Elections 2010 Mjue mgombea mwenza wa CHADEMA

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
08_10_177eaa.jpg

THE CHADEMA Presidential candidate Dr Willibrod Slaa (left) and his running mate, Said Mzee Said display their forms received from the National Electoral Commission (NEC) Chairman, Judge Lewis Makame in Dar es Salaam on Monday
 
Nimeupenda ubunifu wa shati la Mgombea Mwenza, nadhani Dr. Slaa anapokuwa kwenye vazi la Bendera basi lisiwe lile alilokuwa amevaa last week, kitafutwe kitu kama hicho alichovaa mgombea mwenza, nadhani kuna wabunifu wengi wanaweza kutengeneza kitu much better than that.
 
Wakuu,

Naomba mwenye data za mgombea mwenza azimwage.

Ningeomba pia nitoke nje ya mada kidogo ili kujenga ulinganifu wa muungano na mgombea mwenza. Mgombea mwenza ni mtu muhimu sana kwa sababu ni kiongozi wa pili kimadaraka. Sasa Zanzibar wana bendera yao, wimbo wao wa taifa, leo wamesema ni nchi iliyoungana na ''hakuna'' maana Tanganyika haipo. Mafuta ni yao ingawa ardhi ni ya muungano. Wanabunge lao,raisi wao,Katiba yao,mikoa yao, Ajira zao lakini pia ajira ni muungano. Sasa kwanini sisi Watanganyika tulipe gharama za muungano ambao practically haupo?.

Gharama mojawapo ni hii ya kutulazimisha kuwa na mgombea kutoka visiwani! why?

Naomba kuelimishwa tafadhali! :confused2:
 
Una pointi ila nadhani jibu lake halitapatikana mapema.
 
naona data za huyu jamaa mgombea mwenza! sina data zake jamani mwenye nazo azimwage hapa ili tuangalie record zake kiuongozi.
 
Tunahitaji Wasifu wake, maana huyu in any case rais akipata matatizo yeye ndo ataenda kukaa mjengoni
 
Una pointi ila nadhani jibu lake halitapatikana mapema.
Mi siwalaumu walioziunganisha Tanganyika na Zanzibar. Pengine kwa wakati ule wa vita baridi na matishio ya kuvamiwa, muungano ulikuwa sahihi. Lakini kwa sasa kama muungano wenyewe ndio huo, wa nchi moja kuwa na dola yake wakati nyingine haina, then huu muungano uangaliwe upya. Umekwisha wakati wa kufanywa watoto, na kuzuiwa kuhoji.

Ni hesabu rahisi mno;

Tanganyika + Zanzibar = Tanzania.

Hapa kuna three and different components. Sasa kama mbili kati ya hizo zina-exist, za zina dola zake, ile ya tatu iliishia wapi? Kama lengo lilikuwa kuwa wamoja, then kwanini ka-component kamoja huko left hand side kanaexist?
 
Mbona hiyo rangi ya shati la m.mwenza inafanana na rangi ya CUF ya haki sawa kwa wote? au nimefananisha!
 
Amethibitishwa rasmi leo kuwa ndiye mgombea mwenza pamoja na Dr. Slaa katika kikao kilichofanyika leo
 
Amethibitishwa rasmi leo kuwa ndiye mgombea mwenza pamoja na Dr. Slaa katika kikao kilichofanyika leo
Shukrani Invisible kwa kutujuvya, waliokuwa wanasema katiba imevunjwa walikuwa hawajasoma kanuni zake.
 
08_10_177eaa.jpg

THE CHADEMA Presidential candidate Dr Willibrod Slaa (left) and his running mate, Said Mzee Said display their forms received from the National Electoral Commission (NEC) Chairman, Judge Lewis Makame in Dar es Salaam on Monday

mbona kama amelazimishwa? anaonekana bado ni CUF huyu
anyway hivi ana CV gani huyu bwana maana tunamgoogle lakini hakuna kitu
 
mbona kama amelazimishwa? anaonekana bado ni CUF huyu
anyway hivi ana CV gani huyu bwana maana tunamgoogle lakini hakuna kitu

Si bora awe amelazimishwa (kama alivyolazimishwa Dkt Slaa) kuutmikia umma kuliko fisadi Gharib Bilal (ex-Mlimani students tunakumbuka sana uhuni wake) aliyeteuliwa kishkaji kupoza mzuka wa washabiki wake Zenji?
 
Kikubwa hapa ni Slaa. Wagombea-wenza Tanzania hawajawahi kuwa muhimu. Si Shein wala aliyemtangulia wamefahamika. Hili tumaini lililoibuka Tanzania sasa linatokana na kukubali kwa Slaa kuwa Mgombea. Mengine yote hayana neno. Nobody will think about hawa wagombea wenza wakati wa kukipigia CHADEMA kura.
 
Yaani ndugu zangu na huu utume mnaojivika. Hii siasa ya kutaka kulabel kila aliye CCM ni fisadi na kila aliye upinzani ni MTUME ama Mkombozi ni siasa za kuhuni zisizo heshimu misingi ya uungwana ambayo wengi wenu mnapenda kujinasabisha nao.

Ni kweli nafasi hiyo ina kila dalili za nia ya kupoza washabiki wake Zanzibar lakini kamwe huwezi kumhusisha Dr Gharib Bilal na ufisadi. Kwa watu wanaohubiri ukombozi kutoka katika mfumo fisadi wenye kugubikwa na ujanjaujanja kama tulionao we expect more than just naming and shaming politics zilizojaa ujanjaujanja ambazo mtaji wake unaisha October mbili na yawezekana kabisa mkajikuta mmetumia mabilioni kutengeneza faida ya elfu kadhaa.

Chonde jamani Tanzania ni zaidi ya October 30......Ama hata kurasimisha Tanzania yenye chuki na mgawanyiko....
 
Kikubwa hapa ni Slaa. Wagombea-wenza Tanzania hawajawahi kuwa muhimu. Si Shein wala aliyemtangulia wamefahamika. Hili tumaini lililoibuka Tanzania sasa linatokana na kukubali kwa Slaa kuwa Mgombea. Mengine yote hayana neno. Nobody will think about hawa wagombea wenza wakati wa kukipigia CHADEMA kura.

Hivi mgombea mwenza si ndiye anayepaswa kushika majukumu ya urais pindi rais anaposhindwa kutekeleza ama kupatwa na matatizo makubwa? Hivi makamu wa rais si ndio mshauri mkuu wa rais katika maamuzi? Hivi mgombea mwenza ama makamo wa rais si ndio msimamizi mkuu wa masuala ya muungano? Hivi kiutamduni hapa Tanzania Makamo wa rais si ndio Mzee wa busara anayepaswa kuwa speed governor ya mapungufu ya rais?

Inaelekea kwa wengi wetu hapa mgombea mwenza is just another stupid consititution need and vote machine and no more than that...

Lets be serious jamani, Maslahi ya Taifa ni pamoja na kuwa responsible katika suala nyeti kama Umakamu Rais...ama rais wa akiba

omarilyas
 
Back
Top Bottom