Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,955
- 22,131
MAKAMAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imemruhusu mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya wizi wa sh bilioni 3.3 za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jayantkumar Chandubhai Patel, maarufu Jeetu Patel, kutembea nje ya Dar es Salaam.
Uamuzi huo ulitolewa jana na kiongozi wa jopo la mahakimu wakazi, Richard Kabate, baada ya mtuhumiwa huyo kupitia wakili wake, Mabere Marando, kuwasilisha maombi hayo.
Awali akiwasilisha ombi hilo, Marando alisema mtuhumiwa huyo anaomba ruhusa ya Aprili mosi na 14 mwaka huu, kwenda mikoa ya Mogogoro, Mwanza, Arusha, Zanzibar, Pwani, Kibaha na Tabora pamoja na Bagamoyo kwa ajili ya kuangalia shughuli zake.
Kutokana na mtuhumiwa kuwa na shughuli nyingine katika mikoa mbalimbali anaomba ruhusa ya mahakama kwenda mikoa hiyo kwa ajili ya kwenda kusimamia shughuli zao, kwani kwa kuwa Dar es Salaam pekee shughuli zao hizo zitakwama, alidai wakili Marando.
Aidha, wakili Marando aliomba ruhusa pia kwa mtuhumiwa namba tatu Amit Nandy, katika tarehe hizo kwenda Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusimamia shughuli zake. Marando pia aliwasilisha maombi ya mshitakiwa namba mbili, Ketan Chohan, mahakamani hapo kwenda mikoa ya Morogoro na Arusha kwa ajili ya kusimamia miradi yake. Washitakiwa hao kwa pamoja wameruhusiwa kwenda katika mikoa hiyo na kutakiwa kuhudhuria vikao vya mahakama vya kesi yao.