Mjue Yoabu - Jenerali Mkuu wa Mfalme Daudi, Katili na asiyeogopa chochote!

Ila hata daudi chuma aisee wakati wake akiwa mpiganaji b4 ufalme nae alitisha vitani ukisoma kitabu cha swamweli!!!
kweli mkuu,Daudi alikua na roho wa MUNGU lakini alikua na displine sana aisee...Nakumbuka wakati anataka kwenda kumuua yule tajiri aliekua anamchungia kondoo zake wakiwa nyikani mke wa tajiri alitoka fasta na kumbembeleza asimuue mumewe,Daudi akamsamehe akaondoka,Nakuhakikishia mkuu Yoabu hana busara hizo angeanza ua mke wafanyakazi kila kitu,kuna Mji Yoabu aliingia hakuacha hata Kuku
 
Ukioata muda tafadhali san shusha ndefu ya namna hii juu ya Mfalme Nebukadreza. Isiwe fupi. Iwe ndefu kuanzia asili yake, utawala wake, maadui zake mpaka kuangukankwake!

Pia ukipatavkibali machoni pa Bwana utupie pia juu ya SAMWELI
 
Mkuu usijali, Ya Samweli iko very interesting...nitaileta lakini kabla ya hapo nitaishusha ya yule mbabe mfalme wa aina yake...Daudi mwana wa Yese...Mfalme Daudi
 
Katika watu makatili na wakorofi katika Biblia,Yoabu anaweza kukufanya ukamwona kama mwehu,Lakini Alishinda karibu vita vyote katika utawala wa Miaka 40 wa Mfalme Daudi Huko Israel na Yuda Akiwa kama Kamanda Mkuu.

Yoabu Alikua pia Mjanja Kisiasa akimwacha kwa mbali mfalme daudi,na akikwepa Adhabu nyingi mno ziwe zimetolewa na MUNGU mwenyewe au Mfalme Mwenyewe,alisababisha Machungu mengi Mno kwa Watu wengi maadui wa Israel,Huku pia Akileta Tafrani ya Aina yake ndani Ya Israel,Hayo yote Mfalme Daudi Aliyaona,na Aliyavumilia hadi Mwisho...Yoabu Alipokua ameanza uzee...

Yoab alikua Mtoto wa Seruya,Dada wa Kambo wa Mfalme daudi,kwa hiyo alikua akimwita Mfalme Mdaudi Mjomba,Seruya (Zeruiah) Alikua mtoto wa nje wa Mzee Yese,Baba Yake Daudi,Kwa hiyo walikua ni ndugu wa Damu kabisa,na kiukweli Yoabu Hukumbukwa kwa damu nyingi Alizomwaga.

Wakati Utawala wa Mfalme Sauli ulipoanguka,Mtoto wake Isbosheth bado alikua akitawala upande wa kaskazini wa Israel,Huku Daudi akitawala YUDA iliyokua upande wa kusini,Abner mwana wa Neri aliekuwa Jemedari wa Mfalme Sauli alikua ndio Kamanda wa Majeshi ya Isbosheth.

Majeshi ya Isbosheth yakiongozwa na Abner Mwana wa Neri yalikutana na Yale ya Daudi Yakiongozwa na Yoabu,Vita vikawa vikali sana na Majeshi ya Isbosheth yakakimbia mbele ya yale ya Daudi,Lakini Wakati Abneri Kamanda wa Isbosheth akitoroka,Asahel Mdogo wake Yoab wa mwisho,ambae nae alikua mwanajeshi alimkimbiza, Abner alijaribu kumsihi bwana mdogo asimkimbize kwani alikua anajua kabisa yule ni mdogo wake Yoabu na alijua madhara ya kumwua,lakini asaheli aliendele hata baada ya kuonywa mara tatu,mwisho Ikabidi Abneri amchome mkuki tumboni na Kumwua, ukaibuka uhasama mkubwa sana kati ya tawala mbili za Israel.

