Mjue mmiliki halali wa Wasafi Tv

Mtu kuwa majority shareholder ktk kampuni hakumfanyi awe mmiliki wa kampuni kuzidi wanahisa wenzake.

Majority shareholder ana enjoy right ya maamuzi ya wapi kampuni ielekee kibiashara. Ila at the same time, minority shareholders wanakuwa protected na sheria ya makampuni endapo majority shareholder ataathiri interests zao ktk kampuni.

Sheria ya makampuni ya Tz inamruhusu minority shareholder kwenda mahakamani kulinda maslahi yake.

Mtu akiwa minority shareholder, hata akiwa na hisa moja...bado ni mmiliki halali wa kampuni kwa kiwango chake cha hisa anachomiliki. Na anazo haki za kufanya maamuzi yahusuyo kampuni kwenye members meeting.

So uwe majority au minority shareholder, what matters ni kuwa kampuni ikitoa gawio na wewe unapata kulingana na class za shares zako...whether ni ordinary au preferential shares.

So Diamond bado ni mmiliki halali wa Wasafi maana anahisa 45%...yaani kwa maneno mengine yeye anamiliki asilimia 45 ya thamani ya kampuni ya Wasafi Media. Huku mke wa kusaga akimiliki asiliamia 53...na huyo mwanahisa mwingine akimiliki asilimia 2.

Wote watatu kwa pamoja ni owners wa Wasafi media.
 
1.Mtoa mada umejipambanua kutoa elimu lakini kumbe wewe ni mchochezi tu.(Rejea kichwa cha habari ulichoweka) na kama kuna mmiliki asie halali pale umtaje mkuu
2.Ushahidi unaoeleza unao ni wa mwaka 2018, almost miaka mitatu sasa. Je kwa elimu uliyonayo huwezi ukafanya utafiti ili utupatie current data, au hizo hisa ni static?
3.Kwa mfano wako kuhusu Simba na Mo, unahisi kati ya nyie wanachama wenye %51 na Mo mwenye 49% nani ni mshika pembe?
4.Nje ya usomi wako na mambo ya shares, wewe binafsi una rate vipi nguvu ya Diamond pale wasafi?
 
Hakuna anayetaka kushusha mondi
Na ukimuona mtu anaemshusha mwenzake Basi huyo ni mchawi tu tena mchawi hasa.

Nilichomaanisha Mondi sio majority shareholder.

Who is major shareholder, what are his/her rights, nadhani kuna internet unaweza soma.

#YNWA
Mkuu, tatizo humu pamejaa wasomi wengi wa shule za Kata ambao vichwa vyao vimejaa makamasi tupu. Watakupa shida sana kuwaelimisha aisee!
 
1.Mtoa mada umejipambanua kutoa elimu lakini kumbe wewe ni mchochezi tu.(Rejea kichwa cha habari ulichoweka) na kama kuna mmiliki asie halali pale umtaje mkuu
2.Ushahidi unaoeleza unao ni wa mwaka 2018, almost miaka mitatu sasa. Je kwa elimu uliyonayo huwezi ukafanya utafiti ili utupatie current data, au hizo hisa ni static?
3.Kwa mfano wako kuhusu Simba na Mo, unahisi kati ya nyie wanachama wenye %51 na Mo mwenye 49% nani ni mshika pembe?
4.Nje ya usomi wako na mambo ya shares, wewe binafsi una rate vipi nguvu ya Diamond pale wasafi?
Sasa hiki umeandika nini mkuu? Au nawe ndio wale wale washabiki mandazi? Tuliza akili uandike kitu kinachoeleweka.
 
Bwashee na wewe unateseka hivyo kweli mekuu,tafuta hela acha ufala wewee,we kweli ni bwashee au mshua kabambakiziwa?
Yaani unamchukia kijana mpambanaji elimu ndogo kisa kakuzidi kipato,tafuta helaaa
Mimi simchukii mtu na napenda sana bidii yake lakini msimuone mungu mtu...ilo ndio kosa lenu
 
Mimi simchukii mtu na napenda sana bidii yake lakini msimuone mungu mtu...ilo ndio kosa lenu
Hakuna anayemuona ni Mungu mtu,Mungu huwezi kumfananisha na kitu chochote kile labda kama una mapungufu kichwani,acheni kumchukia dogo aliyetoboa kwa juhudi zake huku akiwa hana shule na anazidi kufunguliwa kila siku na Mungu huyo huyo tena
 
Sasa kama hamumuoni mungu mtu kwanini mnamuona kakamilika na hakoseagi? Anajiweza na kila kitu ni chake? Hata mkiambiwa ukweli mnakataa kwa nguvu zote? Iyo ni kama kwamba mnamwabudu. Binadamu hajakamilika kuwa jamaa kusema mwenye hisa nyingi pale ni Kusaga kuna tatizo gani? Na ushahidi umepewa unataka nini tena?
 
Kwa hiyo ktk hili la uwekezaji wewe unaona kakosea?

Au kwa mtizamo wako labda kosa lake ni miliki hisa ndogo 45% kuliko Kusaga?

Basi kama ndivyo kwa akili yako basi hata Michael Jordan atakuwa kakosea,sababu nae ktk brand ya Jordan Nike wanashare kubwa kuliko Michael Jordan.
 
Sasa kama hamumuoni mungu mtu kwanini mnamuona kakamilika na hakoseagi? Anajiweza na kila kitu ni chake? Hata mkiambiwa ukweli mnakataa kwa nguvu zote? Iyo ni kama kwamba mnamwabudu. Binadamu hajakamilika kuwa jamaa kusema mwenye hisa nyingi pale ni Kusaga kuna tatizo gani? Na ushahidi umepewa unataka nini tena?
Hakuna anayemuona ni Mungu mtu sema nyie mnamchukia na kumuonea wivu kwa sababu ya mafanikio yake tu na si vinginevyo na ndio maana na sisi tunamtetea,hatuwezi kukubali mtu aliyehustle kivyake mumshushe tu kwa sababu ya chuki zenu
 
Wabongo kwa wivu hatujambo..Diamond kumiliki hisa 45% ni mafanikio makubwa sana.tujifunze kuwapongeza wenzetu wanapopiga hatua za kimaendeleo.
Upo sahihi sana mkuu,kuna watu hata hiki kidogo alichowekeza wanamuonea gere,yaani wabongo tuna roho nyeusi sana na ndio maana tunabaki na misongo ya mawazo sana kwa kuwachukia hata wasiopaswa kuchukiwa,imagine a couple of years ago ze boy from Tandale was very poor,but now he is a hero to his life,but still bad people don't appreciate him,they are just jelousy with no reason and they are not ashamed of themselves,very bad
 
Mkuu Ungeandika wajue wamiliki wa wasafi na sio mmiliki, Tambua kampuni kisheria na wamiliki ni vitu viwili tofauti, hapo kusaga anaingiaje?, Pili hoja yako ya umiliki wa asilimia haina mashiko wala uhusiano na kusaga. Tambua hata jeff bezos ni mmiliki na muanzilishi wa amazon na anamiliki 10% ya amazon.
ndugu umeongea kweli ilibidi aandike wamiliki,ni wazi anaonesha ana grudge na almasi,japo maelezo yake ni mazuri ya kitaalamu
 
Upo sahihi sana mkuu,kuna watu hata hiki kidogo alichowekeza wanamuonea gere,yaani wabongo tuna roho nyeusi sana na ndio maana tunabaki na misongo ya mawazo sana kwa kuwachukia hata wasiopaswa kuchukiwa,imagine a couple of years ago ze boy from Tandale was very poor,but now he is a hero to his life,but still bad people don't appreciate him,they are just jelousy with no reason and they are not ashamed of themselves,very bad
umesema kweli kabisa diamond ni nembo ya maisha ya vijana wengi,wenye malengo tofauti tofauti huku mtaani kuwa kumbe inawezekana kufika mahala unataka kama una nia
 
Iko hivi Clouds media ni family business ambayo ipo chini ya Kussaga Family yaaani iliazishwa kupitia Fedha za Marehemu Mzee Kussaga alafu mtoto wake huyu Kussaga Jr ndio akawa mkurungezi kutokana na yeye kuwa na experience kuwa na mshiko wa kutosha akaazisha Clouds media dubai, Rwanda na kampuni zingine lakini baadae akaona kama apati pesa za kutosha kutoka Clouds media bcz ya family ownership ndio akaazisha Wasafi Media from copy and paste ya Clouds media lakini akaingia makubaliano ya mkataba na Diamond ili watumie Wasafi brand kwa minajili ya kuipa Airtime kubwa huku Diamond akipata sehemu ya kuongelea mziki wake na matamasha yake ndio maana unaona Wasafi Media wanapita mule mule kwenye njia za Clouds media mfano Kuja kwa Koffi; Koffi anamawasiliano ya Karibu sana na Joseph Kussaga pia Tigo Wanaelewana sana na Kussaga ndio maana wameweza kukaa na Clouds media for more than 4 yrs to support Fiesta. Ukiangalia hata Vifaa wanavyotumia kwenye matamasha yao ni kutoka Prime time promotion. Clouds Media ilikuwa Ruge na Joseph. Ruge ni mtendaji lakini nyuma ya picha alikuwa chini ya Kussaga ndivyo ilivyo kwa Wasafi Media Diamond anaonekana ndio mmiliki lakini nyuma ya picha yupo chini ya Joseph Kussaga kupitia Mke wake.... Vijana tutafute pesa na tuwe na focus na vision.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom