Mjue Kanali Ali Mahfoudh

Kanali Ali Mahfoudh ni Mmoja wa Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ waliotajika sana kwa Miaka hii 50 ya Jeshi letu hili, viza Ushupavu, Ushujaa na Umahiri wake Vitani zikielezewa kwa Vijana na kuwashajiisha wengi kutamani kuingia Jeshini kufuata njia yake njema ya Utumishi wa Kutukuka, Kujituma, Weledi, Ushupavu na Ushujaa.

Akifanya kazi njema ya Ukombozi tokea Mapinduzi ya Zanzibar ambapo vipawa vyake na Umahiri wake Jeshini lionekana mwanzoni tu, japo kwa kuwa naye alisomea Ukomandoo wa Kijeshi Nchini Cuba alihusishwa zaidi na kundi la Makomredi wa Umma Party chini ya Profesa Abdulrahman Mohammed Babu na Mzee Ali Sultan Issa.

Mara baada ya Mapinduzi na kuundwa Muungano wa Nchi za Tanganyika na Zanzibar, Kanali Ali Mahfoudh na wengi wa Makomredi wenziwe waliingizwa kwenye Serikali ya Muungano na kuondolewa kabisa Zanzibar kwa kukhofiwa kwa Ujemedari wao, Usomi wao na "Utata" wao.

Kanali Ali Mahfoudh alikuwa Mkurugenzi wa Operesheni wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ kuanzia Mwaka 1964 alipohamishiwa Bara mpaka Mwaka 1972. Mwanajeshi huyu ni mmoja wa askari waliopata umaarufu sana katika JWTZ kwa utumishi wao, Wengi wamesikia jina lake, lakini wachache wamepata kumuona kwa sura na hao waliobahatika kumuona wakikiri kwamba "alikuwa na sura nzuri" lakini alikuwa Shupavu hasa.

Kanali Mahfoudh alipata Umaarufu zaidi kati ya Mwaka 1964 - 1972 katika kuvisaidia Vyama vya Ukombozi vya Afrika kama FRELIMO, ZANU, ZAPU na MPLA katika vita vyao vya Msituni vya Ukombozi wa Nchi zao, na pia akitajwa kuwa ndiye aliyeongoza Kikosi cha JWTZ katika RABSHA moja Maarufu dhidi ya Uchokozi wa Rais Kamuzu Banda wa Malawi.

Wakati wa Mapambano ya Frelimo kudai Uhuru kutoka kwa Waremo Kanali Mahfoudh alijichimbia Nachingwea akiwasapoti Majemedari wa Msumbiji Albarto Sipande na Raymundu Pasinuwapa katika ukombozi wa nchi hiyo kutoka Mikononi mwa Wakoloni hao waonevu.

Kati ya Mwaka 1972 mpaka mwaka 1978 aliwekwa kizuizini Jijini Dar es salaam kwa Tuhuma za kuhusika na Mauaji ya Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Makamo wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheikh Abedi Amani Karume na akahukumiwa Kifo katika Kesi ambayo iliendeshwa Zanzibar bila yeye kuwepo.

Wengine waliotiwa Kizuizini pamoja naye ni Profesa Abdulrahman Mohammed Babu, Tahir Ali Salim, Hashil Seif Hashil, Salim Saleh Salim, Ali Yusuf Baalawi, Hemed Hilal Mohammed, Suleiman Mohammed Abdullah, Amour Mohammed Durgheish, Ahmed Mohammed Habib, Haji Omari Haji, Saleh Abdallah, Abdallah Juma Khamis, Ali Salim Hafidh, Shaaban Salim Mbarak, Badru Said, Ali Mohammed Ali na Abdulaziz Abdulkadir Ahmed, Makomredi wengine kama Ali Sultan Issa, Sharifu Ahmad Badawy Qullatein na wenziwao walishikiliwa Zanzibar.

Baada ya Mbinyo mkali wa Shirika la Haki za Binaadam la Amnesty International na Mataifa ya Kigeni juu ya kushikiliwa kwao, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Julius Kambarage Nyerere alitoa amri ya kuachiwa kwa Kanali Ali Mahfoudh na Makomredi wenzie Tarehe 26, Mwezi Aprili Mwaka 1972.

Mara baada ya kutolewa Gerezani Kanali Ali Mahfoudh alichukuliwa na Serikali ya Msumbiji kwa Ombi Maalum la Rais Samora Machel kwa kuthamini mchango ambao Nguli huyu alitoa kwa Nchi hiyo, japo ikidaiwa kuwa kulikuwa na Makubaliano Maalum ya Kuhakikisha Kanali Ali Mahfoudh hakanyagi tena Ardhi ya Tanzania.

Nchini Msumbiji Kanali Mahfoudh alikuwa Mshauri Mkuu wa Mambo ya Kijeshi wa Rais Samora Machel na kwa kiasi kikubwa ndiye anayetajwa kuisaidia Msumbiji kimbinu kupambana na Waasi wa Renamo waliokuwa wakipewa Msaada wa Mbinu za Kijeshi, Silaha na Fedha kwa Dhahiri na Makaburu wa Afrika ya Kusini pamoja na Mataifa mengi makubwa ya Magharibi. Kwa kutambua Ushujaa na Ujuzi wa Mbinu mbalimbali za Vita wa Kanali Ali Mahfoudh, Makaburu walijaribu Mara tatu kutaka kumuua lakini Mara zote walishindwa katika Majaribio yao hayo.

Kanali Ali Mahfoudh aliendelea kuishi Msumbiji hata mara baada ya kustaafu kazi yake ya Ushauri wa Mambo ya Kijeshi kwa Serikali ya Msumbiji, Baadaye alijiingiza kwenye Biashara, mara nyingi alikuwa Akipatikana katika Klabu ya Watanznia iliyokuwa katika Jengo la Ubalozi wa Tanzania Nchini Msumbiji ambalo tulipewa zawadi na Serikali ya Msumbiji kwa msaada wetu kwao. Hata alipofariki Dunia Nchini humo bado Kanali Ali Mahfoudh hakurudishwa Tanzania na alizikwa Katika Makaburi ya Mashujaa (Heroes Cemetary) Jijini Maputo huko huko Msumbiji.

Aliyekuwa Mke wa Kanali Ali Mahfoudh, Mama Naila Majid Jiddawi aliendelea kubaki Tanzania ambapo baadaye naye alikuja kuwa Mtu Maarufu na Nguli mno katika Siasa za Tanzania hasa kwa Upande wa Zanzibar, ambapo alipambana sana katika siasa kupitia Vyama vya CUF na NCCR Mageuzi (aliwahi kuwa Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama hicho) lakini naye kama Mumewe alikutana na Rungu la Serikali kwa kufanyiwa Hujuma za wazi katika Biashara zake kiasi cha kufikia Mpaka kuchomewa Hoteli anayoimiliki.

Wakati Rais Amani Abedi Amani Karume akiwa Madarakani alishutumiwa sana kwa kutoa Msamaha kwa Wafungwa ambao walifungwa kwa kosa la kuchoma hoteli ya Mama Naila Majid Jidawwi, ikionekana ni kama vile Serikali ilikuwa inatoa Msamaha kwa watu ambao ilidhanika kwamba iliwatuma wachome Hoteli ya Mama huyu.

Mama Naila Majid Jiddawi bado yuko hai huko Zanzibar, akifarijika kwa Mtoto wake mwema aliyefanikiwa kuzaa katika ndoa yake na Kanali Ali Mahafoudh, Mtoto huyo anaitwa Mahfoudh au kwa jina Maarufu "CHE" Mahfoudh kwa kuwa kama baba yake naye kafanana sana na Mwanamapinduzi Enersto "Che" Guvara wa Amerika ya Kusini.

Pichani ni Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akimvisha medali ya Ushujaa wa Vita vya Ukombozi wa Nchi za Afrika Mwanajeshi Mkakamavu, Komandoo aliyeogopwa na Maadui wa Tanzania na Afrika na Mpiganaji Shupavu aliyejitolea kupigania Ukombozi, Kanali Ali mahfoudh, Picha hii ilipigwa mwaka 1969.View attachment 502350
REKEBISHA KAMA ALIWEKWA KIZUIZIN MWAKA 1978 ALIACHIWAJE TENA MWAKA 1972? AMBAO NDIYO KARUME ALIUAWA?
 
Aliyekuwa Mke wa Kanali Ali Mahfoudh, Mama Naila Majid Jiddawi aliendelea kubaki Tanzania ambapo baadaye naye alikuja kuwa Mtu Maarufu na Nguli mno katika Siasa za Tanzania hasa kwa Upande wa Zanzibar, ambapo alipambana sana katika siasa kupitia Vyama vya CUF na NCCR Mageuzi (aliwahi kuwa Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama hicho) lakini naye kama Mumewe alikutana na Rungu la Serikali kwa kufanyiwa Hujuma za wazi katika Biashara zake kiasi cha kufikia Mpaka kuchomewa Hoteli anayoimiliki.
Mama Naila Majid Jiddawi yupo na ingependeza waandishi wa habari wakafanya mahojiano naye juu ya mtu huyu maarufu barani Africa aliye mZanzibari na mtanzania Colonel Mahfoudh

 
Aliwekwa kizuizini halafu baadae anaonekana aliachiwa toka gerezani

Hili pia lirekebishwe kuweka kumbukumbu sawa, kuna tofauti ya kizuizi na gereza
 
His son too was quite a lookie. Mahfoudh Ali Mahfoudh. Very silly, so much fun to hang out with and had beautiful dogs way back like a decade ago.
Mmmh Kuna kitu hapa sio kwa hizo masifa ulizompatia. 😜😜
 
Mfumo Galatia noma...ha ha haaa! By the way mkuu, hii umeiandika mwenyewe au ni Sheikh Said Mohammed? Kama ni wewe hongera japo sifa zimezidi mno dah!
Sifa hazijazidi huyu jamaa alikuwa ni komandoo wa uhakika aliyekuwa trained Cuba (hata Wamarekani kwanza walidhani ni Wacuba - hiyo ni kwa mujibu wa de-classified reports za CIA). Kumbuka enzi zile hakikuwepo kikosi cha makomandoo. Na ndiyo maana Nyerere alimpeleka Msumbiji kwenda kusaidiana na Frelimo wakati wa ukombozi.
 
Kumbe Best wewe watokea Zenji?
πŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈ
 
πŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈ
Kimbia taratibu...wengine tuna magonjwa ya kikubwa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom