Mjue Kanali Seif Bakari, ivumayo haidumu, asubuhi imekaribia

Sasa umkute mjukuu wake twitter anavyojifanya ametoka ukoo wa watakatifu kumbe ni hamna kitu.
 
..kuna watu wameuawa Znz wakati wa utawala wa Shekhe Karume na mpaka leo haijulikani walipozikwa.

..baadhi ya wanaotuhumiwa kuwapoteza Wazanzibari wenzao ni Col.Seif Bakari pamoja na wenzake waliokuwa ktk vyombo vya ulinzi vya Znz baada ya Mapinduzi.
 
Nnauye alikuwa kwanza Mwenyekiti wa TANU Youth League( miska ya 70 mwanzoni), halafu mkuu wa Wilaya Bagamoyo halafu RC Singida. Katikati ya miaka ya 70 ndiyo alikuwa mwalimu wa siasa jeshini.
 
Use your brain mkuu,lets say babu yako akiwa" mwiz"i wewe mjukuu inakuhusu nini mpaka usiwe "police"?
Alaf Moral authority wewe unaielewaje?
Hivi unafahamu hivi vitu spiritually huwa vinaenda vizazi hadi vizazi au haufahamu ukiua na mwanao ataua tuu ipo hivyo kama sio mwanao basi katika damu yako yupo ataifanya hiyo dhambi.

Je mhusika ameshawahi hata kusema babuye was wrong maana asiwe busy kutoa vibanzi wakati kuna maboriti ya hatari kwenye macho yake.
 
“Fedha ya kichwa cha Malkia si yako na usiniulize, labda niulize juu ya hii (sh.) yenye picha ya kichwa chako.”
:D nimecheka sana.... Alikuwa anajiamini sana.... Hawa tuliokuwa nao visiwani sijui kama wanaweza haya!
 
Kawaulize watu wa Zanzibar ndio watakupa majibu kama alikua poa. Jamaa kaua sana watu kihuni huni tu
Tatizo la hawa watu, wakiwa na watu wao wa karibu wanakuwa wakarimu na wacheshi sana. Mpaka ukiambiwa huyu jamaa muuaji unakuwa kama huamini.

Kwa sababu mimi nilivyomuona katika mazingira rafiki alikuwa mcheshi na mkarimu sana inakuwa vigumu kuamini aliua watu bila kituo.

Lakini sijawahi kumuona katika mazingira yake ya kikazi akiindoa mazingira rarfiki.

Hata Joseph Stalin kuna watu walisema alikuwa mtu poa sana, lakini kikazi alikuwa anaua watu kama nzi.
 
Kikosi cha Usalama wa Taifa chini ya Kanali Seif Bakari, kilichopewa jina la Viwavi Jeshi, kilichofunzwa Ujerumani Mashariki kikaiva kwa mbinu za utesi na mauaji, kilipewa mamlaka ya kukamata, kutesa, kutia kizuizini na hata kuuwa bila mashitaka
Haya mambo kama ya State Research Bureau ya Iddi Amin, Go with him to where he sleeps
 
Unamjua mtu anaitwa Kanali Seif Bakari? Huyu ndie alikuwa kitendea kazi mhimu cha Mzee Karume katika utawala wake. Mathalani, Kiburi cha madaraka kilipokolea, Karume alianza kuwa mwiba kwa Mwl. Nyerere, hasa juu ya Muungano. Kwa mfano, alimkatalia Mwl. Nyerere kwa lugha ya dharau na bezo juu ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha kutumika Zanzibar. Na kuhusu akiba ya fedha za kigeni ya Zanzibar iliyofikia dola milioni 80 mwaka 1972, alimpa Mwl. Nyerere onyo kali, asithubutu kuitolea macho, akamwambia: “Fedha ya kichwa cha Malkia si yako na usiniulize, labda niulize juu ya hii (sh.) yenye picha ya kichwa chako.” Na kuhusu Muungano, Karume alianza kuchoka nao. Siku moja alisema, “Muungano ni kama koti tu; likikubana unalivua.”

