Mjue mchina(Malkia wa Tembo) aliyetumalizia tembo wetu Tanzania

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
Ivory Queen': Mahakama ya Kisutu yampata na hatia 'malkia wa pembe za ndovu' Yang Feng Glan Tanzania
Ivory Queen': Mahakama ya Kisutu yampata na hatia 'malkia wa pembe za ndovu' Yang Feng Glan Tanzania

'Ushahidi wote unaonyesha jinsi gani nyinyi( washtakiwa) mmefahamiana kwa muda mrefu' amesema jaji Huruma Shaidi.

''Ushahidi unaonesha jinsi gani washtakiwa wote watatu walivyosaidiana kuhakikisha wanatafuta meno ya tembo sehemu mbalimbali na kuyasafirisha'' ameongeza jaji Shaidi.

Waendesha mashtaka wamebaini kwamba Bi Feng aliidhinisha mtandao wa kihalifu na kufanikiwa kusafirisha meno ya tembo katika maenoe tofuati kwa kutumia mgahawa wake wa vyakula vya Kichina kujificha na hata kutishia kuwaua watu katika kuidhibiti biashara hiyo haramu.

Kwa mujibu wa wanaharakati, hii ni kesi kubwa inayohusu ulanguzi wa pembe za ndovu kuwahi kushuhudiwa Tanzania.

Mnamo mwaka 2015, jopo maalum la wanyama pori nchini Tanzania liliwakamata Bi Feng miongoni mwa wengine walioshukiwa kusafirisha pembe za ndovu.

Makundi ya kampeni dhidi ya uwindaji haramu yalieleza kuwa wale waliokamatwa ni pamoja na mwanamke aliyepewa jina la utani 'Malkia wa pembe za ndovu' Yang Feng Glan.

_105699279_a9feacd1-fe8f-4248-a0fc-cac834ec2e66.jpg

Wahifadhi wameitaja Tanzania kama shina la uwindaji haramu wa pembe za ndovu.


  • 1550575139938.png
    • Ametoka Beijing, Bi Yang alifika Tanzania kwa mara ya kwanza katika miaka ya 70.
    • Ni mwanafunzi wa kwanza wa Kichina aliyefuzu Kiswahili.
    • Amefanya kazi kama mkalimani katika shirika la reli Tazara lililojengwa kwa usaidizi wa China.
    • Inaarifiwa kwamba baada ya ujenzi wa reli hiyo mnamo 1975 alirudi Beijing kufanya kazi katika idara ya biashara ya nje.
    • Mnamo 1998 aliamua kuanzisha biashara Tanzania.
    • Alikodisha jengo la orofa mbili Dar-es-Salaam, na kufunguwa mgahawa wa vyakula vya Kichina katika sehemu ya chini ya jengo na kufungua kampuni ya uwekezaji, Beijing Great Wall Investment, katika orofa ya juu.
  • Anashutumiwa kwa kuendeleza shughuli hiyo kwa takriban miaka 14.

    Maafisa wa serikali Tanzania walitaja kukamatwa kwa Yang Feng Glan kama ufanisi mkubwa.

    Taifa hilo la Afrika mashariki limepoteza thuluthi mbili za ndovu wake katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

 
Tajiri kuingia mbinguni ni sawa na Ngamia kupenya tundiu la Sindano...
 
Me nashauri alipe faini (japo ndiyo hali halisi) alafu afungishwe vilago arudi kwao china.
 
Atupwe serengeti na atembee kwa miguu mpaka atapobaki kichwa tu

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Mali zake zitaifishwe, alipe fidia, awaseme washirika wake wote kwanza, kabla ya kifungo cha maisha.
 
Bado hapo wakuu kuna vigogo wakubwa nyuma yake huyo bb.....

Huyu bb aliiweka serikali mfukoni,,,
Kila nukta alikua anapewa baraka na viongozi waovu wa Sirikali za nyuma...
Sasa kanasa kwa baba J
Kuna maeneo baba J namuelewaga sana,,,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom