Ota Benga: Kijana aliyewahi kuwekwa kwaajili ya maonesho nchini Marekani

steve_shemej

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,092
1,433
Ota Benga alitekwa nyara kule ambako sasa hivi kunafahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 1904 na kupelekwa Marekani lengo likiwa nikumfanya kuwa onyesho.

Mwanahabari Pamela Newkirk, ambaye ameandika mengi kuhusu suala hilo, anaangalia matukio kadhaa ya kuficha ukweli wa kile kilichotokea.

Zaidi ya karne moja baada ya suala hilo kuangaziwa kimataifa kwa kumuonesha mwanaume kijana Mwafrika katika makazi ya nyani, Bustani ya Wanyama ya Bronx, mji wa New York hatimae imeonesha masikitiko yake.

Shirika la kuhifadhi Wanyama pori limeomba msamaha kwa onesho la mwaka 1906 la kumuonesha Ota Benga, mzaliwa wa Congo, hatua iliyokuja baada ya maandamano duniani yaliyosababishwa na video inayoonesha mauaji ya George Floyd na kuanza tena kuangazia ubaguzi unaotokea Marekani.

Wakati Marekani inakumbana na maandamano hayo, Cristian Samper, Rais wa chama cha uhifadhi wa wanyama pori, alisema ni muhimu "kuakisi historia ya hifadhi hiyo na ubaguzi wa rangi katika taasisi zetu".

Aliapa kwamba bustani ya wanyama ya Bronx, itahakikisha kwamba inakuwa na uwazi kuhusu kile kilichogonga vichwa vya habari kote Ulaya na Marekani kuanzia Septemba 9, 1906 siku moja baada ya Ota Benga kuoneshwa kwenye onesho hadi alipoondolewa kwenye bustani hiyo. Septemba 28, 1906.

'Alikuwa mfanyakazi wa hifadhi hiyo'

Badala ya kujikita kwenye mafunzo waliopata, Shirika hilo la uhifadhi wa wanyama pori limejihusisha na walivyoficha ukweli kwa karne nzima kipindi ambacho lilishindwa kuweka sawa au kuzungumzia kile ambacho hasa kilikuwa kimetokea kwa mwanaume huyo mweusi.

Mapema mwaka wa 1906 barua kutoka kwa hifadhi hiyo inaonesha kwamba wakati ukosoaji wa kitendo hicho unaendelea, maafisa waliamua kuanzisha taarifa za uongo kwamba Ota Benga alikuwa mfanyakazi wa hifadhi hiyo.

Ota Benga alikuwa nani?

Alikamatwa Machi 1904 na mfanyabiashara wa Marekani Samuel Verner kutoka kule ambako kulikuwa kunafahamika kama Congo ya Ubelgiji. Umri wake haujulikani, pengine alikuwa na miaka 12 au 13

Alisafirishwa kwa meli hadi New Orleans na baadae mwaka huo aliwekwa kwenye maonesho ya Dunia huko St Loius na vijana wengine wanane

Maonesho hayo yaliendelea hadi miezi ya baridi ambapo kundi hilo halikupewa nguo za kujikinga na wala malazi.

September 1906, aliwekwa kwenye maonesho kwa siku 20 katika bustani ya wanyama ya Bronx huko New York na kuwa kivutio cha wengi kufika katika eneo hilo.

Ghadhabu kutoka kwa mawaziri wa Kikristo ilitamatisha kushikiliwa kwake na alihamishwa hadi hifadhi ya yatima weusi ya Howard New York iliyokuwa inasimamiwa na mchungaji Mmarekani Mweusi James H Gordon.

Januari 1910 alienda mji wa Lynchburg. Seminari ya kitheolojia kwa wanafunzi weusi huko Virginia.

Huko alifunza wavulana waliokuwa jirani namna ya kuwinda na uvuvi pamona na kuwasimulia kilichomtokea nyumbani.

Baadae alisemekana kwamba amepata ugonjwa wa sonona kutokana na kutamani nyumbani kwao na Machi 1916 akajipiga risasi kwa bunduki ambayo alikuwa ameificha. Inadhaniwa kwamba wakati huo alikuwa na umri wa karibu miaka 25.

_114113571_otabenga976.jpeg
 
Anaitwa Ota Benga alitekwa ili akawe maonyesho huko marekan.https://www.bbc.com/swahili/habari-53945853?xtor=CS3-33-%5Bwsswahili%7EC%7EA41B40C45D38E38F39G38otabenga%7ESwahili_otabenga_Faceboock_Traffic_Multi_C%5D-%5BFacebook%5D-%5B6211068770541%5D-%5B6211068770341%5D
 
IMG_1641.jpg

#Elimika

Mfahamu kwa Ufupi OTA BENGA,

Ni kijana mdogo wa Mbuti huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zamani ikiitwa Zaire,

Alizaliwa mwaka 1883 huko Kwenye misitu ya Ituri nchini Congo, Kisha baada ya kukua kidogo Akatekwa na Wazungu na Kupelekwa New York Marekani,

Kule Marekani akapelekwa kwenye hifadhi ya wanyama iitwayo BRONX ZOO ( Aliwekwa pamoja na Nyani) Akawa kivutio cha mamia ya watalii, Na hii ilikuwa September 1906,

Benga Alifanyiwa majaribio Mengi ya kiutafiti kama mnyama wa kawaida ikiwa ni pamoja na Kuchongwa meno kama anavyoonekana pichani,

Ilipofika mwaka 1910 mpaka 1914 kwa msaada wa Wamarekani weusi Benga alijitahidi kupambana ili arudi kwao Afrika lakini ikishindikana kwani wakati huo vita ya I ya dunia ilikua imepamba moto,

Hatimaye mwaka 1916 OTA BENGA alifariki kwa Kujinyonga baada ya kupitia kipindi kigumu cha msongo wa mawazo.

#Jifunze #Elimika #Furahi
IMG_1642.jpg
 
Inasikitisha sana hii, binadamu mwenzao kumfanya mtu wa maonyesho
lehmann_22741u.web_01c8ac7cc3b849e525e370bc51344120.jpg
 
Back
Top Bottom