CV ya Prof. Ibrahim Lipumba, msomi, mtumishi aliyetukuka na mwanasiasa mvumilivu

Dah jamaa amenipa hasira vibaya kwenye results zake,hiki kichwa adimu duh gpa 4.5 means A kwenye theory na Practicals zote damn kukaza kwangu kote hz results cjawah pata,thnw mtumaji umenipa motisha
ni stanford university

CV YA PROF. IBRAHIM LIPUMBA - SEHEMU YA 1
1st part of Prof. Ibrahim Lipumba’s Profile;
Professor Nguyuru Ibrahim Haruna Lipumba (born 6 June 1952) is a Tanzanian economist, politician and chairman of the Civic United Front (CUF) party.
Although he is more known for his involvement in the political arena, Professor Lipumba, born in the Tabora region of Tanzania, and holding a doctorate in Economics from Stanford University is a prominent scholar (professor of economics). He has held a number of positions in the field of education, as a University Professor both in the United States and at home; and as a freelance economist -having been the economic adviser to the Ugandan government in the late 80s to early 90s.
Professor Lipumba has held the position of Chairman of one of the Tanzania’s main opposition party, The Civic United Front from 1995 to present day. He has also contested every presidential election in Tanzania since the country instituted a multiparty system in the early 1990s. In the first election in 1995, he placed third and won 6.43% of the vote. He finished second behind incumbent President Benjamin Mkapa in 2000, capturing 16.26% of the vote.
Running again as the CUF presidential candidate in the 14 December 2005 elections, Lipumba again finished second to Jakaya Kikwete of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) party winning 11.68% of the vote.
In 2010 Tanzania Elections he became third after CCM’s Kikwete and CHADEMA’s Wilbroad Peter Slaa.
Professor Lipumba is a skilled orator drawing large crowds for his rallies; he is also an intellectual at heart and continues his career as a freelance economist albeit on a smaller scale due to political commitments.
Curriculum Vitae for Prof. Nguyuru Haruna Ibrahim LIPUMBA:
Date of Birth: 6th June 1952

Marital Status: Married
Field of expertise:
• International Trade and Finance, Macroeconomics

• Development Economics and Agricultural Economics
Current research focus:
•Impact of
 
Dah jamaa amenipa hasira vibaya kwenye results zake,hiki kichwa adimu duh gpa 4.5 means A kwenye theory na Practicals zote damn kukaza kwangu kote hz results cjawah pata,thnw mtumaji umenipa motisha
ni stanford university

CV YA PROF. IBRAHIM LIPUMBA - SEHEMU YA 1
1st part of Prof. Ibrahim Lipumba's Profile;
Professor Nguyuru Ibrahim Haruna Lipumba (born 6 June 1952) is a Tanzanian economist, politician and chairman of the Civic United Front (CUF) party.
Although he is more known for his involvement in the political arena, Professor Lipumba, born in the Tabora region of Tanzania, and holding a doctorate in Economics from Stanford University is a prominent scholar (professor of economics). He has held a number of positions in the field of education, as a University Professor both in the United States and at home; and as a freelance economist -having been the economic adviser to the Ugandan government in the late 80s to early 90s.
Professor Lipumba has held the position of Chairman of one of the Tanzania's main opposition party, The Civic United Front from 1995 to present day. He has also contested every presidential election in Tanzania since the country instituted a multiparty system in the early 1990s. In the first election in 1995, he placed third and won 6.43% of the vote. He finished second behind incumbent President Benjamin Mkapa in 2000, capturing 16.26% of the vote.
Running again as the CUF presidential candidate in the 14 December 2005 elections, Lipumba again finished second to Jakaya Kikwete of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) party winning 11.68% of the vote.
In 2010 Tanzania Elections he became third after CCM's Kikwete and CHADEMA's Wilbroad Peter Slaa.
Professor Lipumba is a skilled orator drawing large crowds for his rallies; he is also an intellectual at heart and continues his career as a freelance economist albeit on a smaller scale due to political commitments.
Curriculum Vitae for Prof. Nguyuru Haruna Ibrahim LIPUMBA:
Date of Birth: 6th June 1952

Marital Status: Married
Field of expertise:
• International Trade and Finance, Macroeconomics

• Development Economics and Agricultural Economics
Current research focus:
•Impact of

kweli jamaa ni role modo mzuri jamani.maana ni exceptional accademically na in skills,HANA HOFU YUPO NA EIMU YAKE.JUZI BUNGENI KANIFURAISHA SANA
 
wabongo bwana kwenda usa na kuhojiwa bbc ndo imekuwa nongwa; kuna kujua nadharia za uchumi na kunakujua namna ya kufix uchumi. Prof haruna ni mzuri kwenye nadharia za uchumi. Lakini sio mweledi wa kutengeneza uchumi. Hawezi kwenda ugiriki akatengeneza uchumi wa nchi ile kwasababu hataweza. Ulishawahi kuona prof amekuja na kabrasha linaloeleza namna ya kukwamua uchumi wa nchi hii? Zaidi ya kuwa picky kwenye baddhi ya maeneo fulani fulani. Lakini sijawahi kuona mkakti wake mbadala wa kukwamua uchumi- usiniambie habari ya ilani ya uchaguzi
ni mwokozi wa uchumi wa uganda miaka ya 80s,ni mshauri wa mambo ya uchumi nchi nyingi tu nje,pia anakataba na shirika la umoja wa mataifa kufanya research fuan hiv ambapo duniani alipata nafasi kati ya maelfu ya maprofesa
 
wataalam wa uchumi wa tanzania ni wa vitabu tu....kwa vitendo hawawezi...dunia ya sasa ama tanzania tunataka watalam kwa vitendo pia waoneshe
 
Maisha ya awali ya Prof Ibrahim Haruna Lipumba ni safara yenye kusisimua na kujitutusa kizalendo huku tukiweka kando roho zetu za eda, Lipumba mwenyeji wa ubwa, mhafidhina wa kizalendo, mwenye tabasamu la kati, mwenye busara ya nera na asiyeishiwa hekima, ni simulizi la kujivunia utaifa wetu na Utanganyika wetu kila umuelezapo binadamu huyu aliyebeba alama ya usomi wa Kitanzania.

Prof Ibrahim Haruna Lipumba alizaliwa tar. 6 Juni Mwaka 1952, katika kiji cha Ilolangulu Wilaya ya Tabora Mkoani Tabora Tanzania. Ameanza elimu ya msingi 1959 - 1962 katika shule ya msingi ya Swedish Free Mission Primary School, Sikonge 1962 - 1966 : L.A Upper Primary School, Sikonge

Baadae kuendelea masomo na Elimu ya Sekondari 1967 hadi1970 Tabora Boys Secondary School 1971 hadi 1972 Pugu Secondary School Kisha Elimu ya Chuo Kikuu 1973 hadi 1977 University of Dar es Salaam 1978 hadi 1983 Stanford University. Akapata Shahada BA (Hon.Economics) University of Dar es Salaam 1976 MA (Economics) University of Dar es Salaam 1977 MA (Economics) Stanford University 1979 Phd (Economics) Stanford University1983

Uzoefu wa Uongozi

Aliwahi kuwa mweka hazina wa Umoja wa Vijana Tabora Boys Secondary School toka mwaka 1969 hadi 1970 pia akawahi kuwa Katibu mkuu wa wa Kikundi cha Majadiliano cha Tabora Boys Secondary School toka mwaka 1969 hadi 1970, baadae akaja kuwa Mjumbe wa kamati ya Umoja wa Vijana katika shule ya pugu Secondary School hiyo ilikuwa mwaka 1970 hadi 1971, baadae akaja kuwa tena Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam toka mwaka 1975 hadi 1976. na pia ndiye Mwanzilishi na Rais wa Kwanza wa Stanford African Students Association (SASA), Stanford University; Stanford, California USA hiyo ilikuwa mwaka 1978.


Kazi
◾1976 hadi 1977 Mkufunzi Msaidizi (T.A)
◾1977 hadi 1983 Mhadhiri Msaidizi
◾1983 hadi 1986 Mhadhiri
◾1986 hadi 1989 Mhadhiri Mwandamizi
◾1989 hadi 1993 Profesa Mshiriki
◾1991 hadi 1993 Msaidizi wa Rais Mambo ya Uchumi
◾1993 hadi 1995 Fulbright Visiting Professor, Williams College, Massachussets, United States of America
◾1996 hadi 1998 Senior Research Fellow, United Nations University, World Institute of

Economic Research, Helsinki Finland.


Heshima za Kitaaluma

◾1993 hadi 1995 Fulbright Visiting Professorship
◾1986 hadi 1989 Kellogg International Fellow in Food Systems
◾1977 hadi 1983 Rockefeller Foundation Fellowship
◾1976 Zawadi ya Mwanafunzi Bora, Best Student

Award, Faculty of Arts and Social Sciences,University of Dar es Salaam.


Mshauri wa Uchumi

◾The World Bank
◾UNDP
◾Global Coalition for Africa
◾Preferential Trade Area for Eastern and Southern Africa ( COMESA )
◾Swedish International Development Agency ( SIDA )
◾NORAD
◾DANIDA
◾Ministry of Foreign Affairs Finland
◾Bank of Tanzania
◾Macroeconomic and Financial Management Institute of Eastern and Southern Africa (MEFMI)
◾African Capacity Building Foundation.


Shughuli za Kimataifa

Utafiti kuhusu kushiriki kwa nchi za kusini katika mfumo wa biashara wa kimataifa, Uruguay Round Multilateral trade negotiations kuanzia mwaka 1986 ha 1990.

Utafiti kuhusu sera za kilimo za nchi zinazoendelea.

Kuwasilisha maelezo (Testmony) kuhusu matatizo ya madeni ya Afrika kwenye kamati ya Bunge la Marekani - House Sub Committee on International Development, Finance, Trade and Monetary Policy - Februari 1994.

Kuwasilisha, maelezo (Testmony) kuhusu shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na uhusiano wake na nchi masikini kwenye kamati ya Bunge la Marekani House - Sub Committee on International Development, Finance, Trade and Monetary Policy - Aprili 1994

Kutayarisha "Report of Group of Independent Advisers on Development Cooperation issues between Tanzania and Aid Donors". Juni 1995

Kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya sera ya maendeleo (member of the United Nations Committee for Development Policy (1995 hadi 1999.)

Kutayarisha vigezo vya kuainisha nchi masikini sana duniani. (The list of Least Developed Countries (1997 na 2000)

Kutayarisha na kuratibu utafiti na kupendekeza sera za viwango vya kubadilishana sarafu (exchange rate policy) na sera za kulegeza masharti ya mfumo wa fedha (financial liberalization) Kampala, Uganda (1997).

Kutayarisha na kuratibu utafiti na kupendekeza sera za viwango vya kubadilishana sarafu (exchange rate policy) na sera za kulegeza masharti ya mfumo wa fedha (financial liberalization) Kampala, Uganda (1997).

Kutoa taarifa katika Kamati ya Umoja wa Mataifa ya mambo ya uchumi na maendeleo (ECOSOC) kuhusu mgogoro wa kimataifa wa fedha katika nchi za Asia, NewYork (1998).

Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Windhoek, Namibia (1998).

Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Mbabane, Swaziland (1998).

Kutathmini maendeleo ya ‘The Macroeconomic And Financial Management Institute Of Eastern And Southern Africa', (MEFMI) ili kuwasaidia wahisani kufanya maamuzi juu ya kuendelea kuisaidia taasisi hiyo,1998.


Shughuli za Kitaifa

◾Mjumbe - Kamati ya kurekebisha mashirika ya umma, 1992 - 1993

◾Mwenyekiti - Tume ya kuchunguza matatizo ya chama cha ushirika cha mkoa wa Shinyanga (SHIRECU), 1992

◾Mwenyekiti - Tume ya Waziri wa Fedha ya kuchunguza matatizo ya Shirika la Bima (NIC) 1993


Baadhi ya Tafiti za Uchumi na Maandishi Muhimu

◾Stabilization Policies in Tanzania, University of Dar es Salaam, 1984

◾African Unity, Some Practical Guidelines, MAWAZO Vol. 1. No. 2, Mei 1983. Published by Stanford African Students Association.

◾Problems and Prospects of African Economic Integration , MAWAZO Vol. 1. No. 1, Aprili 1982

KATIKA SIASA,

Lipumba katika siasa ameanza kuhudumu tangu mfumo wa vyama vingi ulipoingia nchini 1992, na yeye Lipumba ni muumini wa siasa za kiliberali, anaamini katika usawa, haki kwa wote na uhuru wa kutoa maoni,

Katika uwanda huu wa siasa Lipumba hajafanikiwa vyakutosha, chama chake hakijawa sehemu ya tishio kubwa kwa chama tawala kwa siasa za kitaifa kwa ujumla, hii inatokana na madhaifu machache ya Prof Lipumba katika uga huu wa siasa za kisasa,

Siasa za kisasa zinahitaji mageuzi, zinahitaji kusafiri na nyakati pia siasa zinahitaji fikra mpya kulingana na mapokeo mapya ya kidunia hasa katika ukuaji wa fikra za kibinadamu. Hayo Lipumba ameyakosa ama hana kabisa, CUF hayo imeyakosa ili kuiishi dunia mpya ya fikra chanya.

Tatizo kubwa lipo kwenye muundo wa Chama na falsafa yake ikiwemo itikadi, CUF kiliundwa kwa mtazamo wa harakati za wanyonge waliokosa vyote katika nchi inayojengwa na wanyonge wenye moyo na kuliwa na wajanja wenye meno (ccm). Muundo huu ulibeba taswira hasi hasa baada ya makutano hawa kukosa vyote kabisa na kikubwa ikawa ni elimu, na wezo wa kushawishi makundi ya wasomi kujiunga nao.

Hili lilikuwa pigo kuu, kwakuwa ili chama kiweze kuishi na kutembea katika kila hatua ya mageuzi ni lazima kiwezeshwe na wasomi na wenye fikra chanya (mawazo mapya), Chama kikajijenga mwambao mwa nchi, kikapata ufuasi mkubwa katika matabaka ya wanyonge tena wanyonge hasaaaa yani wasioweza kulinda kura zao hata kwa masaa 12 tu, hili lilikuwa pigo hasa ukipambana na ccm inayosafiri na kuishi kwa mbeleko ya Usalama wa Taifa na vyombo vingine vya dola.

Msomi Lipumba pekee yake asingeweza kuleta mageuzi mapya ndani ya CUF bali alihitaji na anahitaji nguvu kubwa ya fikra za wasomi kila pembe ya nchi ili kusafiri kisiasa, Itikadi ya CUF imeweza kushamiri Zanzibar kwasababu ya slogan yake imara hasa ile ya uhuru wa Zabzibar, lakini Uhuru ukipatikana CUF itakosa itikadi kabisa yenye kuishi kisiasa, itakosa kama ilivyo ccm leo huko visiwani.

Muungao wa vyama ndugu wa UKAWA umeileta CUF katika uso wa dunia mpya, umemleta Prof Lipumba yule wa 2001, sasa sauti kuu ya siasa za nera imezaliwa upya, mwana wa unyamwezi amerejea katika uga wake.

Kama UKAWA watampitisha Prof Ibrahim Haruna Lipumba kugombea urais, basi sarafu halisi itakuwa imetua mahali stahiki kati ya hazina walizo nazo UKAWA.
 
Baada ya kusoma huo wasifu wa Lipumba nilichogundua ni kuwa anafaa zaidi katika nafasi za kitaaluma za kiutendaji lakini si nafasi za kisiasa.Siasa sidhani kama kwa wasifu huo alionao zinamfaa.Naona kapotea njia angebaki huko kwenye taaluma angefika mbali zaidi hata kuwa murugenzi MKUU wa shirika la maendeleo la umoja wa mataifa.

Kwenye siasa naona hakumfai kabisa.Yeye si mtu wa kushinda kwenye maandamano mabarabarani kama wasiosoma akina Sugu au mbowe angeweza kuchangia vizuri kwenye hii dunia kupitia taaluma yake
 
Ukiondoa kasoro ya siasa/kampeni zake za kidini 2010 (hilo linarekebishika)...nitampa kura yangu ya uRais iwapo UKAWA watamsimamisha kama mgombea pekee wa uRais kwa upinzani.
 
Ilolangulu vipi wamenufaika popote na hii CV? Na umoja wa vijana kwa wakati ule unamaanisha wa Tanu na CCM?
 
Mkuu Yeriko, kati ya Lipumba na Dr Slaa, nani anafaa kupeperusha bendera ya ukawa kwa kigezo cha elimu, uzoefu, tabia njema, mahusiano na jamii, umri nk?
 
Hata wewe unakubaliana na propaganda za CCM? Umesahau container la majambia waliyoipakazia CUF...
Ukiondoa kasoro ya siasa/kampeni zake za kidini 2010 (hilo linarekebishika)...nitampa kura yangu ya uRais iwapo UKAWA watamsimamisha kama mgombea pekee wa uRais kwa upinzani.
 
Hata wewe unakubaliana na propaganda za CCM? Umesahau container la majambia waliyoipakazia CUF...

Sio kila kitu wa kulaumiwa ni CCM...video za Lipumba akifanya kampeni/siasa kwenye mihadhara misikitini zipo kila mahali. Lakini kila binadamu ana mapungufu, kama nilivyosema, hilo linasameheka na kusahaulika...he will make a good president, hasa kuinua uchumi wa nchi hii kama alivyojitahidi mzee Mkapa! na atapata kura yangu akisimama kwa UKAWA.
 
Back
Top Bottom