Mjumbe wa Baraza Kuu CUF ajiuzulu; Awatuhumu viongozi wake ( UKAWA Effect)

Juliana Shonza

Verified Member
Dec 19, 2012
2,009
2,000
Mjumbe wa Baraza Kuu na Katibu wa CUF wilaya ya Lindi ndugu Abubakar Taher amejiuzulu nyadhifa zake katika chama hicho kuanzia leo tarehe 21st May 2014, kwa kile alichokieleza kuchoshwa na ubabe na uvunjaji wa katiba unaofanywa na Mwenyekiti wake Ambae pia ni Mbunge wa Lindi Mjini Salum Barwany pamoja na uongozi wa Juu wa Chama hicho.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa mgogoro ndani ya Chama hicho hasa juu ya mwenendo wa Mwenyekiti huyo na viongozi wa Taifa wa Chama hicho. Miongoni mwa mambo ambayo Katibu huyo ameyataja ni pamoja na Uongozi wa Juu wa Chama hicho kupoteza muelekeo kwa kujiunga na Vyama vingine vya upinzani ambavyo tayari viliwatenga hapo kabla na kwamba kwa udhalilishaji na jeuri kubwa iliyoonyeshwa na viongozi wa Kambi ya upinzani bungeni haikuwa busara na ni kukosa msimamo na kujishushia hadhi kwa viongozi wakuu wa Chama hicho kuendelea kushirikiana na Chadema baada ya kejeli na udhalilishaji huo.

abuu.jpg katibu wa CUF Ndugu Abuubakar Taher aliyejiuzulu.


Tabia ya Viongozi wakuu wa Vyama vya upinzani kuhamishia na kujisahaulisha matatizo ya ndani ya vyama kwa kushirikiana na vyama vingine ambavyo navyo vinatumia mbinu ya muungano usio na Anuwani unaitwa UKAWA. Kwa tabia hii ya Viongozi wa juu wa Vyama vya siasa vya Upinzani kutumia UKAWA kama ngao ya kujihami na kujisahaulisha na Changamoto za ndani ya Vyama vyao itasababisha vyama hivyo kusambaratika kabisa.

Katika press yake aliyoifanya leo mjini Lindi Katibu huyo wa CUF ametamka kuwa "SIKU ZOTE KAZI YA UPINZANI NI KUKOSOA, KUKATAZA NA KUTOA SULUHISHO MBADALA NA BORA KATIKA KUSHUGHULIKIA MATATIZO NA CHANGAMOTO ZA MAENDELEO. LAKINI UPINZANI SASA UMEACHA KAZI YAKE, WAMEGEUKA VIBARAKA WA KUFANYA KAZI ZA MATAIFA YA NJE....."

Nami naungana na kauli yake hiyo kuwa UPINZANI wa nchi hii umeundwa na viongozi wajanja wajanja na watumia tumbo ambao hawaoni shida kuweka rehani amani ya Tanzania na hata kuhatarisha Utulivu na mshikamano tulionao kama Taifa, wanachochea ubaguzi, Udini, Ukabila na Utengano. Ni mabaya mno mawazo yao na dhamira zao.

Ni heri mtu UFE ila mawazo yako yawe hai (kama Mwalimu Nyerere) kuliko kuwa hai huku mawazo yako yamekufa (kama Mheshimiwa TUNDU)
 

duanzi

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
16,446
0
dr.slaa anaruka kwa helicopter, lipumba gari, mbatia toyo,, chadema wameanza kuwabagua cuf na nccr
 

bujash

JF-Expert Member
Aug 9, 2013
3,468
0
Wanaopigania Katiba walibaki bungeni kwenye bunge la katiba! Hawa UKAWA uroho wa Madaraka ndio umewasukuma kuunda huu umoja feki, usiokidhi viwango vya kisheria.

BP zitawapanda sana nyie mainterahamwe mwaka huu,UKAWA umewashika pabaya
 

duanzi

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
16,446
0
Lipumba ameisusa ukawa..pesa za wafadhili wa ukawa zimeliwa na mbowe na slaa
 

Gefu

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
6,944
1,500
...moto wa ukawa umewalamba mpaka wanaweweseka.na mamluki wote watajulikana tu...
 

bujash

JF-Expert Member
Aug 9, 2013
3,468
0
Kila mwenye wazo tofauti na ninyi ni mamluki. Huu ugonjwa CHADEMA ndio mmeuleta UKAWA.

Rasimu ya katiba iliyotokana na mawazo ya wananchi lazima iheshimiwe,porojo zenu peaneni hukohuko kwenye makambi yenu ya janjaweed na interahamwe.
 

Papizo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
4,700
2,000
UKAWA inawanyima usingizi vilaza wa CCM stu.pid na mpaka kieleweke.

Uchaguzi wa 2010 Chadema na CCM walishindina kwa % kidogo sanaaa sasa 2015 vyama vya upinzani kuungana CCM hamfikirii bado??

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

Juliana Shonza

Verified Member
Dec 19, 2012
2,009
2,000
tatizo la Vijana wa bavicha ni matusi.,chochote unachopost hapa wao hata kusoma hawasomi kazi kutukana tu. wanatumwa kutukana ili waandikiwe posho zao Ufipa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom