Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Leo nimekutana na Bibi kizee anaweza kuwa na miaka kati ya 85-90 kaniambia hivi kwa lugha ya kisukuma, "kijana Wangu Mhere Mwita Mimi nimezeeka niona Mengi sana nimeona jua likichanua nimeona jua likizama nimeona kiangazi nimeona masika nimeona ukame nimeona mafuliko Kijana Wangu ninaomba Mikono yako niitemee mate"
Nikamwambia ; "sawa Bibi" nikampa mikono Akatema mate akasema maneno haya kwenye mikono yangu "nimeona nyota njema kwako utaitwa mfalme, Watu watasimama pembeni kukuona ukipita usiwadharau simama uwape mikono, mjukuu Wangu na baya lolote lisikupate lirudi kwa hao waliletao uishi miaka kama yangu kwa Neema ya Mungu".
Alipomaliza kuongea Mimi nikachukua mikono yangu nikapaka mate yake usoni kwangu ili nionyesha unyenyekevu na heshima kwake. Bibi akaenda zake.
Ninaomba niwaulize Bibi ameona Nyota Ya nini inakuja kwangu. Na je nilikosea kufuta mate yake usoni kwake.