Mjue mchina(Malkia wa Tembo) aliyetumalizia tembo wetu Tanzania

Mwisho wa cku tutaambiwa Mtuhumiwa hana hatia, au akipatikana na hatia atapigwa faini ya milioni5 Shamba la Bibi na Babu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli hizi mahakama zetu huwa zinafunga masikini tu...
Nimejiuliza wapo wapi wale akina Masamaki yule mwenye nyumba 70...
Wapi aliyetengeneza milioni 700 kwa SAA?
Wapi waliojiungia pipe ya mafuta toka bomba kuu bandarini?
Hao kina Rugeimarila mbona hawafungwi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ivory Queen': Mahakama ya Kisutu yampata na hatia 'malkia wa pembe za ndovu' Yang Feng Glan Tanzania
Ivory Queen': Mahakama ya Kisutu yampata na hatia 'malkia wa pembe za ndovu' Yang Feng Glan Tanzania

'Ushahidi wote unaonyesha jinsi gani nyinyi( washtakiwa) mmefahamiana kwa muda mrefu' amesema jaji Huruma Shaidi.

''Ushahidi unaonesha jinsi gani washtakiwa wote watatu walivyosaidiana kuhakikisha wanatafuta meno ya tembo sehemu mbalimbali na kuyasafirisha'' ameongeza jaji Shaidi.

Waendesha mashtaka wamebaini kwamba Bi Feng aliidhinisha mtandao wa kihalifu na kufanikiwa kusafirisha meno ya tembo katika maenoe tofuati kwa kutumia mgahawa wake wa vyakula vya Kichina kujificha na hata kutishia kuwaua watu katika kuidhibiti biashara hiyo haramu.

Kwa mujibu wa wanaharakati, hii ni kesi kubwa inayohusu ulanguzi wa pembe za ndovu kuwahi kushuhudiwa Tanzania.

Mnamo mwaka 2015, jopo maalum la wanyama pori nchini Tanzania liliwakamata Bi Feng miongoni mwa wengine walioshukiwa kusafirisha pembe za ndovu.

Makundi ya kampeni dhidi ya uwindaji haramu yalieleza kuwa wale waliokamatwa ni pamoja na mwanamke aliyepewa jina la utani 'Malkia wa pembe za ndovu' Yang Feng Glan.

_105699279_a9feacd1-fe8f-4248-a0fc-cac834ec2e66.jpg

Wahifadhi wameitaja Tanzania kama shina la uwindaji haramu wa pembe za ndovu.


  • View attachment 1026354
    • Ametoka Beijing, Bi Yang alifika Tanzania kwa mara ya kwanza katika miaka ya 70.
    • Ni mwanafunzi wa kwanza wa Kichina aliyefuzu Kiswahili.
    • Amefanya kazi kama mkalimani katika shirika la reli Tazara lililojengwa kwa usaidizi wa China.
    • Inaarifiwa kwamba baada ya ujenzi wa reli hiyo mnamo 1975 alirudi Beijing kufanya kazi katika idara ya biashara ya nje.
    • Mnamo 1998 aliamua kuanzisha biashara Tanzania.
    • Alikodisha jengo la orofa mbili Dar-es-Salaam, na kufunguwa mgahawa wa vyakula vya Kichina katika sehemu ya chini ya jengo na kufungua kampuni ya uwekezaji, Beijing Great Wall Investment, katika orofa ya juu.
  • Anashutumiwa kwa kuendeleza shughuli hiyo kwa takriban miaka 14.

    Maafisa wa serikali Tanzania walitaja kukamatwa kwa Yang Feng Glan kama ufanisi mkubwa.

    Taifa hilo la Afrika mashariki limepoteza thuluthi mbili za ndovu wake katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Tukiri kuwa mtandao wa wauwaji wa tembo na Faru ulikuwa mkubwa na mzito sawa na ule wa madawa ya kulevya, Ingawa wanaweza kuendelea kufanya maovu hayo kimyakimya, lakini pia serikali zetu za awamu zilizopita hazikwepi hii lawama, vigogo wengi walijihusisha haswa huko katika kitengo cha wanyama pori
 
Back
Top Bottom