Mjuzi anifahamishe tija (Faida) inayopatikana katika free apps kwa wahusika

papaayenga

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
765
500
Naomba kuuliza kwa wale wanao tengeneza free app. Wanapo zituma kama vile YouTube au katika website nyingine huwa wanalipia katika hizo site? Na kama wanalipia wawo hupataje kipato kwa kaziyao hiyo wakati wawo huzitangaza kuwa ni app. za bure?

Pia mtu binafsi anapo upload clip yake YouTube au sehemu nyingine huyo mwenye clip hiyo hufaidika vipi kwa watu kuitazima maana takuta kila clip inaorodha ya idadi ya watu walio ipitia hii inasaidia nini?

Pia kupeleka clips huko YouTube na kwingineko huwa kunahiaji kibali au leseni?

Tafadhali naomba watu wenye elimu na hili jambo wanifahamishe. Kama hulifahamu utakuwa muungwana ukikaa kimya.Sent using Jamii Forums mobile app
 
papaayenga

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
765
500
YouTube wanafaidika kwa kuuza matangazo ya biashara. Ndiyo maana wanaoweka video YouTube wanalipwa kama Mtazamaji ataangalia na video ya tangazo nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nashukuru tafadhali unaweza kunifafanulia jinsi ya malipo inavyokua kwa mfano mie nanunua bando ktk kampuni ya airtel kwa . 500/- Halafu naingia utube inakuwaje hapo tayari hela anayo airtel

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
1,992
2,000
Nashukuru tafadhali unaweza kunifafanulia jinsi ya malipo inavyokua kwa mfano mie nanunua bando ktk kampuni ya airtel kwa . 500/- Halafu naingia utube inakuwaje hapo tayari hela anayo airtel

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa unamaanisha nini!?

Hiyo kero iliyonunua Airtel bundle ndo wanayofaidika Airtel.

Kuperuzi kwako mtandaoni hakuilipi Airtel Bali kununua kwako aiirtel bundle.

YouTube utaipata kwa bandia lako la Airtel n.k, lakini kwa kuwa unatumia YouTube zaidi utambue kuwa kuna biashara za watumishi zinafanyika chini ya jua na wafanya biashara hao wanataka wateja wengi, na wateja hao wanapatikana kwa wingi mtandaoni hasa YouTube.

Kwa hiyo mimi kama mfanya biashara nitalipa kampuni inayomiliki YouTube website/app ili kutangaza biashara yangu kupitia video za zilizopo YouTube kwa mfano video za mond zinawatazamaji wengi kama biashara yangu ilitangazwa kupitia video hiyo ujue nimeshajulikana karibia dunia nzima huoni napata faida kwa kutafutwa wordwide na wateja hivyo YouTube au mumliki wa app inayotumia kutangaza naye atataka chake.
Ndio hivyo

Labda sijakusoma
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
26,781
2,000
Naomba kuuliza kwa wale wanao tengeneza free app. Wanapo zituma kama vile YouTube au katika website nyingine huwa wanalipia katika hizo site? Na kama wanalipia wawo hupataje kipato kwa kaziyao hiyo wakati wawo huzitangaza kuwa ni app. za bure?

Pia mtu binafsi anapo upload clip yake YouTube au sehemu nyingine huyo mwenye clip hiyo hufaidika vipi kwa watu kuitazima maana takuta kila clip inaorodha ya idadi ya watu walio ipitia hii inasaidia nini?

Pia kupeleka clips huko YouTube na kwingineko huwa kunahiaji kibali au leseni?

Tafadhali naomba watu wenye elimu na hili jambo wanifahamishe. Kama hulifahamu utakuwa muungwana ukikaa kimya.Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna msemo maarufu online unasema

if its Free you are a Product

Kwa tafsiri isio rasmi kama ni bure wewe ndio bidhaa yenyewe.

App nyingi (sio zote) ambazo ni bure wanapata hela kwa kukuwekea matangazo ama kukusanya Taarifa zako.

Mfano unatumia Instagram ama Facebook si kila posti unayoiona ametuma rafiki yako, nyengine zimeekwa na facebook kama Matangazo, unaperuzi facebook unaona posti simu inauzwa unachukua namba unapiga unanunua, kumbe yule muuza simu amelipia facebook elfu kadhaa ili tangazo lake waone watu wengi.

Njia nyengine ni hio ya kukusanya taarifa zako, unaitwa nani, unakula nini, unakaa wapi, unavaa nini, unaumwa nini etc. Unaweza siku umeagizwa pharmacy ukanunue dawa ya kifua, ukiingia google tu tayari wanakuwekea matangazo ya dawa. Hizi taarifa zinauzwa bei mbaya kwa makampuni/mamlaka kubwa duniani.
 
The best 007

JF-Expert Member
Oct 6, 2019
24,803

Ww uliza kwa urahisi tu maxence melo anapataje pesa kupitia ww kuitumia jf
 
papaayenga

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
765
500
Hapa unamaanisha nini!?

Hiyo kero iliyonunua Airtel bundle ndo wanayofaidika Airtel.

Kuperuzi kwako mtandaoni hakuilipi Airtel Bali kununua kwako aiirtel bundle.

YouTube utaipata kwa bandia lako la Airtel n.k, lakini kwa kuwa unatumia YouTube zaidi utambue kuwa kuna biashara za watumishi zinafanyika chini ya jua na wafanya biashara hao wanataka wateja wengi, na wateja hao wanapatikana kwa wingi mtandaoni hasa YouTube.

Kwa hiyo mimi kama mfanya biashara nitalipa kampuni inayomiliki YouTube website/app ili kutangaza biashara yangu kupitia video za zilizopo YouTube kwa mfano video za mond zinawatazamaji wengi kama biashara yangu ilitangazwa kupitia video hiyo ujue nimeshajulikana karibia dunia nzima huoni napata faida kwa kutafutwa wordwide na wateja hivyo YouTube au mumliki wa app inayotumia kutangaza naye atataka chake.
Ndio hivyo

Labda sijakusoma

Nashukuru nilipotaka fahamu ni kati ya airtel na utube au fb na alie post clip biashara hii ikoje kuhusu ile 500 nilio nunua bando?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,862
2,000
Nashukuru tafadhali unaweza kunifafanulia jinsi ya malipo inavyokua kwa mfano mie nanunua bando ktk kampuni ya airtel kwa . 500/- Halafu naingia utube inakuwaje hapo tayari hela anayo airtel

Sent using Jamii Forums mobile app
Kampuni za simu hazishare chochote na mtandao wowote unaotembelea, watu wengi uwa wanawaza hivi lakini siyo kweli ukiweka bundle ela ni ya kampuni ya simu wao watakuja kulipa kwa mmiliki wa mkonge mfano kama seacom
Tovuti, na app wanapata ela kutokana na matangazo mfano ukiwa watazama video youtube unaweza kuta linatoka tangazo la sbt japan au voda basi voda wamewalipa youtube kwa ajili ya matangazo nao youtube kupitia hiyo ela watampa mmiliki wavideo % inayobaki ya kwao.
Wenye tovuti na blogs hivyo hivyo kama umewahi kusikia kitu kama google adsense au propellar ads yani wanakuwa wanaweka matangazo ya huduma na makampuni na unalipwa kutokana na watembeleaji.
Facebook naye anauza matangazo ndo maana ukiwa facebook mara uone tangazo la voda mara uone sijui tangazo la magari wale wamelipa hiyo huduma. Pia nawe unaweza lipia facebook wakutangazie kitu
 
RReigns

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
17,046
2,000
Nashukuru nilipotaka fahamu ni kati ya airtel na utube au fb na alie post clip biashara hii ikoje kuhusu ile 500 nilio nunua bando?

Sent using Jamii Forums mobile app
youtube hafaidiki chochote na hela ya bundle ile hela ni kama njia au unalipia nauli kukufikisha sehemu kupata huduma.

Mfano umepanda gari kwenda kariakoo kununua nguo. Ile nauli muuza nguo ana manufaa nayo?
 
papaayenga

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
765
500
Kuna msemo maarufu online unasema

if its Free you are a Product

Kwa tafsiri isio rasmi kama ni bure wewe ndio bidhaa yenyewe.

App nyingi (sio zote) ambazo ni bure wanapata hela kwa kukuwekea matangazo ama kukusanya Taarifa zako.

Mfano unatumia Instagram ama Facebook si kila posti unayoiona ametuma rafiki yako, nyengine zimeekwa na facebook kama Matangazo, unaperuzi facebook unaona posti simu inauzwa unachukua namba unapiga unanunua, kumbe yule muuza simu amelipia facebook elfu kadhaa ili tangazo lake waone watu wengi.

Njia nyengine ni hio ya kukusanya taarifa zako, unaitwa nani, unakula nini, unakaa wapi, unavaa nini, unaumwa nini etc. Unaweza siku umeagizwa pharmacy ukanunue dawa ya kifua, ukiingia google tu tayari wanakuwekea matangazo ya dawa. Hizi taarifa zinauzwa bei mbaya kwa makampuni/mamlaka kubwa duniani.

Hapa nilikua namaanisha baadhi ya clips au games kuna clips au game kuzitizama ni bure hakuna malipo na zingine mpaka ulipie hata kama bandle unalo ndio utaiona. Sasa zile za bure mwenye clip anafaidika vip kutokana na wanao itizama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
papaayenga

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
765
500
Kampuni za simu hazishare chochote na mtandao wowote unaotembelea, watu wengi uwa wanawaza hivi lakini siyo kweli ukiweka bundle ela ni ya kampuni ya simu wao watakuja kulipa kwa mmiliki wa mkonge mfano kama seacom
Tovuti, na app wanapata ela kutokana na matangazo mfano ukiwa watazama video youtube unaweza kuta linatoka tangazo la sbt japan au voda basi voda wamewalipa youtube kwa ajili ya matangazo nao youtube kupitia hiyo ela watampa mmiliki wavideo % inayobaki ya kwao.
Wenye tovuti na blogs hivyo hivyo kama umewahi kusikia kitu kama google adsense au propellar ads yani wanakuwa wanaweka matangazo ya huduma na makampuni na unalipwa kutokana na watembeleaji.
Facebook naye anauza matangazo ndo maana ukiwa facebook mara uone tangazo la voda mara uone sijui tangazo la magari wale wamelipa hiyo huduma. Pia nawe unaweza lipia facebook wakutangazie kitu

Ahsante
kongole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom