Mjue "Mbokoo" kibaka aliyewahi kuitikisa Kigamboni-Dar kabla ya kudhibitiwa kwa mbinde na Polisi

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Alifahamika kwa jina la MBOKOO!

Alikuwa kibaka mwenye miraba minne, Ambaye alikuwa kero kubwa kwa wakazi wa Kigamboni!

Taarifa za uhalifu wake ziliwahi kuwa kero zilivyoripotiwa kila siku kwa matukio tofauti kiasi Cha kujaza REPORT BOOK (RB) ya polisi kila kuchwao akituhumiwa kuhusika na uharifu mbalimbali.
  • Inaelezwa kwamba MBOKOO alikuwa na uwezo wa kukaba hata kikundi cha watu kwa mpigo akiwa peke yake.
  • Kutokana umahiri wake wa ukabaji, inasadikika mwili wake ulikuwa hausikii maumivu anapopigwa ngumi, panga au risasi haikuwa rahisi kumuumiza
  • Alisumbua sana makachero kumkamata kutokana na mbinu zake alizotumia kuwakwepa akisaidiwa na baba yake ambae alisadikika kuwa mshirikina.
  • Kibaka MBOKOO aliwahi kuhisiwa kuhusika na tukio na uvamizi na uporaji wa hostel za wanafunzi waliokuwa wamepanga Midizini, Jambo ambalo lilizua taharuki kutokana na uporaji na ulawiti katika tukio hilo la kusikitisha!
  • Kibaka MBOKOO Aliwahi kukamatwa na kufungwa Mara kadhaa lakini alipoachiwa hakuacha tabia yake ya ukabaji
  • Aliripotiwa kukaba watu mbalimbali wakiwemo wanajeshi na kuwaumiza vibaya!
  • Inasimuliwa Kuna wanajeshi wawili walivaa hijabu usiku wa manane ili wakutane na MBOKOO Wamkamate, lakini aliwazidi nguvu hawakufanikiwa!
  • MBOKOO Alikuwa na mshipa wenye nguvu sana kiasi kwamba akikupiga ngumi utadondoka mbali mithili ya mdori uliopigwa ngumi!
  • Uharifu wa MBOKOO Uliwahi kusumbua vichwa vya makachero kutafuta namna ya kumtia nguvuni.
  • Doria ya kumsaka ilipamba Moto Sana enzi za kamishna Kova, kiasi kwamba siku moja KIBAKA. Huyo (MBOKOO) alionekana kwenye kivuko na wasamaria wema kureport haraka polisi ili akamatwe!
  • Polisi waliwahi eneo la kivuko na kuamru kisiegeshwe ili wamtie nguvuni MBOKOO Haraka iwezekanavyo!
  • Kwa jinsi alivyokuwa kero kibaka huyo, ilivutia hadi kamishna kutamani kumuona akitiwa nguvuni, lakini AMBUSHI Ile iligonga mwamba baada ya MBOKOO kujitosa baharini Kama sub Marine Ambapo alionekana kuibukia mbele na kuteka mtumbwi wa wavuvi kabla ya kutokomea Zanzibar!
  • Lipongezwe Sana Jeshi la polisi kwa mtandao mpana Ambapo inasadikika walimkamatia huko Zanzibar kwa kusaidiana na wakojani!
  • Zipo tetesi kwamba walimhasi na kumharibu kiasi Cha kupoteza nguvu zake za ukabaji .
  • Tangu hapo Kigamboni ikawa shwari na salama; mwaka unaenda wa tano Kibaka MBOKOO hasumbui ni dhahiri alidhibitiwa, maana kwa Kariba yake hakustahili kufungwa maana angesumbua hadi wafungwa.
UKWELI NI KWAMBA MBOKOO ALISTAHILI KUNYONGWA HADHARANI
Screenshot_20200605-053910.png
Screenshot_20200605-053832.png


Updates June 2021

Kibaka mbokoo baada ya kumaliza kutumikia kifungo huko Zanzibar na kutoka jera mapema mwaka huu!
Alirudi uraiani kujiunga na jamii ingawa aliendelea na ukabaji!

Jitihada za kipolisi za kumuonya na kumsihi aachane na ukabaji zilifanyika lakini hakuwa msikivu!

Baada ya jitihada za kiungwana kugonga mwamba!

Kibaka mbooko aliuwawa katika majibizano mapema Mwezi uliopita kwa kupigwa na kitu kizito wakati akiwa katika majukumu yake ya ukabaji!
 
Kuna Miaka fulani Kigamboni kulikuwa na Pati ya first year UDSM Show kabambe pia alikuwa Mwamba wa Kaskazini Joe Makini alipokuwa anaingia kuimba akajitokeza Bouncer moja hivi Kipande cha Mtu.. akaforce ati anamlinda Joe ulingoni basi kamtafaruku kiasi kakatokea na Joe akaimba nandani Joe Hakumind maana Mibouncer ikisimama ukimaliza kuimba inadai pesa... Basi masaa yakapita tukasema Tuwahi Kivuko maana that Time ikifika saa sita hivi au Saa Saba kilikuwa kinapaki hadi Alfajiri.

Si ndio tukasepa hadi ferry.. mida ya Saa saba hivi tukakuta foleni na kivuko kimekwamia pande za Kivukoni tukawait tukaona chenga wadau tukasema tupite Mbagala tuzunguke. Wadau wakaniambie nigeuze gari.. Nikamuona yule Bouncer na Jamaa mwingine wanatembea kuja upande wangu nikaingingia garini nikakanyaga Break Taa zake zikawaka Basi wale jamaa wakasimama nyuma ya gari kaumbali kama mita tano hivi wanaongea nikasema nirudi reverse nigeuke nikarudi kidogo tu kama nusu mita si wakatembea hadi kwa haraka hadi karibu na Gari wakasimama.

nikasema nitoe kichwa niwachungulie niwaambie wasogee basi yule mwembamba akaanza kusema nataka niwagonge... nikawaambie hapana nimewaona muda mrefu na kila nikitaka mpite hampiti why! Bouncer likaja juu unataka kutugonga likafungua mrango wa Gari likashika juu maana kioo kilikuwa nimekishusha nikaona hapa ishakuwa Soo nikapiga reverse kwa kasi hakuachia ule mrango basi gari likaserereka hadi kwenye mtaro nae akawa kama kazubaa nilichomoka faster garini nikakimbilia chini kule pantoni inapotia Nanga.

Yule jamaa yake Bouncer akawa ananikimbiza anishike lakini hakuweza nikaelekea hadi kwenye Maji nikazunguka senyenge zilikuwa zimeenda hadi pale kwenye nanga nikazunguka nikaenda upande wa poli kwa wavuvi na mitumbwi kibao watu wanashangaaa tu jamaa akashindwa kunifuata nikawasikia wanasema mzungukieni kwa kule nikaona sipo sehemu salama nikapandisha juu faster nikajikuta kwenye kipori chenye majani mengi sana nikasema hata nikikutana na nyoka poa tu au kama ni kwa wanajeshi poa tu...

nikachutama kimya nikawaona wamekuja maeneo ya karibu nawachora tu nikaa kama lisaa hivi washikaji wakanipigia simu wakaniambia njoo washasepa zao walidai walipwe elfu kumi wakapewa elfu tano... wakadai yule bouncer ndio zake hasira za kunyimwa posho kwa Joe Makini ndio alikuwa anataka kumalizia kwa Abiria... titokea siku hiyo niliichukia sana Kigamboni... hadi binti wa Kiarabu niliekutana nae ndio alinirejesha tena kigamboni.

I hope yule Bouncer ndio huyo jamaa kama Kadedi poa tu
 
lakini wananchi ndo tunawafuga hatutoi taarifa hadi mambo yaharibike Kama yale ya MBOKOO na SCORPION

Kwa Dar vibaka wengi wanajulikana na familia wanazotoka ila ni ngumu kuwakamata sababu ya kujuana "yule mtoto wa mzee au mama flani". Kingine ukiwaitia polisi na siri ikavuja bhasi kimbia mtaa maana wahuni watakudhuru hadharani na hakuna atakaekusaidia
 
dmkali
Mlaleo
Mmeandika story ni kama vile matukio yalifanyika last week.

Kwa nn msielzee siku/mwaka wa matukio.

Dmkali ata hajamalizi kueleza kama huyo alishakufa,alishazeeka,ni mlemavu au alifungwa maisha gerezani baada ya kuhasiwa.
story haijitoshelezi ina ongeza mlundikano wa maswali.

Ma story teller mzingatie hayo jamani.
History bila tarehe au mwezi au mwaka ni udaku.
 
Hii ndio maana polisi waliambiwa wanyang'anye silaha za hao vibaka wanaotumia silaha. Kwa wanaotumia silaha au wanaobaka Inabidi wawe wanapoteza maisha kabla ya kufika hospitali au wawe wanakatwa viganja vyote viwili.
Huko geza nasikia huyo kibaka Aliwahi kumpora mwanajeshi mstaafu siraha, ndo chanzo Cha kumsaka kwa udi na uvumba, yaan yule jamaa alikuwa jini yaan.
 
Back
Top Bottom