Mfalme daudi Hakuipenda hali ile ikabidi wakutane kufanya mapatanisho,baada ya Mapatanisho kati ya Abner na Yoab na mfalme daudi na isbosheth,wakati Abner anatoka ikulu Yoab akamwita pembeni kidogo kama anataka kuongea nae,akamchoma tumboni na kumwua hapo hapo,Mfalme Daudi Alilia sana,Akafunga na Kulaani mno mauaji yale na kusema yeye hausiki ila Yoabu, lakini hakumfanya kitu, ikumbukwe daudi na Abner walipigana vita nyingi wakiwa chini ya mfalme Saul, na Daudi Akimheshimu sana Abner Lakini Yoab Hakujali Akamwua tena Baada ya Wote Kupatanishwa.

Mfalme Daudi alipomwona Bathsheba akioga mtoni,Daudi akiwa ghorofani kwake Ikulu alituma watu wakamwita akalala nae,huku akijua ni mke wa Uriah,Askari wake aliyeko Vitani,akampa mimba, Daudi akaona ambambikie uriah Mimba,Akamwita kutoka vitani akamwambia akapumzike nyumbani,kumbe Uriah hakwenda Nyumbani,akalala na walinzi wa Ikulu, Daudi akamwona asubuhi na kumwakia wewe mbona hukwenda nyumbani,uriah akamwambia hata iweje hataenda Nyumbani kulala na mkewe wakati wenzake wako vitani,usiku wake dadui akaandaa sherehe na kuwaagiza wahudumu wampe jamaa pombe ya kutosha,jamaa pombe akanywa akalewa mno na nyumbani hakwenda,Mfalme akaona hapa naumbuka,Akampa Uriah Barua kwamba Ampelekee Kamanda wake Yoabu kule Vitani,Kumbe kamwandikia Yoabu kuwa Amweke Uriah mbele kwenye mapigano makali ili afe,na kweli uriah akafa,Daudi akamwoa Mkewe,ila Daudi alipata adhabu za kutosha,ikiwemo watoto wake kuuana, mtoto mwingine kuzaliwa na kufa, na kupinduliwa na mtoto mkubwa na kukimbilia mafichoni,hii ilikua adhabu ya MUNGU kwa sababu Ya kumuua Uriah...Hii nayo Yoabu Akakwepa Adhabu.

Yoab Alikua Anajua namna ya kujikomba Kwa Mfalme,Kuna Siku Aliupiga Mji Mmoja na Kuushinda, Kisha Akamtumia Mfalme Daudi Ujumbe na kumwambia,Njoo Uingie Ndani Y Mji Ukautwae nisije Nikaingia mimi,Ukaitwa Jina langu,yaani vita zote Akishashinda ndo mfalme anaitwa kuja kumalizia aonekane na yeye ni Shujaa.

Mfalme Daudi Akapata Tamaa Ya Kuhesabu Watu, kinyume na Matakwa ya MUNGU,maana Aliwaambia yupo pamoja nao,wasije kujihesabu wapo wangapi,Yoabu akamshauri mfalme Daudi kwamba sio wazo zuri na aachane nalo,litaamsha Hasira ya MUNGU,lakini Mfalme akatoa Amri ya Mfalme,Yoabu ikabidi ahesabu watu..MUNGU akakasirika mno,na kumuadhibu daudi ila YOABU hiyo akaikwepa pia.

Mtoto Mkorofi wa Mfalme Daudi,Absalom, akakatiza anga za Yoabu,kwanza Absalomu akamwua ndugu yake Amnoni mtoto wa Mfalme Daudi kwa mama Mwingine,Kisa alimbaka dada yake Tamari, Mfalme Daudi hakumfanya kitu Absalomu,Yoabu alikasirika mno akaiweka rohoni,Absalomu akakimbia mbele ya baba yake,ila Yoabu kwa hila zake akambembeleza mfalme na kumwombea Absalomu msamaha mpaka akarudi kutoka mafichoni
Absalom akaenda mbali zaidi,akaunda jeshi,Akampindua baba yake Ghafla,ikabidi baba yake akimbilie Milimani,Yoabu akakusanya jeshi fasta akafanya vita na Absalomu,Lakini wakati anaenda vitani,Mfalme Daudi akasema Kabisa,Naombeni msimuue wala kumtenda Vibaya mwanangu Absalomu,Yoabu akamvamia Absalomu kama Upepo wa kisulisuli akalisambaratisha jeshi lake na Absalomu akatoroka lakini akakwama kwenye miti ya mialoni,Maafisa wengine wote wakakataa kumuua Absalomu,Yoabu akaenda akamchoma na Kumuua Mtoto wa Mfalme kisha akamzika kwenye lishimo huko huko porini,bila hata ya heshima yoyote,pamoja na kumwombea kwa baba yake alipokimbia bado hakusita Kumuua bila huruma.

Mfalme Daudi akalia na kuomboleza kwa Ajili ya mwanae,na israel yote ikalia nae nae,na wanajeshi,Yoabu Akamfata Mfalme akamwambia Badala Utoke nje uwaambie watu leo tumeshinda ndo unawavunja moyo kwa maana adui yako kafa na wewe unaomboleza sasa walienda vitani kufanya nini? ikabidi mfalme ajifute machozi ajikaze na kushangilia kwamba wameshinda Vita,ushauri wa Yoabu ukapita ila Mfalme akawa kamchoka kwa uovu wake.

Akamshusha Yoabu cheo,na Kumpandisha Amasa Kuwa Jenerali wa Jeshi,wakiwa vitani Yoabu akamwita Amasa Amkumbatie, kwa Amani,Amasa alivyosogea tu,Yoabu akamchoma tumbomboni na jambia hadi akafa,wakati Amasa anatoka damu na kukata Roho,Yoabu akaongoza majeshi kwenda kwenye vita zote Mfalme daudi alizompangia Amasa,na akashinda zote akarudi kama Jemedari na jenerali Mkuu,what a Villain?

Mfalme Daudi Alipokua mzee,na Yupo kitandani,Mtoto wake Adoniyah alijitangaza Mfalme kinyume na matakwa Ya mfalme Daudi, Mfalme Daudi Akamtawaza Solomoni awe Mfalme Badala yake,wakati huo Yoabu alikua Ameungana na Adoniyah,Aliposikia Solomoni kawa Mfalme alitetemeka Mno,Na Mfalme Daudi alimwambia Solomoni Mambo yote Yoabu Aliyoyafanya,Akimwambia wewe Una Busara,utajua Cha kumfanya, usiache Mvi zake zikashuka kaburini kwa Amani, Yoabu Akakimbilia Madhabahuni na kushika pembe ya Madhabahu,Mfalme Solomoni Akamtuma Kamanda wake mkuu Benaya mwana wa yehodaya, na kumpa Amri amwulie hapo hapo Madhabahuni,kisha wakamzika nyikani...yaani porini...na huo ndo ukawa mwisho wa ubabe wake.

My Take: Yoabu Alikua Katili sana,nakumbuka nilisoma mahali mfalme wa edom anaitwa Hadadi alikimbilia misri hadi aliposikia Yoabu amekufa,Mfalme Daudi alikua anamwogopa Yoabu,na inasemekana kama sio undugu wao hakuna ambae angeweza kumzuia Yoabu asiwe Mfalme Israel,ndio maana alijitaftia position anayoitaka japokua alikua na kaka yake Abishai ambae alikua mwanajeshi na rafiki wa Mfalme,Pamoja na Hayo bado Yoabu alishinda vita nyingi akiwa mtu katili na akicha kumbukumbu mbaya kwa maadui wa mfalme,akipiga kila utawala adui wa mfalme daudi na kumletea mali nyingi mno na milki kubwa sana,cha kushangaza alikua mtiifu kwa daudi na mkatili kwa wakati mmoja,huku akiamua mambo yake anayafanya,iwe mfalme anataka au la.

Alilinda nafasi yake ya jemedari kwa Ncha ya upanga,Alimwua Abner kwa Kisa cha ndugu yake Asahel lakini wachambuzi wanasema ilikua ni hofu ya nafasi yake kuchukuliwa na Abneri na hii ilidhihirika alipomwua pia Amasa.

Huyo Ndio Yoabu bin Seruyah au yoav bin zeruiah....nakaribisha maswali maoni na pia marekebisho nilipokosea...
Sasa pamoja na ujanja wote na ushujaa wa Yoabu ilikua je Suleiman akamuua kama kuku?
 
Mh atakwepaje adhabu ya Mungu ilihali Mungu anakujua kabla,na baada ya kuzaliwa hadi kufa kwako.....

Je! Ata mimi naweza nikakwepa adhabu za Mungu ilihali nimekosa mbele zake
Ndio mkuu unaweza kuikwepa adhabu yake kupitia 'kujidhabihu' mbele zake kupitia TOBA ya kweli.
 
Mkuu umekufuru, je kuna mtu awaye yote awezaye kukwepa adhabu ya Mungu?
Hapana hajakufuru ni kweli kabisa hata wewe unaweza ukaikwepa adhabu ya Mungu kupitia TOBA ya kweli mara kwa mara pindi umkoseapo Bwana Mungu.
 
Asante sana na hongera kwa thread nzuri sana. Mimi ni mjinga kwenye baadhi ya mambo ya biblia. Naomba nifafanuliwe kiasi ili nielewe, hivi Israel raia wake wote walitekwa wakapelekwa misri na nchi ikabaki tupu na ndipo baadae sana chini ya Nabii Musa ndio wakarudi au ilikuwaje??
Duuh kweli kiazi kimeiva
 
Mungu wa wayahudi anaua mpaka Leo watu wasio na hatia. Huyo jamaa kama Luca brass kwenye the godfather
 
Katika watu makatili na wakorofi katika Biblia,Yoabu anaweza kukufanya ukamwona kama mwehu,Lakini Alishinda karibu vita vyote katika utawala wa Miaka 40 wa Mfalme Daudi Huko Israel na Yuda Akiwa kama Kamanda Mkuu.

Yoabu Alikua pia Mjanja Kisiasa akimwacha kwa mbali mfalme daudi,na akikwepa Adhabu nyingi mno ziwe zimetolewa na MUNGU mwenyewe au Mfalme Mwenyewe,alisababisha Machungu mengi Mno kwa Watu wengi maadui wa Israel,Huku pia Akileta Tafrani ya Aina yake ndani Ya Israel,Hayo yote Mfalme Daudi Aliyaona,na Aliyavumilia hadi Mwisho...Yoabu Alipokua ameanza uzee...

Yoab alikua Mtoto wa Seruya,Dada wa Kambo wa Mfalme daudi,kwa hiyo alikua akimwita Mfalme Mdaudi Mjomba,Seruya (Zeruiah) Alikua mtoto wa nje wa Mzee Yese,Baba Yake Daudi,Kwa hiyo walikua ni ndugu wa Damu kabisa,na kiukweli Yoabu Hukumbukwa kwa damu nyingi Alizomwaga.

Wakati Utawala wa Mfalme Sauli ulipoanguka,Mtoto wake Isbosheth bado alikua akitawala upande wa kaskazini wa Israel,Huku Daudi akitawala YUDA iliyokua upande wa kusini,Abner mwana wa Neri aliekuwa Jemedari wa Mfalme Sauli alikua ndio Kamanda wa Majeshi ya Isbosheth.

Majeshi ya Isbosheth yakiongozwa na Abner Mwana wa Neri yalikutana na Yale ya Daudi Yakiongozwa na Yoabu,Vita vikawa vikali sana na Majeshi ya Isbosheth yakakimbia mbele ya yale ya Daudi,Lakini Wakati Abneri Kamanda wa Isbosheth akitoroka,Asahel Mdogo wake Yoab wa mwisho,ambae nae alikua mwanajeshi alimkimbiza, Abner alijaribu kumsihi bwana mdogo asimkimbize kwani alikua anajua kabisa yule ni mdogo wake Yoabu na alijua madhara ya kumwua,lakini asaheli aliendele hata baada ya kuonywa mara tatu,mwisho Ikabidi Abneri amchome mkuki tumboni na Kumwua, ukaibuka uhasama mkubwa sana kati ya tawala mbili za Israel.

