG amekuwa akitoa hati safi katika hili. Je atamweza JK ili hali amemshindwa DG wa PPF? PCCB mko wapi mbona mnabagua? David Mattaka kila kuchapo mnamuandama hadi kumlaza keko, mbona anayoyafanya DG wa PPF haguswi? Au hagusiki?


   
 5. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na maoni yenu kwamba CAG anaweza kufunikwa na Rais. Lakini ukaguzi wake unaweza kua chanzo cha kupata suluhu. Si mmeona jinsi ambavyo kamati ya bunge iliweza kuundwa chap chap kumfuatilia Jairo ingawa CAG hakuibua yote? Hivyo kama CAG akianzisha ukaguzi itakuwa nafasi nzuri kwa bunge na kamati zake kujadili report hiyo na vile vile kuchukua hatua zaidi. Ni kweli system nzima ni mbovu ila inabidi tuanzie mahali fulani na the only solution ni kuanza kwa kumtumia huyo CAG, aje na ripoti yake then tuendelee mbele..
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  ulianza vizuri ukamaliza vibaya. Mkaguzi mkuu wa serikali ni AG na sio CAG
   
 7. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45

  Raia, wewe ndiye umeanza vibaya na kumaliza vibaya kabisaaaaaaaaaaaaaaaaa!

  AG ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  CAG ndiye mkaguzi mkuu wa serikali.
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  You can not be serious ! Mtu aliyemteuwa ? Sio Tanzania hii. Ndio maana tunahitaji katiba mpya ili hizi post zote watu waombe an wenye uwezo ndio wapatiwe. Si umeona Kenya? Deputy CJ anachunguzwa.
   
 9. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,590
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  Usingizi au?
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Ajabu ni kwamba Jaji Mstaafu Ramadhani ni miongoni mwa wanaomchunguza Nancy Baraza
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mojawapo ya faida zinazosemwa ni msaada wa $780 million toka Marekani. Pesa hizo ndizo zinatumika kuweka lami barabara za Tunduma - Sumbawanga, Tanga -Horohoro na huko songea maeneo ya namtimbo kwenda mbinga! Pia nilisoma mahala.kwamba pesa hizo zinatumika kuimarisha usafirishaji wa umeme na kwenye masuala ya maji pia. Naona kama si haba japo sijasikia toka nchi nyingine.
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Great Thinkers tuna safari ndefu ila kwa kudra za mwenyezi Mungu tutafika tu japokuwa tutakuwa tumechoooka!
   
 13. m

  muchetz JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 496
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  AG=Attorney General
  CAG=Chief Auditor General

  Kama itakusaidia
   
 14. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ww ndio katika walee wanaoangalia vibanzi kwa wenzao kumbe wao wana boriti. Kwa kuzingatia msemo huo wa hekima, nakubaliana na mawazo yako, ila ukaguzi tuanzie kwako. Je ww sio fisadi, mvivu mzururaji, kibaka, mwizi, mtoa/mpokea rushwa...? Je umeifanyia nn nchi yetu au unasubiri serikali ikufanyie kilakitu?
   
 15. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2012
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hahahaha kweli jf imeingiliwa,yan nimeamimi kipofu hawez muongoza kipofu mwenzake ny kirefu cha CAG si Chief Auditor General bali ni Controller and Auditor General
   
 16. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  CAG ni Controller and Auditor General sio Chief Auditor General

   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jamani ni Namtumbo sio kama ilivyoandikwa apo juu.
  Alafu wakaguzi wapo kwa ajiri wa kuwakagua subordinates wa boss na kumpa bosi report na si vinginevyo.
  In other words ni watchman wa ma CEO,MD,GM,MARAISI etc
  Sasa kama unaweza mkagua aliyekupa ulaji TAFAKARI baada ya hapo nini kifuate
   
 18. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naweza kuwa na hivyo vyote kwenye nyekundu, lakini situmii fedha za walipa kodi. JK anatumia hela zetu sisi walipa kodi wa Tanzania ndo maana inaniuma. Kwa hiyo mimi niibe, halafu nilipe kodi halafu mtu mwingine aje kujiienjoy tu kiulaini????!!!! Sikubaliani na hoja yako...
   
Loading...