Mjue Kanali Nyamburi Mashauri, ADC wa Rais Samia Suluhu

Zama mpya na mambo mapya. Samia Suluhu Hassan ndio Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kula kiapo leo, akichukua nafasi ya Hayati John Pombe Magufuli.

Baada ya kula kiapo, Rais Samia Suluhu (Double S) tukamuona mpambe mpya nyuma ya Rais Samia, kinyume na ilivyozoeleka na wengi, mpambe akawa mwanamama.

Wengi hawamfahamu, mpambe huyu anaitwa Nyamburi Mashauri ambaye ni Kanali kutoka JWTZ na nimepenyezewa kuwa ni mtu makini sana kwenye utendaji wa kazi hivyo Rais wetu amepata msaidizi sahihi.

Kanali Nyamburi Mashauri anachukua nafasi ya Kanali Bernard Mlungwa ambaye alikuwa mpambe wa Hayati Rais Magufuli.

Nikutakie utendaji mzuri wa kazi Kanali Nyamburi Mashauri katika jukumu lako kubwa la kumsaidia Rais wetu mpendwa Samia Suluhu.

Naona huyu mama wa kikurya ameendana vyema sana na Hangaya.
 
Back
Top Bottom