Mjukuu wa Mandela atoa wito wa kufungwa ubalozi wa Israel nchini Afrika Kusini

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
6,026
2,000
Mjukuu wa Mandela atoa wito wa kufungwa ubalozi wa Israel nchini Afrika Kusini

May 13, 2021 13:33 UTC

[https://media]

Maelfu ya raia wa Afrika Kusini vikiwemo vyama na baadhi ya watu muhimu na mashuhuri wamefanya maandamano na kukusanyika katika maeneo mbalimbali muhimu kama mbele ya Bunge na kutoa wito wa kususiwa utawala haramu wa Israel.

Miji muhimu ya Afrika Kusini jana ilishuhudia maandamano na mikusanyiko ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina ambapo waandamanaji walitangaza pia chuki na upinzani wao wa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina.

Waandamanaji mjini Cape Town walifanya maandamano na kuelekea upande wa jengo la Bunge nchini humo huku wakipiga nara za kuwaunga mkono wananchi wa Palestina. Mjukuu wa shujaa wa mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Mandla Mandela aliyeshiriki katika maandamano hayo ametoa wito wa kufungwa ubalozi wa utawala haramu wa Israel nchini humo.

[https://media]Maandamano ya wananchi wa Afrika Kusini ya kuunga mkono wananchi wa PalestinaMjukuu huyo wa Mandela amesema, licha ya Israel kuwauwa kinyama watoto wa Kipalestina lakini ulimwengu umeendelea kunyamaza kimya. Aidha amesema, wakati linapozungumziwa suala la Palestina, sisi tukiwa Waafrika Kusini tuna umoja na tunapaza sauti moja kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.

Siku ya Jumanne pia, watu wasiopungua 300 walikusanyika mbele ya ubalozi wa utawala dhalimu wa Israel nchini Afrika Kusini na kutoa wito wa kususiwa utawala huo ghasibu unaoendelea kutenda mauaji kila uchao dhidi ya Wapalestina kwa uungaji mkono wa Marekani na madola ya Magharibi.

4by17a8a7156491vec1_800C450.jpeg
4by1730d4e6f7d1vec3_800C450.jpeg
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,783
2,000
Yeyote anayedhani kukemea udhalimu wa kutisha unaofanywa na Israel Taifa la wauaji dhidi ya Wapalestina ni lazima uwe muislamu ana ufinyu mkubwa wa akili.
Na ndiyo south waisilamu wachache lakini wameandamana. Huku sasa!!! Waisilamu ni wengi kuliko manaswara lakini hakuna aliethubutu kutia neno la "maandamano" tumebakia kusikitika kwenye mitandao.
 
Nguseroh

JF-Expert Member
Jan 18, 2020
1,864
2,000
Na ndiyo south waisilamu wachache lakini wameandamana. Huku sasa!!! Waisilamu ni wengi kuliko manaswara lakini hakuna aliethubutu kutia neno la "maandamano" tumebakia kusikitika kwenye mitandao.
mimi nawasifu wa hapa hawajaandamana kwasababu wangeandamana wangeonekana wanafki kwasababu ISIS na Alshabab wanachinja Waislamu wenzao waafrika lakini hata tamko la kulaani hamna
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
9,087
2,000
Kwani muisrael akiwaacha wapalestina atapungukiwa nini?
Lengo kuu la Israel wanataka eneo lote la Palestina liunganishwe na Israel liwe Taifa moja, baadae watafute mbinu za kuwafukuza wapalestina wote na kuwaleta Wayahudi kutoka Ulaya,Amerika,Asia na Latin America kuja kuishi Israel iliyo panuka baada ya ku-annex taifa la Kipalestina.
 
let the caged bird sings

JF-Expert Member
Sep 19, 2020
423
1,000
Na ndiyo south waisilamu wachache lakini wameandamana. Huku sasa!!! Waisilamu ni wengi kuliko manaswara lakini hakuna aliethubutu kutia neno la "maandamano" tumebakia kusikitika kwenye mitandao.
We jamaa Jinga na linafiki likubwa, wengi mnao pinga dhuluma ya muisrael dhid ya parestina mko kidini zaid na sio humanity kama mnavyopretend hapa..

Kifo ni halali kwa asiye muislam, akiwa muislam ni jinai..

