Mjue tapeli aliyewatapeli graduates wengi kwa kuwahadaa nafasi za kazi NMB

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,120
Jamaa Facebook anajiita Venance Mbike akitaka kukutapeli anakuanzia mbali kidogo kwenye kipengele cha kukuomba urafiki. Kisha anajifanya mlisoma wote aidha chuo kikuu au sekondari lakini yeye alikutangulia kidogo but anakufahamu sana.

Kama unapenda siasa atakupeleka huko, kama u mpenzi wa mpira hatakuwa nyuma pia.

Atakwambia kuwa yeye ni muajiriwa NMB mkoa fulani mbali na wewe. Sasa kuna siku atakwambia kuwa job wametangaza nafasi nyingi kama una ndugu hana kazi aombe.

Hapo kwenye mchakato wa kuomba kazi ndipo utakapoibiwa. Atakupiga ya certify vyeti, atakupiga ya hongo kwa meneja wa kanda au tawi, atakupiga ya vikorombwezo vingi mdogomdogo.
Kawapiga wengi.
Anatumia picha hii Facebook sijui kaitoa wapi. Kuna picha nyingine inafanana na hii kimavazi pia anaitumia kuwaibia vijana wenye njaa na ajira.

Mimi hajaniibia niliuruka mtego wake.
Vijana tuwe makini, ni aibu msomi kutepeliwa kirahisi.
FB_IMG_15916490789007679.jpg
 
Maisha ya average graduate kwa Tz ni utata. Ndiyo maana hawa matapeli hawapungui na wanasurvive kiuchumi.

Kuna mshkaji nimemaliza naye chuo. Yeye alikua education ila kuna modules tulishea, yule mshkaji sasa hivi ni freelancer wa Airtel anasajilisha watu laini so anapita mtaani kwangu almost every other day.
 
Hivi kuna mabogus bado wanaibiwa kizembe hivi
Mkuu hawa vijana wanasikitisha sana.
Kibaya zaidi wameenda shule.
Muda huu nipo sokoni hapa vijana na wazee hawalali wanapiga kazi hasa.
Wamama pia wanakoleza majiko wapike vitafunio chai na uji.

Cha ajabu sisi vijana tena wasomi hatutaki fanya kazi na kuamua kujiajiri kwenye utapeli.
 
Umejuaje kama amewaibia vijana wengi?
Wingi unaanzia na 2, niliosoma nao kadhaa ashawapiga. Siku ananitonya nafasi za kazi NMB kanda ya kaskasini mimi sikuwa tayari kuingia NMB kwakuwa nina kibarua changu sehemu nyingine, nikasema nimuunganishe rafiki yangu. Nilipomwambia tu nimempa namba akasema huyu kamtapeli fulani, fulani na fulani.
 
Kuna Jamaa mwingine sijui kwasababu sasa yupo wapi anaitwa Andrew Njile kawatapeli sana marafiki na graduates wengi tu kwa ahadi kama hizi akijinasibu anafanya kazi Benjamin Mkapa Foundation kama HR msaidizi.

Huko instagram walishamuexpose akijinasibu kama mtoto wa kigogo mmoja mstaafu serikalini. Isijekuwa ndio yeye akiendelez harakati zake kwakutumia picha za mtu mwingine.
 
Mkuu hawa vijana wanasikitisha sana.
Kibaya zaidi wameenda shule.
Mda huu nipo sokoni hapa vijana na wazee hawalali wanapiga kazi hasa.
Wamama pia wanakoleza majiko wapike vitafunio chai na uji.

Cha ajabu sisi vijana tena wasomi hatutaki fanya kazi na kuamua kujiajiri kwenye utapeli.
Shauri wakalime na siyo kuchoma maandazi na chapati. Kilimo pekee ndiyo suluhisho la umasikini kwa vijana. Ardhi tunayo kubwa na mahotaji ya chakula ktk hii Kanda bafo yapo juu

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Wingi unaanzia na 2, niliosoma nao kadhaa ashawapiga. Siku ananitonya nafasi za kazi NMB kanda ya kaskasini mimi sikuwa tayari kuingia NMB kwakuwa nina kibarua changu sehemu nyingine, nikasema nimuunganishe rafiki yangu. Nilipomwambia tu nimempa namba akasema huyu kamtapeli fulani, fulani na fulani.
Utapeli wa kitoto huu
 
Uvivu, Kupenda kitonga, kutoshughulisha akili ndio chanzo cha kutapeliwa..

Ila Mkuu una uhakika hio picha ni yake?
Matapeli wengi wa mtandao hawatumii picha zao.

Kama huyu kweli ni tapeli hivyo na katumia picha yaka na/au jina lake halisi....

Naye akili zake hazitofautiani na hao anaowatapeli.
Ni pwagu na pwaguzi....
 
Mwenye picha akiiona ndipo achukue hatua, ajue kuwa watu wanaibia watu kwa picha yake. Unajua mtu akitumia details zako mufanya uhalifu wewe unaweza kuingia matatizoni na utakapojitetea sio mimi ushaumia na kuchafuliwa.
 
Shauri wakalime na siyo kuchoma maandazi na chapati. Kilimo pekee ndiyo suluhisho la umasikini kwa vijana. Ardhi tunayo kubwa na mahotaji ya chakula ktk hii Kanda bafo yapo juu

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
Mtaji wa kuchoma maandazi ni kilo 2 za ngano, mkaa wa buku na mafuta lita moja na nusu.

Magazeti robo buku.

Niambie huo mtaji wa kukodi au kununua shamba, mbegu vitendea kazi.
Changamoto za kilimo zote, sijaongelea sokoni bado.

Kilimo cha matajiri.
Ni bora awe ananunua mazao shambani anapeleka sokoni kuliko kulima.

Kulima ni kwa matajiri.
Maskini ni mateso.
 
Back
Top Bottom