Mjumbe wa Baraza la Maulamaa na Imamu wa Msikiti wa Manyema, amewageukia wanaokataa kura ya wazi.

Kama wajumbe wameenda kwenye bunge la Katiba kusimamia maslahi ya wananchi waliowatuma, kitu gani kinawafanya watake kujificha kwenye maamuzi ya mwanvuli wa kura ya siri katika kupitisha, kukataa au kubadilisha vipengele vya Rasimu ya Katiba?.

Wananchi wanataka kufahamu kile wajumbe wao wamekikubali na kukikataa bungeni ili iwe ni historia iliyoandikwa kwa kila mjumbe na siyo kwa mwanvuli wa wajumbe wote wa bunge la Katiba.

Kujificha kwenye kura za siri katika maamuzi haya muhimu ya kitaifa ni kujenga taifa la waoga na wanafiki kitu ambacho ni hatari sana katika mstakabali wa Taifa endelevu.

Wananchi wanataka kuweka historia wazi kwa kila mjumbe kwa kizazi hiki na cha baadaye.

Kama kuna watu wameingia kwenye Bunge la Katiba bila kuelewa umuhimu wao katika mstakabali wa taifa na mpaka sasa bado wameendelea kuwepo, basi hawataweza kusamehewa kwa makosa makubwa kama haya kwa taifa.

Kila mjumbe lazima aubebe msalaba wake wa kuingia kwenye bunge la Katiba na siyo kujificha kwenye mwanvuli wa corrective responsibility.

Moja ya nguzo kuu ya CCM iliyochangia kwa chama kudumu mpaka sasa katika ahadi zake ni pamoja na kusema kweli daima na fitina ni mwiko.

Huyu Shekhe ni kibaraka wa Maccm! Na hapo ndio naamini ccm wamejazana mle!
Kikwete mbona unajisuta? Si wewe ukietaka katiba mpya!
Sasa mbona umejaza wapuuzi mle?
 
Kura ya kificho ni uhuni kwani tunaficha nini mangapi tumefanya wazi watanzania wanataka kuona mchakato wote hakuna kificho hapo.

Aisee! Kweli CCM mmenyweshwa maji ya bendera! Yani hata mbuturi matari wa mitaani ndio msee!
 
Jamani wana JF na hili lituhangaishe? Siri na sio Siri? Yaani nini faida ya kuwa ya Siri na nini faida ya kuwa ya wazi? Nini hasara ya Siri na wazi?

Siri kwenye kura mengine wazi? Lakini mshahara wa Pinda uwe wazi na kura Siri? Posho mlizokuwa mnadai zilikuwa hoja za wazi wazi kura Siri?

Kuna usemi usemao" two things that a man can not hide is when is in love and drunk" kwa hiyo ukiwa na mapenzi na chochote huwezi kujifisha hata ufanyaje!

Sioni mantiki ya kuwa na Siri!

Wale waleee!
Ivi CCM ni lini mtajiamini?
Hizi hila zenu zinahatarisha maisha ya watu!
Ivi kuna kura ya wazi kweli?
 
Back
Top Bottom