Ufa huu kati ya viongozi hao wawili juu ya Muungano, ndio uliosababisha Kamati ya Kupendekeza Katiba isiundwe na Bunge la Katiba lisiteuliwe ndani ya muda wa mwaka mmoja tangu Muungano, kama ilivyotakiwa chini ya Mkataba wa Muungano wa Sheria ya Muungano ya mwaka 1964. Wadadisi wa mambo ya siasa wanakubaliana kuwa, kama Karume angeendelea kutawala miaka kadhaa baada ya mwaka 1972, Muungano ungefikia kikomo kwa njia ya kutisha na kusikitisha.

Kufikia mwaka 1972, upinzani kwa Serikali ya Karume ulikwisha chukua harakati za uasi wa umma, chini kwa chini, kwa mara ya kwanza tangu Hanga na wenzake wanyongwe mwaka 1969. Kwa vigezo vyovyote vile vya utawala na uongozi, Karume alitawala kwa mkono wa chuma cha pua. Alitawala kiimla (utawala mkavu wa unyama) katika nyanja zote za maisha ya Wazanzibari kisiasa, kiuchumi na kijamii!―, pia alikuwa kero kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwl. Nyerere dhidi ya Muungano.

Kwa kusema haya, kitabu hiki hakitafsiri kwamba Karume hakutenda mema kwa Zanzibar na kwa Wazanzibari, bali kinajaribu kutafiti tu kuona ni mazingira na sababu zipi zilizochochea na kuharakisha kuuawa kwake. Ama huenda kati ya sababu za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimuungano ndizo zilizoharakisha kifo chake. Tunajua kwa mfano, kwa baadhi ya Wazanzibari, Karume alitawala kikatili, mzandiki asiye na huruma wala hakujua kusamehe. Kwa upande mwingine, alikuwa na sifa za pekee nzuri kama kiongozi na binadamu; alikuwa mhimili na mtetezi wa Waafrika wa Kizanzibari na hakuyumbishwa na siasa za migogoro Visiwani. Alikuwa mwenye fikra zenye kujitegemea, alifanya maamuzi yake bila woga wala kuhofia matokeo; alikuwa kiongozi mwenye kuthubutu na mwenye kujituma.

Licha ya Karume kuitawala Zanzibar kwa mkono wa chuma cha pua, na namna alivyowaengua wote aliodhani hawakuwa upande wake ama kwa kuwahamishia kwenye Serikali ya Muungano, ama kwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha, jamii ya Kiarabu wasio Wazanzibari, iliamriwa kuondoka, na wale Waarabu raia waliobaki, waliishi chini ya jicho kali la Serikali; waliweza kukamatwa, kama Wazanzibari wengine na kutiwa kizuizini bila kufunguliwa mashitaka. Walifanyiwa jinsi serikali ilivyofikiri inafaa; mashamba na mali zao zilitaifishwa bila kufidiwa. Wapo waliohukumiwa na Mahakama ya wananchi, kifungo na kuchapwa viboko. Kuonesha kwamba Serikali ya Karume haikuwa ya mchezo mchezo, akaionya jamii ya Ki-Athnasheri wa Kiajemi kwamba kama wangeendelea kuleta mgogoro, wangefukuzwa wote Zanzibar licha ya kuwa raia.

Karume alitangaza utawala wa chama kimoja cha ASP na kuamrisha kila Mzanzibari mtu mzima, kuwa mwanachama. Kila familia ilitakiwa kutundika picha ya Karume nyumbani, na ambaye angekaidi, alikuwa amefanya kosa la jinai lenye kustahili adhabu kali. Kikosi cha Usalama wa Taifa chini ya Kanali Seif Bakari, kilichopewa jina la Viwavi Jeshi, kilichofunzwa Ujerumani Mashariki kikaiva kwa mbinu za utesi na mauaji, kilipewa mamlaka ya kukamata, kutesa, kutia kizuizini na hata kuuwa bila mashitaka (yaani sheria iliwapa haki ya kua kama haki nyingine). Yeyote aliyelalamika, hata juu ya upungufu wa chakula tu, aliitwa adui (au mchochozi kama ilivyo sasa) wa Mapinduzi na hivyo mhaini. Enzi hizo, nduguyo akigongewa mlango usiku na kutakiwa kwa mahojiano na Serikali, usingemwona tena milele na milele.

Wakati wa Karume, wakati wa mkono wa chuma, hapakuwa na utawala wa Sheria wala Katiba. Amri za Rais ndizo zilizotawala nchi. Mapema mwaka 1966, mfumo wa mahakama wa kawaida ulipigwa marufuku; na Oktoba 1966, Rais alijipa madaraka ya kuteua mahakama maalumu za watu wasiozidi kumi na wanne (14), wenye mamlaka ya kusikiliza kesi za makosa ya kisiasa kama vile uhaini, uhujumu uchumi na wizi wa mali ya umma. Mahakama hizi hazikufungwa na kanuni zozote katika kusikiliza kesi; huduma za kisheria kwa watuhumiwa zilifutwa na mawakili kupigwa marufuku Zanzibar. Upande wa mashitaka ndio uliokuwa upande huo huo wa utetezi.

Yaani, mwendesha mashtaka wa serikali alipomaliza kuwasilisha mashtaka dhidi ya mtuhumiwa, aligeuka kuwa mtetezi wa mtuhumiwa huyo huyo. Ilikuwa vichekesho vya kutamausha. Mahakama hizi zilipewa uwezo wa kutoa hukumu ya kifo, iwapo waliona adhabu nyingine ni nyepesi kwa mtuhumiwa. Mwaka huo huo (1966), Baraza la Mapinduzi lilipiga marufuku haki ya kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki [EACA] na rufaa zote zikawa kwa Rais Karume pekee. Mwaka 1970, Karume alipitisha amri ya kuanzishwa mahakama (za kienyeji) za watu watatu. Mahakimu wapya wa mahakama hizo waliteuliwa na Karume mwenyewe kutoka miongoni mwa makada wa ASP. Moja ya sifa ya kuteuliwa ni kutokuwa msomi wa sheria, na ikiwezekana uwe hujui kusoma na kuandika....

Where the hell is this book? Haya ni madini ya nadra kupatikana.
 
Na si lazima ujue kila Kitu Ndugu na ndiyo maana huwa mnaambiwa kuna ambayo mnapaswa kuyajua ila mengine hampaswi pia muwe mnayajua.

Cha kushangaza hakuna ukweli unaofichwa chini ya kapeti usijulikane. Nia hasa ni kujifunza ili kuelewa namna bora ya kuendesha maisha yetu kwa manufaa ya vizazi vyetu vyote.
Sio busara kukataa elimu maana gharama yake ni kubwa mno. Tutafeli kwa kufanya makosa yale yale ambayo wenzetu walifanya na yakawarudi mazima
 
Huu ndio uzuri wa historia naamini bwana huyu akiondoka madarakani tutaambiwa mengi Sana wanaomsifu Leo ndio watakaotuhabarisha mbivu na mbichi alizozitenda wakati wake hapo ndipo tutakapojua Ben alikuwa mifupa siku nyingi au atakuwa mzee mwenye mvi atakaeachiwa huru huko mbeleni. Muda ni mwalimu mzuri.

 
sasa mtu wa namna hii huwa kwanini inatengwa siku ya kumkumbuka badala ya siku ya kupiga viboko kaburi lake! wajerman hawajawai kutenga siku ya hitler kwa sabab hizi hizi.
 
Back
Top Bottom