Mfalme daudi Hakuipenda hali ile ikabidi wakutane kufanya mapatanisho,baada ya Mapatanisho kati ya Abner na Yoab na mfalme daudi na isbosheth,wakati Abner anatoka ikulu Yoab akamwita pembeni kidogo kama anataka kuongea nae,akamchoma tumboni na kumwua hapo hapo,Mfalme Daudi Alilia sana,Akafunga na Kulaani mno mauaji yale na kusema yeye hausiki ila Yoabu, lakini hakumfanya kitu, ikumbukwe daudi na Abner walipigana vita nyingi wakiwa chini ya mfalme Saul, na Daudi Akimheshimu sana Abner Lakini Yoab Hakujali Akamwua tena Baada ya Wote Kupatanishwa.

Mfalme Daudi alipomwona Bathsheba akioga mtoni,Daudi akiwa ghorofani kwake Ikulu alituma watu wakamwita akalala nae,huku akijua ni mke wa Uriah,Askari wake aliyeko Vitani,akampa mimba, Daudi akaona ambambikie uriah Mimba,Akamwita kutoka vitani akamwambia akapumzike nyumbani,kumbe Uriah hakwenda Nyumbani,akalala na walinzi wa Ikulu, Daudi akamwona asubuhi na kumwakia wewe mbona hukwenda nyumbani,uriah akamwambia hata iweje hataenda Nyumbani kulala na mkewe wakati wenzake wako vitani,usiku wake dadui akaandaa sherehe na kuwaagiza wahudumu wampe jamaa pombe ya kutosha,jamaa pombe akanywa akalewa mno na nyumbani hakwenda,Mfalme akaona hapa naumbuka,Akampa Uriah Barua kwamba Ampelekee Kamanda wake Yoabu kule Vitani,Kumbe kamwandikia Yoabu kuwa Amweke Uriah mbele kwenye mapigano makali ili afe,na kweli uriah akafa,Daudi akamwoa Mkewe,ila Daudi alipata adhabu za kutosha,ikiwemo watoto wake kuuana, mtoto mwingine kuzaliwa na kufa, na kupinduliwa na mtoto mkubwa na kukimbilia mafichoni,hii ilikua adhabu ya MUNGU kwa sababu Ya kumuua Uriah...Hii nayo Yoabu Akakwepa Adhabu.

Yoab Alikua Anajua namna ya kujikomba Kwa Mfalme,Kuna Siku Aliupiga Mji Mmoja na Kuushinda, Kisha Akamtumia Mfalme Daudi Ujumbe na kumwambia,Njoo Uingie Ndani Y Mji Ukautwae nisije Nikaingia mimi,Ukaitwa Jina langu,yaani vita zote Akishashinda ndo mfalme anaitwa kuja kumalizia aonekane na yeye ni Shujaa.

Mfalme Daudi Akapata Tamaa Ya Kuhesabu Watu, kinyume na Matakwa ya MUNGU,maana Aliwaambia yupo pamoja nao,wasije kujihesabu wapo wangapi,Yoabu akamshauri mfalme Daudi kwamba sio wazo zuri na aachane nalo,litaamsha Hasira ya MUNGU,lakini Mfalme akatoa Amri ya Mfalme,Yoabu ikabidi ahesabu watu..MUNGU akakasirika mno,na kumuadhibu daudi ila YOABU hiyo akaikwepa pia.

Mtoto Mkorofi wa Mfalme Daudi,Absalom, akakatiza anga za Yoabu,kwanza Absalomu akamwua ndugu yake Amnoni mtoto wa Mfalme Daudi kwa mama Mwingine,Kisa alimbaka dada yake Tamari, Mfalme Daudi hakumfanya kitu Absalomu,Yoabu alikasirika mno akaiweka rohoni,Absalomu akakimbia mbele ya baba yake,ila Yoabu kwa hila zake akambembeleza mfalme na kumwombea Absalomu msamaha mpaka akarudi kutoka mafichoni
Absalom akaenda mbali zaidi,akaunda jeshi,Akampindua baba yake Ghafla,ikabidi baba yake akimbilie Milimani,Yoabu akakusanya jeshi fasta akafanya vita na Absalomu,Lakini wakati anaenda vitani,Mfalme Daudi akasema Kabisa,Naombeni msimuue wala kumtenda Vibaya mwanangu Absalomu,Yoabu akamvamia Absalomu kama Upepo wa kisulisuli akalisambaratisha jeshi lake na Absalomu akatoroka lakini akakwama kwenye miti ya mialoni,Maafisa wengine wote wakakataa kumuua Absalomu,Yoabu akaenda akamchoma na Kumuua Mtoto wa Mfalme kisha akamzika kwenye lishimo huko huko porini,bila hata ya heshima yoyote,pamoja na kumwombea kwa baba yake alipokimbia bado hakusita Kumuua bila huruma.

Mfalme Daudi akalia na kuomboleza kwa Ajili ya mwanae,na israel yote ikalia nae nae,na wanajeshi,Yoabu Akamfata Mfalme akamwambia Badala Utoke nje uwaambie watu leo tumeshinda ndo unawavunja moyo kwa maana adui yako kafa na wewe unaomboleza sasa walienda vitani kufanya nini? ikabidi mfalme ajifute machozi ajikaze na kushangilia kwamba wameshinda Vita,ushauri wa Yoabu ukapita ila Mfalme akawa kamchoka kwa uovu wake.

Akamshusha Yoabu cheo,na Kumpandisha Amasa Kuwa Jenerali wa Jeshi,wakiwa vitani Yoabu akamwita Amasa Amkumbatie, kwa Amani,Amasa alivyosogea tu,Yoabu akamchoma tumbomboni na jambia hadi akafa,wakati Amasa anatoka damu na kukata Roho,Yoabu akaongoza majeshi kwenda kwenye vita zote Mfalme daudi alizompangia Amasa,na akashinda zote akarudi kama Jemedari na jenerali Mkuu,what a Villain?

Mfalme Daudi Alipokua mzee,na Yupo kitandani,Mtoto wake Adoniyah alijitangaza Mfalme kinyume na matakwa Ya mfalme Daudi, Mfalme Daudi Akamtawaza Solomoni awe Mfalme Badala yake,wakati huo Yoabu alikua Ameungana na Adoniyah,Aliposikia Solomoni kawa Mfalme alitetemeka Mno,Na Mfalme Daudi alimwambia Solomoni Mambo yote Yoabu Aliyoyafanya,Akimwambia wewe Una Busara,utajua Cha kumfanya, usiache Mvi zake zikashuka kaburini kwa Amani, Yoabu Akakimbilia Madhabahuni na kushika pembe ya Madhabahu,Mfalme Solomoni Akamtuma Kamanda wake mkuu Benaya mwana wa yehodaya, na kumpa Amri amwulie hapo hapo Madhabahuni,kisha wakamzika nyikani...yaani porini...na huo ndo ukawa mwisho wa ubabe wake.

My Take: Yoabu Alikua Katili sana,nakumbuka nilisoma mahali mfalme wa edom anaitwa Hadadi alikimbilia misri hadi aliposikia Yoabu amekufa,Mfalme Daudi alikua anamwogopa Yoabu,na inasemekana kama sio undugu wao hakuna ambae angeweza kumzuia Yoabu asiwe Mfalme Israel,ndio maana alijitaftia position anayoitaka japokua alikua na kaka yake Abishai ambae alikua mwanajeshi na rafiki wa Mfalme,Pamoja na Hayo bado Yoabu alishinda vita nyingi akiwa mtu katili na akicha kumbukumbu mbaya kwa maadui wa mfalme,akipiga kila utawala adui wa mfalme daudi na kumletea mali nyingi mno na milki kubwa sana,cha kushangaza alikua mtiifu kwa daudi na mkatili kwa wakati mmoja,huku akiamua mambo yake anayafanya,iwe mfalme anataka au la.

Alilinda nafasi yake ya jemedari kwa Ncha ya upanga,Alimwua Abner kwa Kisa cha ndugu yake Asahel lakini wachambuzi wanasema ilikua ni hofu ya nafasi yake kuchukuliwa na Abneri na hii ilidhihirika alipomwua pia Amasa.

Huyo Ndio Yoabu bin Seruyah au yoav bin zeruiah....nakaribisha maswali maoni na pia marekebisho nilipokosea...
Myths
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom