Mjumbe: Kauli ya rais kuhusu Muungano siyo sheria

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Tume ya Katiba jana ilizinduliwa rasmi na kukabidhiwa ofisi.

Akizungumzia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba Tume hiyo haiko kwa ajili ya kuvunja Muungano, mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo kutoka Zanzibar, Awadh Ali Said alisema hata kama maneno hayo yalizungumzwa na Rais, siyo kikwazo cha wananchi kukubali au kuukataa Muungano.

"Sisi tunakwenda kuwauliza wananchi, wao ndiyo watakaoamua kama wanautaka au hawautaki Muungano. Kama hawautaki tutaleta majibu hayo. Maneno hayo hata kama yamezungumzwa na Rais, siyo sheria, wananchi ndiyo watakaoamua," alisema Said.

Source Mwananchi.
 
Hakuna haja ya kuwa na katiba, kama wananchi hawajaulizwa kama wanataka Muungano au hapana. Uwepo au kutokuwa na muungano kutasaidi kupata uwanja mzuri wa kufikiria jinsi gani tutaishi,uhusiano wa Tanganyika na Zanziba nk. Kama Muungano hautajadiliwa, ninauhakika katiba hii mpya haitadumu na itakuwa ni upotevu wa hela.
 
Mwenyekiti wa Tume yeye anasemaje kuhusu suala la Muungano kujadiliwa na Tume?
 
Rais angekuwa na maamuzi juu ya katiba asingetuuliza, hiyo mipaka anayotuwekea haifai. Koti likubana unalivua na hulivai tena.
 
Hivi tunajadil kuwepo au kutokuwepo kwa muungano au katiba ya jamhuri ya muungano aw Tanzania. Katika hadidu za rejea ambazo ni sehemu ya sheria iliyoiunda Tume, hakuna popote ambako tume imepewa mandate ya kupigisha kura ya maoni lkuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Suala hapa siyo Rais amesema nini kuhusu muungano Bali sheria na hadidu za rejea zinaipa kazi gani tume..
 
MJADALA KUHUSU SUALA LA MUUNGANO WETU NI JAMBO AMBALO HALITAEPUKWA KUJADILIWA NA WATANZANIA WOTE. Kuna wanaoiona Zanzibar kama Mkoa wa Mara kwa udogo lkn hawafikiri kuwa Zanzibar iliungana na Tanganyika wakati tofauti hizo za ukubwa zinajulikana. Tukumbuke kuwa Zanzibar iliungana na Tanganyika kama nchi au taifa mbili huru kabisa. Kwa hiyo tusione kuwa wamependelewa. La sivyo.

Pengine suala hapa ni kuona aina ya muungano ambao utaridhiwa na pande zote mbili na ni mambo gani yaangaliwe kuwa ni mambo ya muungano. Kwa hili la muungano htutaepuka kuwa na serikali tatu: Muungano (Tanzania), Tanzania-Zanzibar na Tanzania Bara (Tanganyika).

Na mimi napendekeza mapema tu kuwa makao makuu ya Serikali ya Tanzania Bara (Tanganyika) ndio yatakuwa Dodoma; Tanzania-Zanzibar (Zanzibar) na Tanzania (Muungano) makao makuu yake ni Ikulu- Dar es Salaam. Hii ndi itakuwa dawa pekee ya kuihamisha serikali ya Tanganyika Dodoma maana hawatakaa Dar kwa kuwa ofisi zake zitakuwa Dodoma. Huu muungano tulionao hatuuelewi maana kila mtu analalamika na vizazi vijavyo vitaendelea kulalamika maana hta waliokuwepo wakati wa muungano hawauelewi na hawaachi kulalamika. Dawa ni kuwa na muungano unaoeleweka ambao ni wa serikali Tatu.


Na tutayaainisha mambo yapi yashughulikiwe na serikali ya muungano na yapi ya serikali zingine 2. Hatuwezi kuwa wa2 wa kulalamika milele, lazima tufanye jambo amblo ni kumbukumbu kwa vizazi. Walioleta muungano wa serikali 2 walikuwa n utashi wao kwa wao na walielewana. Je, ni wangapi tunaoelewana ktk hili la muungano? Ni kila mtu kulalamika tu eti Zanzibar inapendelewa; kwani nani kasema Zanzibar iliomba ndoa ya mkeka na Tanganyika. Kuna nchi ndogo kuliko hata zanzibar na uuru wao walipigania wenyewe hata kama walitumia marungu na mapanga. Tuwaache.


Tatizo sisi wa bara, tunadhani ukubwa wa pua ni kuwa na makamasi mengi: Sivyo. Hebu; tujaribu kujali haki ya Zanzibar kuwa ni Taifa lililokuwa huru ambalo kwa ridhaa yake iliungana na Tanganyika yetu. Sasa nini hapo? Tanganyika ilibakwa na Zanzibar kuungana au lenyewe liliona umuhimu wa kuungana.


Wengine wanasema eti iweje wajumbe wa tume ya katiba wawe uwiano (idadi) sawa Zanzibar na Bara. Tuache masihara hayo. Zanzibar haikuwa mkoa wa bara bali ilikuwa Taifa huru kama lilivyokuwa Tanganyika. Na kama kuna jambo la kujadiliwa linalohusu muungano lazima idadi sawa ya wajumbe wakae meza moja kujadili na huwahusisha Watz wote ndio maana ya kuunda tume ya katiba.

Sasa inavyoonekana bara tunataka kubaka haki ya Wazanzibari eti kwa kigezo cha udogo wa eneo la nchi.
 
Back
Top Bottom