Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la Vijana CHADEMA wilaya ya Ilemela ajiengua uanachama!

Hivi siku hizi mtu ukihama chama chako kiwe ccm au chadema je, ni lazima uite waandishi wa habari? Au mimi ndio sielewi hizi siasa? naomba mnieleweshe.
Queen Esther
queen ni ajabu kwa watu wanaotumika yaani KUBWA JINGA kwa nini unapojiunga na chama chochote cha Siasa hauiti Press Conference lakini ukitoka unaita Press Conference je hao waandishi nao huwa wanajua wanachoitiwa au wao wanaenda tu sababu wanajua wanapata habari? Waulizeni hao wanaowaita kwamba mbona wakati unajiunga na kula posho zao haukutuita iweje mabaya yawe wakati unatoka lakini mazuri wakati umo unfaidi hauyasemi? Ni unafiki wa watu wazima
 
Last edited by a moderator:
Mwajiri akiwa hajali maslahi ya wafanyakazi wake utakaa tu "hewala bwana mkubwa"?

SIO KWELI, ILA KWA MWENYE MALENGO BINAFSI YA KUNENEPESHA TUMBO LAKE CHADEMA HAPAMFAI, ELa ZA KIFISADI NA ZA KIJANGILI ZIKO CCM
 
Hakika wanafiki, wazindiki na wasaliti CHADEMA si mahali pao salama hata siku 1..
 
Samson Boroyi Chacha nani asiyemjua? Kweli huyu tapeli ndio wa kuita waandishi eti anatangaza kujiengua? Habari zake za toka yuko Sunrise Secondary hadi Thaqaafa tutaziweka wazi ili watu wamtambue.

Hapa ndipo mimi huwa napinga mwisho wa siku naonekana eti sio CDM,hivi CDM ni mtu ama ni watu?!,kwa nini haya maneno yaanze baada tu ya kuondoka CDM,mwachezni aende chama si kina watu wengi jamani!

Hizi sasa ni hasira za kukimbiwa au ni nini?!!,Pili leo bada ya kujiengua CDM ndiyo mnamtishia kwamba mnazijua habari zake toka akiwa sekondari?,kwani wakati akiwa CDM hamkuyasma hya wandugu?!,haya wekeni inaonekana imewauma sana!!!!!
 
Ukileta mchezo kwa chadema kuna watu wengi.wengine wanapanda mlima wengine wanashuka.
 
Yaani watu wanapoteza muda kumjadili huyu tapeli.

Hivi leo ndiyo utapeli wake umeonekana bada ya kutoka CDM?!,hii ni aibu kuna mambo mengine ni kutulia otherwise mtu unaweza kuonekana "Nying'anying'a"
 
Inasikitisha Mtu mzima,Baba mwenye familia,Mama mwenye mji wake unakuwa MALAYA leo uko huku kesho uko kule inaonyesha kutokuwa makini na unachokifanya uliamua kwa mapenzi yako nitakuwa mwanachama wa chama fulani ukitokea uchaguzi ukishindwa unaanza vitimbi ili utoke ulienda huko kwa mapenzi ya chama au kwa maslahi yako ili upate uongozi? Watu kuweni na msimamo na si kukurupuka na kutokuwa na msimamo inareflect hata kwako hauna msimamo pia

Wewe ni kiongozi umeona hautendewi haki sema wazi ukiwa humo humo ya nini kukimbia na kuanza kuongea majungu? Ulishindwa nini kusema ukiwa humo humo? Mnakosa misimamo ndio maana wengine jawana hata pa kwenda shauri ya majungu yenu, Wengine walia majukwaani kwamba fulani alinotaka nikakataa sawa huyo ulimkataa uliowakubali mbona huwataji?

Tuwe wakweli tamaa ya madaraka itawamaliza,wote mkiwa viongozi nani atakuwa muongozwa?
 
