Mjulisheni Magufuli, siasa za kupambana na dunia anazozijaribu hapa zimeshindikana Zimbabwe

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
Zimbabwe wamesalimu amri rasmi, sasa wanarudisha mashamba ya Wazungu waliyoyanyang'anya Miaka 20 iliyopita.

So Mjulisheni Magufuli kuwa anachokijaribu hapa wenzake wamekijaribu na kimewashinda, mjulisheni maana haya mambo ya Kimataifa huwa yanampita hana habari; Kabudi naye yupo kakodoa Macho tu.

Kujaribu kupambana na dunia ni kuchuma janga tu ambalo wengine hatuwezi kukubaliana naye.
 
Ni sisi Waafrika tu ndio tunapenda kuishi kama kunguru na kupapatikia wazungu.

Wazungu wakilinda interest za nchi zao wanaitwa wazalendo sisi tunaitana madikteta .

Trump anapambana na China kuhakikisha haijinufaishi kupitiliza na marekani.

Russia, UK kwenye EU , list ni ndefu.

Tujifunze kuhakikisha kuwa tunanufaika na Rasilimali zetu, tuache woga.
 
Itakuwa ajabu kwenu bavicha kulinganisha akiri ya magufuri na watoto tindu,
Yile kicha kimesimama na ndio maana hata hao amabao mnataka wamusurubu wanashindwa waanzie wapi?
Mnazuia mikopo lakini anapewa, mnaomba nchi isipate misaada bali wao wanatoa, sasa mmebaki na ngonjera tu.
 
Avatar yako tu inaonekana haiwezi mtakia mema Magufuli
Watu wanaongelea nchi wewe unamwongelea mtu.Kwani uyo magu ata akitakiwa mema atakaa milele.swala hapa ni nchi ambayo itaendelea kuwepo hata baada kikazi chetu kupita.Mugabe leo hayupo je anajua yanayoendelea zimbw.Kwahiyo jambo linaloweza kufanyika leo bila weledi wakutosha linaweza kuja kusumbua wajukuu zetu kesho.
 
Tatizo sio maguful,,tatizo ni sisi watanzania wengi wetu ni wanafik,wajinga na hatujitambui ndio maana watawala wanaweza tufanya watakacho bila kupingwa .
Nipo nawewe msitali wa mbele.

Wenzetu wanamawazo kuwa Tanzania ni ya kwao.
 
Hii yote ni kwanini?
Vipaumbele vya watawala sio Vipaumbele vya wananchi.
Ndio maana sasa maccm wakiongozwa na Meko wanafoka jukwaani. Wananchi wanataka maji unanunua ndege, wao wanataka hospitali unajenga flaiova, wao wanataka shule unajenga SGR fupi.

Vipaumbele vya watawala sio Vipaumbele vya wananchi.
Maccm badilikeni
 
Jiwe anajivunia kiswahili. Hoja za wazungu si anazijibu kiswahili hawamuelewi....ajaribu kwa kimombo wamsikie aone
 
Tujifunze kuhakikisha kuwa tunanufaika na Rasilimali zetu, tuache woga
Bado sijaelewa mantiki yako ila niseme kitu, waafrika bado tunatakiwa kuwa chini ya hao hao waliokuwepo kabla ya sisi kujitambua.
 
Ni sisi waafrika tu ndio tunapenda kuishi kama kunguru na kupapatikia wazungu.

Wazungu wakilinda interest za nchi zao wanaitwa wazalendo sisi tunaitana madikteta .

Trump anapambana na China kuhakikisha haijinufaishi kupitiliza na marekani.

Russia, UK kwenye EU , list ni ndefu.

Tujifunze kuhakikisha kuwa tunanufaika na Rasilimali zetu, tuache woga.

Asante Keyboard warrior mwenzangu. Hizo rasimali zinatunufaisha vipi wakti mikataba ni siri.

Mwenyekiti wangu Magufuli kajitahidi pakubwa sana, lakini bado hatujaweza kuwakaba wawekezaji wakubwa kwa sababu ya miktaba ya iliyosainiwa na wachache. Hapa ndipo ninapomuona Lissu ni shujaa wa taifa hili kutaka mabadiliko hasa kwenye jinsi tunavyoingia mikataba ya siri isiyo na maslahi kwa taifa.

Tukitaka tuanze kufurahia rasimali zetu, basi tuanze na katiba, mikataba na kujenga taasisi imara ambazo zitasimama kuwajibishana na kuwawajibisha wapiga dili (sasa hivi tuna wapi dili wa kiwango cha lami, first class yaani ni grade A+ and pure scammers). Then tuje kwenye elimu, tuifumue mitaala yetu ituondolee jangaa la kumeza nondo na madesa zenye misingi ya kikoloni na ubeberu mambo leo. Elimu ikiwa safi tutakuwa na watu wa kukinzana na sera onevu za mabeberu na jinsi kucheza na soko
 
Itakuwa ajabu kwenu bavicha kulinganisha akiri ya magufuri na watoto tindu,
Yile kicha kimesimama na ndio maana hata hao amabao mnataka wamusurubu wanashindwa waanzie wapi?
Mnazuia mikopo lakini anapewa, mnaomba nchi isipate misaada bali wao wanatoa, sasa mmebaki na ngonjera tu.
Mabeberu sio ??
 
Zimbabwe Sasa wanahaha kujaribu kuwarudisha wale wakulima wazungu (CCM mabeberu) ili wananchi wajitosheleze kwa chakula Kama zamani. Bahati mbaya sana wakulima walinyang'anywa mashamba na vyote vilivyokuwemo na kukabithiwa wananchi ambao hawakuwa wakulima kwa hiyo mashamba yakaharibika kabisa.

Wazungu wanaweza wakakubali kurudi maana ni raia lakini lazima watataka walipwe fidia kwa mali zao zilizopotea jambo ambalo litakuwa gumu sana kwa Serikali kwa sababu hali yake ya uchumi bado ni mbaya sana. Pili, kwa sababu ya umahili wao katika kilimo, nchi nyingi za Afrika ziliwakaribisha kwa mikono miwili na kuwapa ardhi walime na wako huko wanalima kuinua uchumi wa nchi zilizowakaribisha.

Rais wetu mpendwa akitokea Kusini alisimama Harare na kukaribishwa vizuri na mwenyeji wake Rais wa huko na wananchi wake lakini akachafua hali ya hewa alipoanza kumsifia mwenyeji wake jambo lililowauthi sana wananchi ikabidi akimbie baada ya kutukanwa.

Zimbabwe walikuwa na shida kubwa ya chakula ikabidi Rais wa kule amwombe Rais wetu amuuzie mahindi ambayo angeweza kupata karibu toka Zambia au Malawi yaliyolimwa na wazungu raia wa Zimbabwe.

Hapa Kuna somo kwa Marais wote wawili; Wa kwetu mazoea ya kusifiwa hata kwa ujinga anapeleka kule ilimgharimu chuki ya raia wa kule wakamtukana; Rais wa kule badala ya kupata chakula karibu ikabidi apate toka Arusha mbali kwa gharama kubwa.
 
Back
Top Bottom