Mjue Oladee, kichwa kinachotembea akiwa analia bila Passport

DIDAS TUMAINI

Senior Member
Nov 11, 2014
122
500
Jina lake halisi anaitwa Oladee kijana mzaliwa wa Nigeria. kwa sasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Ilorin kinachopatkana eneo la Kwara nchini Nigeria.

Mwaka 2009 Oladee alipata mkasa mkubwa ambapo badae mkasa huo ukamfanya kuwa mtu maarufu sana duniani.

Mwaka 2009 alipewa kiasi cha Naira200 na bibi yake kwa ajili ya kununulia mahitaji ya chakula cha usiku,ikabidi aongozane na rafiki yake kwenda sokoni kwa ajili ya kufanya manunuzi hayo, lakini wakiwa Njiani walipita sehemu ya kucheza kamari/ bet na rafiki yake akamshawishi ili waizalishe ile hela N200.

Kwa bahati mbaya hela yote waliyopewa ikaliwa kwenye kamari (bet), hiyo ndio hapo sasa bwana Oladee alipoanza kulia ili arudishiwe hela yake.
1585717183987.png
Alilia kwa hisia kali sana akikumbuka nyumbani bibi yake atamwadhibu hivyo alijaribu kumsawishi aliyemla arudishe hela yake bila mafanikio.

Kwa sasa Oladee yupo chuo kikuu na bado anajishughulisha na kuchekesha na kurekodi video fupi fupi, lakini analalamika kuwa hafaidiki na kile kinachotumika mitandaoni kama Facebook, Instagram na hata WhatsApp anatumika kama stickers lakini hakuna anachofaidika nacho.

Watu wanamwita kichwa kinachotembea bila passport kwa sababu picha yake hii imesambaa dunia nzima na watu wanai edit kwa kuifanyia vituko.
FB_IMG_1580273072675.jpeg FB_IMG_1579984681596.jpeg FB_IMG_1580273070356.jpeg
FB_IMG_1580273067567.jpeg
Sent using Jamii Forums mobile app
 

fundi bishoo

JF-Expert Member
Jun 26, 2018
6,504
2,000
Taffo kotopi uyo jamaa mnaigeria
Nadhan alitoka bush sjui kaenda town kavamia mademu wakamliza hela ndo akawa analia basi ndo akawa maarufu naigeria na hata dunia nzma maana sticker yake inatumiwa sna a.k.a yake wanamwita sticker boy na kuna clip moja jamaa analalamika kutumiwa kwa hy head stiker yake illhali hanufaik kwa lolote anataka awe analipwa

yess BiShoo haswaaAaa
 

kakamtumishi

Senior Member
Jun 18, 2016
162
250
Anaitwa ODELE ni mnaijeria ni tukio la mwaka 2009 alishawishia na rafikize abet pesa aliyopewa bibi yake kwa ajili ya kujikimu!!so akawa analia ili apate huruma pesa irudishwe au mwenye kujitolea ampe fedha ili kutoonekana mdhalimu kwa bibiye!!

Ila cha ajabu picha imesambaa sana kwa sasa kwa mfumo wa sticker na different editings!!anachukizwa na hali sana ya kueditiwa!!amemaliza chuo mwaka 2019
 
Top Bottom