Hivi huyu nae kulikuwa na haja kuita vyombo vya habari? Ni ishara tosha kuwa huyu anatafuta umaarufu. anafikiri akijitangaza kwenye vyombo vya habari na kuimba nyimbo za Nape watamsikiliza.
Vyama vya siasa vimejaa wachumia tumbo wanaofikiri watawin maisha kwa kupata umaarufu kwenye vyama vya siasa. Wengine wakikosa njia yoyote ya kuwa na nafasi kwenye vyama wanaanza vimbwanga vyao. Niliona hili nilipohudhuria mara ya kwanza kwenye kikao cha chama nilisikitika sana. CDM wasivokuwa wapuuzi juzi wametangazwa kusimamishwa uongozi na uanachama. Inasikitisha lakini tujue kuwa wengi hasa wale wanaowania nyadhifa mbalimbali kwenye chama si wapiganaji bali watafutaji wa maisha.
Ni vyema chama kikaweka utaratibu na msimamo usiotetereka kuwathibiti hawa watafutaji na walaji.
 
Fikra rahisi tu,huyu jamaa ni kilaza,akimbiliako ni kwa "maviLaza" waliobobea,hataambulia hata ubalozi wa nyumba 10.
Hana hata jema la kusifia?ni jinsi gani asivyojitambua.
 
Hivi siku hizi mtu ukihama chama chako kiwe ccm au chadema je, ni lazima uite waandishi wa habari? Au mimi ndio sielewi hizi siasa? naomba mnieleweshe.
Queen Esther


Mkuu inashangaza kidogo


- wakati wa kujiunga huwa hawaiti waandishi wa habari

-wanapoharibu na kufanya misigano ya ndani kwa ndani huwa hawaiti waandishi wa habari

wanapoondoka kwa huita waandishi, malengo yakiwa:-

1. Kujikweza nakujipatia umaarufu wa kupaka rangi kutoka vyombo vya habari

2. kwa wanaofuatilia siasa za maji taka, propaganda na kuharibu sifa ya vyama watokako, hawa ni wachafuzi na matapeli wa siasa

3. kwa wanaofanya siasa biashara kama daladala, anaponunuliwa ilikuharibu sifa au kupaka matope chama kingine wakipewa vijisenti hawana breki moja kwa moja mbele ya kamera kukidhi mahitaji ya visenti alivopewa.

4. kwa wachache wapenda haki hutoka chama kimoja kwenda kingine wanapoona ubora na malengo walioyahitaji ndani ya chama
yametoweka, hawa mara nyingi hawaiti wanahabari.


Huyo aliyehama tusubiri anahamia chamagani ndipo tutagundua true color yake.
 
Samson Boroyi Chacha nani asiyemjua? Kweli huyu tapeli ndio wa kuita waandishi eti anatangaza kujiengua? Habari zake za toka yuko Sunrise Secondary hadi Thaqaafa tutaziweka wazi ili watu wamtambue.

Mkuu hebu fasta muanike huyu mamluki, mi ndo leo namfahamu, nadhan asepe zake tuuuuuu
 
Sasa nimeamini watz hatuoni mbali na wala hatutafika mbali, kweli wewe kwa sababu ya tumbo tuu ndo unakubali kuwasaliti millions of people for what reasons?? Ili uwe tajiri au uishi maisha mazuri. I am speechless, good lucky.
 
Upepo umewakalia vibaya CDM yetu macho

UPIU kama kuna chama upepo umewkalia vibaya ni Ccm hata wewe najua unaelewa,ziara za katibu mkuu na Mawaziri imeishia wapi baada ya kuzomewa kila walipoenda wamezomewa wameona aibu wameacha wakaanza kutishia watumishi wa umma kuwafukuza,bado mtasema sana mmekaliwa vibaya Ccm hamtoki salam hiyo mnajipa moyo tu
 
Last edited by a moderator:
Namtakia kila raheli uko aendako, ila kwa sababu alizozitoa kujiondoa chadema hazina mashiko. Chama kina maamuzi yake ambayo kama mfuasi huna budi kuyafuata au unajiondoa si kumtuhumu mtu mmoja mmoja kama alivyo fanya huyu mura. Dr kigwangala alikuwa watatu kwenye kura za maoni na akachukuliwa kubeba bendera ya ccm, seleli na msomali mbona hawakujitoa ccm? Na wasi wasi huyu jamaa amenunuliwa!
 
Back
Top Bottom