Mkaa upigwe marufuku kuingia Dsm, gesi ishushwe bei majumbani

Nyumba za watu zitaungua
Matumizi ya gas yanataka uangalifu sana

Kuna demu mmoja nilikuwa naishi naye nikamwambia jiko la gas hilo hapo tumia ila uwe makini alikataa kata kata kutumia ikabidi niwe natumia mwenyewe.
 
Acheni unafki,haito tokea cku binadamu akamaliza msitu eti kwa ajili ya mkaa tu,wameanza kutumia mababu na mababu mbona haujesha??Allah ameweka balance kati ya supply and demand.

Hauko serious.

Huyu allah si kila sehemu ana fit sehemu zingine mnamtukanisha.nenda morogoro mjini waulize wazawa, ule mlima miaka ya 2000 kurudi nyuma ulikuwaje na nini sababu ya kuwa hivi ulivyo sasa???unajua rc anafanya juhudi gani kuurudisha ulivyokuwa??? Huo ni mfano mmoja.

Mimi nimeishi maeneo ya mororgoro ngerengere huko, maeneo maarufu ya misitu ya mkaa na mbao.nilirudi kwa ishu zingine za kikazi aisee nilichoka.miti imefyekwa mpaka inaogofya na watu wanaendelea kuifuata inakopatikana.

Hizo tani zinazowaka kwa siku dar es salaam pekee ni mamia ya heka za miti zilizofyekwa huko, bila juhudi yoyoye ya kuiotesha tena.acha twende mpaka 2050 matokeo tutaanza kuyaona moja kwa moja.
 
kaka kwanza ni kupongeze kwa kuandika mada yenye mashiko na muhimu sana kwa mstakabali wa taifa letu kuelekea kuwa jangwa.

Kuna vitu Ambavyo Serikali inapaswa ivi angalie kwa umakini mkubwa na kwa haraka sana.

Jambo hili likichukuliwa kama mzaa na Serikali basi miaka 10 ijayo Tanzania hatuta icheka Misri kwamba ni nchi kame na jangwa.

Bali tutavuna tulicho kipanda.

Hai ingii Akilini Serikali ikavipa Kipaumbele Vingamuzi kwa kuondoa Kodi ili kila Mtanzania aweze kununua kingamuzi.

Lakini la muhimu kama Gas Serikali inapata Uzito wa kuongoa Kodi ili kumwezesha kila Mtanzania kununua na kuondokana na matumizi ya mkaa yatakayopelekea madhara makubwa kwa Taifa.

Kama Serikali iliweza kwenye Vingamuzi! Watu tukanunua Kingamuzi mpaka Elf 26 kwa Ges imeshindwa nini?

Karibuni tujadili jambo hili kwa kina maana najua wakubwa wanasoma mada hii.
 
Kitambo gas yetu tunayoisikia kila siku kwenye midomo ya wanasiasa wakipigia kampeni ikianza kujazwa kwenye mitungi ya gas kwa matumizi ya nyumbani hapo kidogo tunaweza pata unafuu lakini sio kutegemea orxy,lakegas,mihane haya makampuni ya nje washushe bei. Ni ndoto
Ni kweli kabisa hiyo gesi ya mtwara mpaka iingizwe kwenye mitungi labda baada ya miaka 100
 
Acheni unafki,haito tokea cku binadamu akamaliza msitu eti kwa ajili ya mkaa tu,wameanza kutumia mababu na mababu mbona haujesha??Allah ameweka balance kati ya supply and demand.
Makadirio ya Food and Agriculture organization yanaonyesha uzalishaji wa tani milion 30.6 za mkaa kwa mwaka barani Africa. Miti inayoangushwa kutengeneza mkaa wote huo ni kiasi gani? Maeneo mengi kaskazini mwa Dar miti imeisha. Ukuwa barabarani kuanzia Segera kuelekea Dar hasa nyakati za usiku hewa imejaa harufu ya mkaa kutoka kwenye matanuru ya kutengeneza mkaa. Hali ni mbaya sana completely out of control.
 
Back
Top Bottom