barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Wengi wa vijana wa mjini wamekuwa wakichagua kazi, lakini hali ni tofauti kwa bidada huyu Swabrina Ghalibu (19), unaambiwa ni mwanamke wa kwanza mhudumu wa Mochuari pale Hospitali ya Tumbi (Kibaha) huku wengi wakimsifia kuwa ni 'Jembe' . Mfwatilie hapa;
SWALI: Wewe mbona huogopi
SWABRINA: Ni kazi ambayo ninaipenda. Sikushawishiwa na mtu na hivyo naifanya kwa moyo mmoja bila ya woga.
SWALI: Marafiki zako wanakuchukuliaje, hasa wale mnaoishi nao Mlandizi na hata wale mliomaliza nao shule ya sekondari?
SWABRINA: Ki-ukweli wananiogopa sana! Kuna waliowahi kuja hapa Mochuari walikuwa wamefiwa. Waliponikuta hapa, walishangaa sana. Waliniogopa na kusema mimi sio mtu wa kawaida.
Una neno gani la kumwambia dada huyu mwenye ujasiri uliowashinda wanaume wengi?