Kile kilichomo mioyoni mwenu dhidi ya wasio waislam ni kikubwa zaidi kuliko mnachokiandika hapa.
Bahati nzuri mmeiteka dunia kwa propaganda na kutafuta HURUMA, MTASHINDA ILI MAANDIKO YATIMIE.
IMG_20210514_080342.jpg
 
let the caged bird sings

JF-Expert Member
Sep 19, 2020
423
1,000
Yeyote anayedhani kukemea udhalimu wa kutisha unaofanywa na Israel Taifa la wauaji dhidi ya Wapalestina ni lazima uwe muislamu ana ufinyu mkubwa wa akili.
Usisahau na wengi wanaopinga dhuluma hiyo wapo kidini zaidi na sio humanity..
SAGA la jamhuri ya kati hao hao wanaopinga komenti zao zilikuwa tofauti.
Sikuchagulii upande wa kusimama, ila hii vita ipo kidini zaidi.

Haya chini ni maoni ya member mmoja anaepinga uovu wa Israeli, lakini ndani ya mapafu yake ana chuki nyingine.

IMG_20210514_080342.jpg
 
let the caged bird sings

JF-Expert Member
Sep 19, 2020
423
1,000
mimi nawasifu wa hapa hawajaandamana kwasababu wangeandamana wangeonekana wanafki kwasababu ISIS na Alshabab wanachinja Waislamu wenzao waafrika lakini hata tamko la kulaani hamna
Hawana lolote hao... Ajabu macho yao hayaoini vilivyo karibu, vya mbali wanaviona...
Msumbiji ipo usoni kwao, ila hawana taarifa na kinachoendelea
 
Msweden

JF-Expert Member
Nov 3, 2020
402
1,000
Na ndiyo south waisilamu wachache lakini wameandamana. Huku sasa!!! Waisilamu ni wengi kuliko manaswara lakini hakuna aliethubutu kutia neno la "maandamano" tumebakia kusikitika kwenye mitandao.
Mmewahi kutia neno kuhusu boko haramu kuteka mabinti 300?
Msumbiji je?
Mauaji ya garisa yaliyofanywa na al shabab?
Nyinyi mnashindwa kupaza sauti kwa wa africa wenzenu mnataka kupaza sauti kwa waarabu
 
maddox

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
389
1,000
Mjukuu wa Mandela atoa wito wa kufungwa ubalozi wa Israel nchini Afrika Kusini

May 13, 2021 13:33 UTC

[https://media]

Maelfu ya raia wa Afrika Kusini vikiwemo vyama na baadhi ya watu muhimu na mashuhuri wamefanya maandamano na kukusanyika katika maeneo mbalimbali muhimu kama mbele ya Bunge na kutoa wito wa kususiwa utawala haramu wa Israel.

Miji muhimu ya Afrika Kusini jana ilishuhudia maandamano na mikusanyiko ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina ambapo waandamanaji walitangaza pia chuki na upinzani wao wa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina.

Waandamanaji mjini Cape Town walifanya maandamano na kuelekea upande wa jengo la Bunge nchini humo huku wakipiga nara za kuwaunga mkono wananchi wa Palestina. Mjukuu wa shujaa wa mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Mandla Mandela aliyeshiriki katika maandamano hayo ametoa wito wa kufungwa ubalozi wa utawala haramu wa Israel nchini humo.

[https://media]Maandamano ya wananchi wa Afrika Kusini ya kuunga mkono wananchi wa PalestinaMjukuu huyo wa Mandela amesema, licha ya Israel kuwauwa kinyama watoto wa Kipalestina lakini ulimwengu umeendelea kunyamaza kimya. Aidha amesema, wakati linapozungumziwa suala la Palestina, sisi tukiwa Waafrika Kusini tuna umoja na tunapaza sauti moja kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.

Siku ya Jumanne pia, watu wasiopungua 300 walikusanyika mbele ya ubalozi wa utawala dhalimu wa Israel nchini Afrika Kusini na kutoa wito wa kususiwa utawala huo ghasibu unaoendelea kutenda mauaji kila uchao dhidi ya Wapalestina kwa uungaji mkono wa Marekani na madola ya Magharibi.

View attachment 1783811 View attachment 1783812
Mtoto WA Mandela ndio Nani kwani?? Mpaka israel istuke????
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,783
2,000
Una ufinyu mkubwa sana wa akili kwa kudhani vita hii ipo kidini. Fungua akili yako zaidi ili uelewe kiini cha vita hii.

Usisahau na wengi wanaopinga dhuluma hiyo wapo kidini zaidi na sio humanity..
SAGA la jamhuri ya kati hao hao wanaopinga komenti zao zilikuwa tofauti.
Sikuchagulii upande wa kusimama, ila hii vita ipo kidini zaidi.

Haya chini ni maoni ya member mmoja anaepinga uovu wa Israeli, lakini ndani ya mapafu yake ana chuki nyingine.

View attachment 1784053
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom