mjue jeetu patel mtanzania anaeiendesha serikali ya tanzania atakavyo

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,050
amka2.gif

MAKAMAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imemruhusu mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya wizi wa sh bilioni 3.3 za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jayantkumar Chandubhai Patel, maarufu Jeetu Patel, kutembea nje ya Dar es Salaam.
Uamuzi huo ulitolewa jana na kiongozi wa jopo la mahakimu wakazi, Richard Kabate, baada ya mtuhumiwa huyo kupitia wakili wake, Mabere Marando, kuwasilisha maombi hayo.
Awali akiwasilisha ombi hilo, Marando alisema mtuhumiwa huyo anaomba ruhusa ya Aprili mosi na 14 mwaka huu, kwenda mikoa ya Mogogoro, Mwanza, Arusha, Zanzibar, Pwani, Kibaha na Tabora pamoja na Bagamoyo kwa ajili ya kuangalia shughuli zake.
“Kutokana na mtuhumiwa kuwa na shughuli nyingine katika mikoa mbalimbali anaomba ruhusa ya mahakama kwenda mikoa hiyo kwa ajili ya kwenda kusimamia shughuli zao, kwani kwa kuwa Dar es Salaam pekee shughuli zao hizo zitakwama,” alidai wakili Marando.
Aidha, wakili Marando aliomba ruhusa pia kwa mtuhumiwa namba tatu Amit Nandy, katika tarehe hizo kwenda Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusimamia shughuli zake. Marando pia aliwasilisha maombi ya mshitakiwa namba mbili, Ketan Chohan, mahakamani hapo kwenda mikoa ya Morogoro na Arusha kwa ajili ya kusimamia miradi yake. Washitakiwa hao kwa pamoja wameruhusiwa kwenda katika mikoa hiyo na kutakiwa kuhudhuria vikao vya mahakama vya kesi yao.


h.sep3.gif


juu
 
Lakini ni haki yao....kuomba na kupewa ruhusa hizo....kweli wana bishara nyingi sana mikoani.....nakumbuka hata kina alwx masawe walizuiwa wakaomba wakapewa....kesi za EPA siasa zimetawala naisubiri sana hukumu ya kesi ya maranda.......
 
lakini ni haki yao....kuomba na kupewa ruhusa hizo....kweli wana bishara nyingi sana mikoani.....nakumbuka hata kina alwx masawe walizuiwa wakaomba wakapewa....kesi za epa siasa zimetawala naisubiri sana hukumu ya kesi ya maranda.......


akuna kesi hata moja ya epa wahujumu waatashindwa nakuahikishia hilo mungu atupe uhai...
Mawakili wenyewe wanacheka jinsi kesi zilivyofunguliwa anyway tusiwape majibu majaji hii ni pesa naitaji kulipwa wacha tuwasubiri
 
Back
Top Bottom