Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la Vijana CHADEMA wilaya ya Ilemela ajiengua uanachama!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
TUESDAY, DECEMBER 4, 2012

buroyi+1.jpg

Bw. Samson Chacha Boroyi

KADA wa CHADEMA Bw. Samson Chacha Boroyi ambaye ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza, amejiengua katika chama hicho huku akikiponda chama hicho kuwa kinaongoza nchini kwa kuwafanya watu Chambo na kuongozwa kwa maslahi ya Ukanda .

buroyi+2.jpg

Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Mwanza amewataja waziwazi baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakiwemo wale wa Kitaifa kuwa hawataki kutii Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi hivyo siku wakipatiwa Dola, hali itakuwa mbaya kuliko ya Misri na Libya.

Mwalimu Samson Boroyi ameyasema hayo huku akikiita Chama hicho kuwa ni Kampuni ya kundi dogo la vigogo wa Kanda ya Kaskazini japokuwa wamekuwa wakijinadi kuwa ni Taasisi ya Kisiasa, alidai kwamba viongozi wa Chama hicho wakiwemo Katibu Mkuu Dkt Willbroard Slaa wamekuwa wakiitumia CHADEMA vibaya kwa kushindwa kufuata Katiba yake na hata kuwa watu wasiotii sheria za Nchi na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw.Boroyi ambaye pia alikuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela, alieleza kwamba pamoja na chama hicho kuendeshwa kama kampuni ya mtu binafsi, kundi hilo dogo ndilo linalotoa maamzi bila kuzingatia Katiba yake na maslahi ya wengi.

Ameongeza kuwa hata Bw Wenje alitoa ahadi ambayo ameshindwa kuitekeleza tangu aitangaze kwenye mikutano yake ya hadhara na kujigamba kusomesha watoto 1,960 katika Sekondari za Kata na kuzipatia madawati, kuboresha huduma ya Hospitali ya wilaya ya Nyamagana ya Butimba wakati hali ni kinyume na mbwembwe hizo.
buroyi+3.jpg

Hata hivyo Bw.Boroyi hakuwa tayari kutaja chama atakachojiunga nacho hadi hapo baada ya wiki mbili,atakapokuwa ametafakari kwa kina ni Chama kipi bora atakachojiunga nacho ili asikosee tena kama alivyopotea muda wake kujiunga na Chadema toka mwaka 2007akiwa mwanachama hai kwa Kadi namba 0359614 na kuahidi kuirejesha Kadi hiyo kwa Katibu wa Wilaya ya Ilemela Jumatatu ijayo ili kuthibitisha kukiacha kabisa chama hicho.

SIKILIZA AKIONGEA na WAANDISHI

[JFMP3]http://ak-media.soundcloud.com/5rGvAbGlSOv3.128.mp3[/JFMP3]

Posted by Albert G.Sengo
Tumtakie kila la heri kwenye safari yake ya kuelekea upotevuni. Better few but better. Jeshi lenye wapiganaji wenye ari, nia na dhamira, wanaojua wanachokifanya ndilo hatimaye hushinda, not just a collection of individuals.

Katika safari hii, wapo watakaokata tamaa, wapo watakaosonga mbele, wapo watakaosaliti, wapo watakaokuwa watiifu, wapo watakaogeuka nyuma, wapo watakaosema mbele kwa mbele, nyuma mwiko, wapo watakaotaka njia za mkato, wapo watakaojua safari hii yahitaji uvumilivu na kujitoa, wapo watakaoanguka, wapo watakaobeba silaha zao na kusonga mbele, wapo watakaofika mpaka mwisho wapo watakaoishia njiani hata kama walitamani kuona mwisho mwema wa kile ambacho kila Mtanzania mpenda nchi yake anatamani kukiona miaka michache ijayo.

Kama tayari ameimba kibwagizo cha Nape cha elements za ubaguzi, ishara ya mtu asiyeweza kujenga hoja dhidi ya CHADEMA, hana haja ya kuwadanganya watu anafikiria. Kama hana uwezo wa kufikiria beyond his tribe and religion, he deserves what he has done.

Watu wa Kanda ya Ziwa hatundanganyiki tena. Mnakotaka kulalia, ndiko tulikoamukia. Watu wa Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, kama mababu zetu walivyoshikamana na Watanzania wote wakati kupambana dhidi ya mkoloni, kizazi cha sasa hatutakubali kudanganywa kwa nyimbo hizi za kuchelewesha ukombozi wa pili wa Tanzania.
 
Akawasalimie huko aendako,maana waliopo hawataki na anaotegemea waingie hawaamini. Tunasubiri mwelekeo wake sijui ni ccm au cuf!
 
Mwita Maranya, jamaa yako kauona ukweli. Tukisema sisi mnatushambulia, Chadema kinaelekea pazuri sasa.
 
Last edited by a moderator:
huyo poyoyo wa wapi tena? anatafuta umaarufu kupitia migongo ya watu
 
Tumtakie kila la heri kwenye safari yake ya kuelekea upotevuni. Better few but better. Jeshi lenye wapiganaji wenye ari, nia na dhamira, wanaojua wanachokifanya ndilo hatimaye hushinda, not just a collection of individuals.

Katika safari hii, wapo watakaokata tamaa, wapo watakaosonga mbele, wapo watakaosaliti, wapo watakaokuwa watiifu, wapo watakaogeuka nyuma, wapo watakaosema mbele kwa mbele, nyuma mwiko, wapo watakaotaka njia za mkato, wapo watakaojua safari hii yahitaji uvumilivu na kujitoa, wapo watakaoanguka, wapo watakaobeba silaha zao na kusonga mbele, wapo watakaofika mpaka mwisho wapo watakaoishia njiani hata kama walitamani kuona mwisho mwema wa kile ambacho kila Mtanzania mpenda nchi yake anatamani kukiona miaka michache ijayo.

Kama tayari ameimba kibwagizo cha Nape cha elements za ubaguzi, ishara ya mtu asiyeweza kujenga hoja dhidi ya CHADEMA, hana haja ya kuwadanganya watu anafikiria. Kama hana uwezo wa kufikiria beyond his tribe and religion, he deserves what he has done.

Watu wa Kanda ya Ziwa hatundanganyiki tena. Mnakotaka kulalia, ndiko tulikoamukia. Watu wa Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, kama mababu zetu walivyoshikamana na Watanzania wote wakati kupambana dhidi ya mkoloni, kizazi cha sasa hatutakubali kudanganywa kwa nyimbo hizi za kuchelewesha ukombozi wa pili wa Tanzania.
 
Tumaini Makene

Msipuuze madai yake ni muhimu kuyafanyia kazi kwa mustakabali wa Chadema.
 
Last edited by a moderator:
huyo poyoyo wa wapi tena? anatafuta umaarufu kupitia migongo ya watu
Mtu mzima unapompiga mtoto wako kwa fimbo, ukiona halii wala kuomba msaada jiulize mara mbili. Siasa ina mapito yake kama mchezo wa draft, usipoangalia kete zinaliwa unabaki patupu.CHADEMA hawa wanachama wenu wanaoondoka msiwapuuze kwa kuwaita mapoyoyo na majina mengi ya kejeli. Huyu ni Mjumbe wa kamati tendaji, wilaya(ilemela) ni mwanachama hai tangu 2007, kadi ya laki tatu na nusu(0359614). Upepo unaenda pabaya.
 
Hapo jamaa ni lazima atakuwa amepata mshiko wa nguvu. Kweli njaa, iogope.
 
Back
Top Bottom