Mkaa upigwe marufuku kuingia Dsm, gesi ishushwe bei majumbani

ray jay

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,084
485
Kama kwa siku Mkoa Tu wa Dsm mkaa wanaotumia nisawa na heka zaidi ya 50 za miti
Source: utafiti wa Waziri Makamba

Basi naona MUTUNGI ya gesi midogo ingeshushwa bei hasa MKOA wa Dsm na mkaa ingepigwa marufuku kuingia .

Gharama za Uzalishaji na uboreshaji wa Gesi mpaka kumfikia mtumiaji zipo juu sana hivyo haiwezekani kamwe kupungua.Labda kodi,umeme nk zishushwe kwanza.
 
Na tutazidi kulia tu,kwa sasa maana vipaumbele vyetu sio maendeleo.
 
  • Thanks
Reactions: 999
Hakika mkaa ni janga la Taifa. Bila kushughulikia suala la mkaa tunajitengenezea janga kubwa la mazingira. Pamoja na kwamba gesi inatakiwa kushuka bei ili kunusuru misitu yetu pia watu inabidi wabadilike. Kuna watu wanaamini kwamba wali uliopikwa kwa mkaa ni mtamu kuliko wali uliopikwa kwa gesi ama umeme. Hawa huwaambii kitu juu ya mkaa watautafuta hata kwa magendo ili mradi wapate wali uliopaliwa kwa mkaa.
 
Kama kwa siku Mkoa Tu wa Dsm mkaa wanaotumia nisawa na heka zaidi ya 50 za miti
Source: utafiti wa Waziri Makamba

Basi naona MUTUNGI ya gesi midogo ingeshushwa bei hasa MKOA wa Dsm na mkaa ingepigwa marufuku kuingia .

ni kweli kabisa
 
Hivi kama tunao mkaa 'coal' kwa nini usiwe processed ukatumika majumbani? Utashi wetu kama taifa katika kulinda mazingira ni upi?
 
Kitambo gas yetu tunayoisikia kila siku kwenye midomo ya wanasiasa wakipigia kampeni ikianza kujazwa kwenye mitungi ya gas kwa matumizi ya nyumbani hapo kidogo tunaweza pata unafuu lakini sio kutegemea orxy,lakegas,mihane haya makampuni ya nje washushe bei. Ni ndoto
 
Hivi kama tunao mkaa 'coal' kwa nini usiwe processed ukatumika majumbani? Utashi wetu kama taifa katika kulinda mazingira ni upi?
Yaani unataka kulinda mazingira kwa kupiga marufuku mkaa na kuhimiza matumizi ya makaa ya mawe kama mbadala? Unalinda mazingira kwa kuyachafua zaidi!!!
 
Hakuna mbadala wa mkaa kwa sasa.hyo gesi ukiamua kupikia kila kitu.hata wiki 3.haifiki.watu was uswahili na vijijini wataweza kununua gesi ndogo kilo 6.kwa 18,000?kilo kumi na tano kwa 48,000?
 
Hakika mkaa ni janga la Taifa. Bila kushughulikia suala la mkaa tunajitengenezea janga kubwa la mazingira. Pamoja na kwamba gesi inatakiwa kushuka bei ili kunusuru misitu yetu pia watu inabidi wabadilike. Kuna watu wanaamini kwamba wali uliopikwa kwa mkaa ni mtamu kuliko wali uliopikwa kwa gesi ama umeme. Hawa huwaambii kitu juu ya mkaa watautafuta hata kwa magendo ili mradi wapate wali uliopaliwa kwa mkaa.
ingawa hii dhana ina ukweli.lakini kwa manufaa ya kizazi kijacho, ni dhana dhaifu yafaa kuwekwa kando kwanza.

Au kodi iongezwe huko kwenye mkaaa mara dufu, yaani mkaa uwe anasa nchini si gesi na umeme.
 
Weeee.unayajua makaa ya mawe moto wake?.unayeyusha hadi sufuria.
Yaaa najua hilo ndio maana nikasema yawe processed; mwaka jana nilikula mishikaki iliyochomwa kwa kutumia mkaa wa mawe viungani mwa beijing nafikiri ipo namna ya kuyafanya yawe mbadala wa mkaa wa miti
 
Nilimsikia waziri akisemw kuwa watapandisha Uhuru. Ni wakati wa serikali kuchukua hatua za haraka sana tujaimaliza nchi hii na vizazi vijavyo watapata tabu sana nchi itageuka jangwa.
 
Acheni unafki,haito tokea cku binadamu akamaliza msitu eti kwa ajili ya mkaa tu,wameanza kutumia mababu na mababu mbona haujesha??Allah ameweka balance kati ya supply and demand.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom