MJUWE MICHEL MARTELLY: Mgombea Urais Haití

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
0
Michel Martelly ni mwimbaji na mpiga piano ambaye aliamua kujitosa katika nafasi ya kugombea uraisi akiwa na nafasi ndogo ya kuchaguliwa. Alipoanza kinyangányiro alikuwa yuko nafasi ya nane katika utabiri wa kura lakini alimudu kuingia katika raundi ya pili kwa kishindo. Na kama si kwa ajili ya uchakachuaji wa kura, anglikuwa amechaguliwa katika duru ya kwanza. Kwa nini alifikia hatua hiyo?
Michel, au Sweet Micky kwa jina la usanii, hakusoma sana. Alianza chuo kikuu katika fani ya Medicine lakini aliwacha chuo kwa ukali maisha. Mwisho wa safari yake ya kutafuta maisha alikamata Mic na kuanza kutumbuiza katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kiitikadi, ni mtu anayepinga na "system" asiye na chama chochote cha siasa. Chama chake ni watu, ni wanyonge na wahanga wa rushwa na majanga ya kibinadamu. Mbali ya muziki, hugawa zawadi kwa watoto wakati wa Krismasi, kujenga mamia ya nyumba kwa watu masikini, ni mmiliki wa kituo cha kuwasidia wagonjwa wa ukimwi.
Wakati wagombea wenzake wakitumia mamilioni ya dola katika kampeni huku wakilindwa na kuongozwa na vimulimuli, Michel alikuwa anapita nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa akifanya kampeni na kundi lake la muziki huku akitumbuiza kwa mitindo ya Carnaval, midundo na miondoko ya Kiafrika. Kampeni hasa alikuwa anaifanya pale umma ulipokuwa unatekea kwa majanga wakati wanasiasa wako mafichoni.
Sasa tusubiri baada ya miezi miwili katika duru ya pili tuone atafikia wapi. Binafsi wasiwasi wangu ni nguvu za uchakachuaji, lakini umma Haití unamtaka na uko pamoja naye.

http://www.youtube.com/watch?v=0MCVp22yCYc&feature=fvst
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom